KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,590
- 4,601
Uchaguzi halijawahi kuwa jambo dogo Kwa wanaoshindwa duniani kote ,hata aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump aliwahi kulalamika kuchezewa faulo iliyopelekea kushindwa na Joe Biden Rais wa Sasa wa Taifa Hilo lenye demokrasia kubwa zaidi duniani.
Kutokana na mfano huo wa Trump na Marekani tunapata picha kubwa ya maumivu wanayopitia wanaoshindwa bila kujalisha aina ya kushindwa kwao. Kama Trump analalamika kuchezewa faulo katika Taifa linalofikiriwa kuwa na demokrasia kubwa dunia basi kuanzia Leo tukubaliane tu kushindwa halijawahi kuwa jambo dogo.
Wengine wanashindwa kukabiliana na hali ya kushindwa na kuamua kubeba silaha na kuingia porini, wengine wanapata mshtuko, wengine wanapata msongo mkali wa mawazo na wengine wanafikia hatua ya kujiua , haya yote ni matokeo hasi ya kushindwa.
Kwa kutambua hili ,kulingana na swali langu kwenye heading nililohoji, je uchaguzi uwe wa vipi ili usiwe na malalamiko?
Hili ni swali gumu kidogo maana majibu ya swali hili yatatolewa na walioshindwa na kutokukubali kushindwa na sio walioshindwa na kukubali kushindwa. Aliyeshindwa na kukubali kushindwa wahenga wanamtanbua kama ni mshindani wa kweli, na kwa sifa za watu wa namna hii kwao kushindwa ni changamoto na wana uwezo wa kulibadilisha changamoto hii kuwa fursa na baadaye kuwa washindani Wazuri.
Bahati mbaya watu wa namna hiyo hapo juu hawapo kwenye siasa zetu ila Kuna watu ambao hawakubaliani kushindwa, hawamjui Kuna kushindwa na kushindwa ni tatizo kubwa kwao. Watu hawa ndio msingi wa hoja yangu.
Kama nilivyosema ,matokeo ya kushindwa yanakuja na athari hasi za muda mrefu Kwa baadhi ya watu. Wasiokubali kushindwa wanahitaji ushauri nasaha kuwakinga na athari za kisaikolojia na msongo mkali wa mawazo na mawazo mengi hasi akilini mwao.
Ninashauri Serikali ianzishe kitengo maalumu Cha ushauri nasaha au huduma maalumu ya ushauri nasaha Kwa wote ambao wameathiriwa au wataathiriwa na matokeo ya kushindwa maana wanahitaji ushauri ili wasonge mbele na kuona kushindwa ni changamoto na jambo la kawaida maana katika hali ya kawaida mtu kulalamika miaka mitano naamini jambo hilo ni hatari Kwa afya ya akili.
Ahsante