Kuishi Ukiwa umepiga magoti... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuishi Ukiwa umepiga magoti...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee Mwanakijiji, Sep 27, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Neno la Leo: Ni bora kufa nikiwa nimesimama kuliko niishi nikiwa nimepiga magoti!

  Rafiki yangu mmoja baada ya kunyanyaswa sana na bosi wake aliamua jana kuacha kazi. Angeweza kuendelea na kazi yake kama angebembeleza na kuomba msamaha na kujishusha (Wamarekani wanaita 'kissing .ss'). Alipoitwa kupewa nafasi ya kuomba radhi hakuwa tayari kwani aliamini hana makosa yoyote ni mgongano wa siku nyingi wa kati yake na bosi wake (ambaye walishawahi kuwa pamoja kazini na mwenye connection (schoolmate) na mkuu wa idara). Rafiki yangu akawaambia "kwaheri". Nilipomdodosa kwanini asingekubali tu kubembeleza ili watoto wasife njaa ndio akatoa kauli hiyo.. imenikaa kichwani na kunifikirisha.

  https://www.facebook.com/mwanakijiji
   
 2. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mkuu tupo wengi wajasiriali tuliokimbia mambo kama hayo
  unakuta wewe ni kichwa hapo ofisini na boss anajua ukiwepo
  hata akisafiri hakiariki kitu ILA siku mwanao aumwe umpitishe hospital
  na kuchelewa kufika ofisi waswahili wana sema KITANUKA!
  MKARIBISHE MTAANI. mmkjj uko kimya sana mkuu:yo:
   
 3. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  mlango huu ukifungwa kwa imani MUNGUatafungua njia yakutokea kama anamwamini
  Ni bora kufa nikiwa nimesimama kuliko niishi nikiwa nimepiga magoti!
   
 4. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  Its all about a means to an end.., na kama kuna alternatives.., sio vibaya kupiga magoti leo na kesho kusimama milele..

  after all Baniani Mbaya Kiatu Chake Dawa...

  LAKINI
  [​IMG]

  KUMBUKA...

  Tofautisha Ujasiri na Ujinga sababu kuacha kazi watoto wakalala njaa kwa kujiita jasiri ni ujinga..
   
 5. mshana jr

  mshana jr JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2012
  Joined: Aug 19, 2012
  Messages: 81,481
  Likes Received: 81,615
  Trophy Points: 280
  Heri nilale njaa kuliko kuomba msamaha bila Kosa nasimamia heshima yangu na micmamo yangu ! Bravo mzee !
   
 6. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2012
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Sasa ujasiri unaupima kwa matokeo yake au kwa tunu uliyoisimamia?? Huwezi kuwa jasiri halafu usilipe gharama iwayo yoyote. Ukiona unaogopa kuipigania tunu unayoithamini basi ujue wewe si jasiri. Hii ni tofauti sana na hicho unachoita "ujinga"
   
 7. Root

  Root JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,309
  Likes Received: 13,017
  Trophy Points: 280
  nimeipata hii
   
 8. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #8
  Sep 28, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  Hata kuomba msamaha (swallow your pride) ni ujasiri.

  Kuangaika kujishusha kwa muda ili wanaokuzunguka waweze ku-survive (sacrifice ni ujasiri)

  Kuacha the one alternative kabla haujapata nyingine just because of pride si ujasiri bali ni pride (all in all its a means to an end) na kupima pros and cons za uamuzi wako
   
 9. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #9
  Sep 28, 2012
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hicho ni Kibuli...Mwambie kwamba jasiri angesema, naomba msamaha mdomoni lakini ndani ya nafsi yangu msimamo wangu hupo pale pale. Unakumbuka mtoto alimwambia mwalimu wake kwamba sawa mwalimu, napiga magoti lakini ndani ya nafsi yangu ningali nimesimama...jamaa yako duh yeye ni fulu 'kuzira'
   
 10. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Uombe msamaha mahali pasipo na kosa? Huo si ujasiri, ni KUJIKOMBA, kujidhalilisha na kuonyesha ujinga wa hali ya juu. Unless uwe incompetent, which means hata kazi yenyewe utakuwa ulipewa tu bila kustahili.
   
 11. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #11
  Sep 28, 2012
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Kuomba msamaha bila kuwa umefanya kosa ni ujinga na unafiki. Huyo bwana hakuomba msamaha kwa sababu aliona hakuwa na kosa lolote alilolifanya zaidi kunyanyaswa tu na huyo bosi.
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  Sep 28, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,336
  Likes Received: 1,801
  Trophy Points: 280
  Amesema watoto wake watalala njaa? And even though, there is 80/20 rule which governs the world. 20% ndio wanaofanya kazi kubwa na 80% ni wafuata mkumbo tu. Kwahiyo kila mtu ana side yake kwenye hixo two sides bila kuitana wajinga.
   
 13. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #13
  Sep 28, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  Wakuu naomba turudi tena kwenye maneno ya mleta mada sio maneno yangu.....


  Just Ask YourSelf
  Does it make a Bigger Man to Fight or Walk Away / Give in....
  "Nilipomdodosa kwanini asingekubali tu kubembeleza ili watoto wasife njaa ndio akatoa kauli hiyo..."


  From the above scenario utaona kwamba watoto are at a stake.., well-being ya watoto na familia.., sasa ngoja nikupe mfano.., kama wewe ni houseboy wa muhindi kila siku anakutukana na kukutesa na bado haujapata alternative ya kwenda pengine kufanya kazi.., ni kweli inakuuma na unapata hasira ndani kwa ndani je ni rahisi kumpiga muhindi na kuondoka au ni vigumu zaidi kuvumilia mateso unayopata for well-being ya familia yako (sacrife your happiness na pride yako)...

  Na je itakuwa ujinga au ujasiri kuondoka pale na kumpa muhindi vidonge vyake na kwa action yako ku-affect familia yako ?

  Kumbuka busara ni kutafuta kazi nyingine / alternative na kuondoka because sometimes your better off alive than dead (sacrificing yourself and your pride for the better future ya familia yako) and that takes guts
   
 14. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #14
  Sep 28, 2012
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mkuu, ukisoma hiyo habari ni kuwa boss wa jamaa alikuwa anamnyanyasa. Na jamaa aliamua kuacha kazi kwa sababu ya manyanyaso. Sasa hapo angeomba msamaha kivipi, wakati hakuwa na kosa lolote?? Unachotaka kutuambia wewe ni kuwa jamaa angenywea, ajipendekeze na kulialia kwa boss mnyanyasaji ili abaki kazini. Sasa huo ni utu? Na inaonekana jamaa alishavumilia kwa muda mrefu; lakini mwisho akaamua kuwa jasiri kulinda utu na heshima yake. Mambo ya "watoto kufa njaa" ni expression tu ya kuonesha kwamba sasa huna kazi, huna kipato, na kwa sababu hiyo mipango yake mingi aliyokuwa amepanga itavurugika. Kwa hiyo usiichukulie hiyo expression kwa neno kwa neno.
   
 15. u

  ureni JF-Expert Member

  #15
  Sep 28, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Mimi kwa upande wangu kama niko mahali na nina malengo fulani na nahitaji kitu fulani nitaomba msamaha hata pasipo kuambiwa nikishafanikiwa kupata nilichokuwa ninachokihitaji nitakavyotoka mwenyewe atabloo na msamaha wake aliopokea,kuna mzee mmoja ambaye ni tajiri sana kwa sasa hivi yeye alikuwa akija kwako wewe mtu mdogo atakunyenyekea hata kupiga magoti atapiga lakini akishapata alichokua anahitaji utalia,hiyo ni mbinu mojawapo ya kivita katika mapambano ya kutafuta maendeleo.Kwa hiyo wakubwa hilo neno msamaha mnaliogopa lakini linaweza kukufikisha pazuri sana.
   
 16. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #16
  Sep 28, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  Mkuu ukinisoma upya utaona maneno yafuatayo;
  Means to an end..., baniani mbaya kiatu chake dawa, A brave man dies once but a coward a thousand times.., kama kuna alternatives...

  Hapo utaona kwamba in general ninaonyesha kwamba sio busara ya kuendelea kunyanyaswa kwenye kazi kwa kuogopa kwamba utakosa kazi nyingine (huo utakuwa uoga, a coward).. lakini kama hakuna alternative ya kazi kuacha shughuli inayokupatia mkate wako na familia yako, sababu ya so called manyanyaso after all its a shortcut and easier way (ambayo wengi wetu tutafanya) ila kukaa kwenye manyanyaso na kuvumilia its even harder.., After all majority yetu kazi tunazofanya ni manyanyaso tofauti tofauti (from waalimu wanaolipwa peanuts kwa kazi yao ngumu, na wafanyakazi kwenye nyumba za watu wanaonyanyaswa ili wapate pesa kupelekea ndugu zao vijinini.., n.k.)

  Hivyo busara ni kutafuta pengine na kuondoka na sio kuondoka kabla ya kutafuta pengine... (Na kuacha mbachao wakati hakuna hata msala upitao its even worse...)
   
 17. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #17
  Sep 28, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Utaombaje msamaha kama hujakosa ? tena kazini? ukiwa unajiamini mambo yataenda vizuri tu,na pia utaheshimika kwa uamuzi wako.
  msamaha bila kukosa labda kwenye ndoa au mahusiano unaweza kuapply.
   
 18. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #18
  Sep 28, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  I wonder kwanini kwenye ndoa au mahusiano uweze ku-apply..., I guess ni just means to an end.., a small price to pay, giving in less to achieve more..

  Sasa kwenye kazi umesema huwezi kuomba msamaha kama hujakosa, inabidi kujiamini na mambo yatakwenda sawa... (sijui kwenye scenario ya mtu kama houseboy au kijakazi ambae for that moment hana alternative ya kupata kazi nyingine, mwenye bosi asiyependa kushindwa utamshauri afanye nini..., kumbuka hapo a price to pay inaweza kuwa ni kukosa pesa za kuwaendeleza wanaomtegemea.

  Kumbuka sometimes decision yako consequences zake does not affect only you.., but your family and loved ones.., Je is kuomba radhi bila kukosa still a high price to pay kuliko well-being ya familia yako (mkate wa kila siku na kumalizia school fees zao)
   
 19. u

  ureni JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Ha ha haaa mkuu unachekesha sana sasa kwa wale wanaotegemea hiyo kazi kuendeleza maisha yake leo kakataa kuomba msamaha akatimuliwa kazi familia yake ikaazirika watoto wakashindwa kula na kwenda shule,pamoja na yeye kwa kukosa kipato na kuwa kapuku unafikiri ataheshimika kwa uamuzi wake kama ulivyonena hapo juu?hiyo heshima itamsaidiaje katika maendeleo yake au nyie ndio wale mnaotafuta fedha mkatengeneze heshima baa?hakuna hiyo wakati mwingine tusifanye maamuzi kwa ajili ya sifa tukasahau impact yake.
   
 20. Masaningala

  Masaningala JF-Expert Member

  #20
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 539
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Tunatafsiri vipi msemo huu? "Mtimizie kafiri upate mradi wako"
   
Loading...