Kuhusu Rais kutumia lugha ya Kiingereza

Kuhusu Rais kutumia lugha ya Kiingereza

Siku kadhaa kulikuwepo na ubishani mkali sana humu 'ukumbini' kuhusu ufaha wa lugha ya kiingereza kwa Mheshimiwa Rais.

Mimi nawamegea hii niliyokutana nayo leo LIVE kwenye mkutano wa wawekezaji wa VIETNAM na Tanzania (Business Forum) kwenye Ukumbe wa mikutano wa Mwalimu Nyerere (nilihudhuria!).

Ujumbe wa Vietnam uliongozwa na Rais wao Trương Tấn Sang.Kwa upande wa TZ kiongozi mkuu alikuwa ni PM na waziri wa viwanda Mhe.Mwijage.Shughuli za ufunguzi zikaanza kwa Kimombo,Mhe.Waziri wa viwanda=Kimombo,PM= Kimombo,MC=kimombo,Dr.wa IPP Ltd= Kimonbo.

Sasa ikafika zamu ya H.E Rais wa Vietnam!Akaanza kuhutubia kwa Ki-Vietnam,wasaidizi wake nao lugha yao,wauliza maswali nao kivietnam isipokuwa MD wa Halotel Tz ambaye alisoma hotuba yake kwa kiingereza na haikueleweka vizuri kwa sababu hajakulia kwenye kizungu.

HADITHI HII INATUFUNDISHA NINI?

Huli ndio tatizo kubwa miongoni mwetu sisi wananchi wa Afrika, kwa ujumla, na wengi wetu nchini mwetu Tanzania, kuwa kama hujasema Kiingereza basi wewe hujasoma, au mjinga, au si mstaarafu. NI KASUMBA TULIOLISHWA NA WAKOLONI WETU, tokea miaka ya kudai Uhuru, hadi baada ya kupata Uhuru wetu. Kwamba Kiswahili ni lugha ya barabarani tu, haiwezi kujitosheleza, na ni lugha ya wajinga. Hivyo, hata kuelimishwa, jographia, hisabati, historia, ufundi wa kutengeneza magari, na mambo mengine, LAZIMA uelimishwa kwa lugha ya Kiingereza. Ni upumbavu wa mwisho kabisa. Wajapani, Wajerumani, Wachina, Wafaransa, Waarabu, Wavietnamu, na wengi wengine walioelimishwa na kuendelea kuelimishwa katika llugha zao weneywe, siyo tu wameelimika na kuelewa walichoelimishwa, bali wanatumia lugha yao kuelimisha wenginne wakijuwacho, na wanaunda vifaa mbali mbali, vya matumizi yao na vya matumizi ya wengine, na hata wanaogopwa, katika maeneo mengine ya maendeleo yao na hao wanasema Kiingereza kama lugha yao ya kuzaliwa au kusomeshewa. Asiyethamini CHAKE hawezi kuthaminiwa na Wengine! Tuache kasumba ya Kiingereza. Tujifunze Kiingereza vizuri, na lugha zote nyengine zilizomuhimu, tujifunze. Ila tusiwe na Kasumba kwamba UJUZI na UELEWA ni kujieleza kwa Kiingereza tu. Jieleze kwa lugha yako, kwanza, na jifunze lugha ya mwenzio ili umeelewe unapohitajia kumuelewa.
 
Back
Top Bottom