GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,689
- 109,104
Kwanza tuelewane chini ya CAF hakuna Shindano la Loosers ( Walioshindwa ) bali Mashindano yote yana Umuhimu na yametenganishwa ili Kukuza zaidi Kiwango cha Soka hasa Kimashindano kwa Bara la Afrika.
Pili kama kuna mwana Simba SC Mwenzangu hapa JamiiForums anabeza Mafanikio haya ya Yanga SC na Jumapili ikifuzu Kihistoria kwa hatua ya Nusu Fainali ya CAFCC hatoishia tu kuwa Mshamba bali atakuwa ni Juha ( Fool ), Mchawi Tukuka na siyo Mwanamichezo.
Tatu na Mwisho Simba SC haijawahi Kucheza Fainali ya CAFCC ila ilicheza Fainali ya Kombe la Washindi Barani Afrika kwa Kucheza na Stella Abidjan ya Ivory Coast.
Tena niwaibieni Siri wana Simba SC Wenzangu hili tusiliendeleze sana kwani hata hilo Kombe lenyewe la Washindi lilikuwa halishirikishi Timu nyingi kama ilivyo sasa katika Kombe la Shirikisho ambalo Yanga SC inashiriki.
Ni Uwendawazimu usio na Mipaka wala Uvumilivu leo hii Kuwabeza Yanga SC wanaoshiriki Michuano yenye Timu nyingi tena wakianzia hatua za Awali ya CAFCC na Kuilinganisha na Michuano ya iliyokuwa Kombe la Washindi ambayo Timu zilikuwa chache na Ushindani wake ukiwa ni Hafifu tofauti na sasa.
Tukubali tu kuwa kwa sasa Watani zetu Yanga SC Gari imewaka Kimataifa na Kitaifa na pia hata Bahati nayo imekaa upande Wao hivyo huu Mjumuiko / Mseto wa haya Mambo yote Mawili yanaifanya Yanga SC izidi Kutakata na Inatakata kweli kweli huku ikituumbua tunayoichukia na kuiombea mabaya Kutwa.
Kama kuna mazuri Kwao tuyaige tu.
Alamsiki nyote.
Mimi ndiyo GENTAMYCINE The King!!!!!