Kuhusu Rais kutumia lugha ya Kiingereza

Kuhusu Rais kutumia lugha ya Kiingereza

Tanzania lugha zote mbili kiingereza na kiswahili zinatumika kufundishia. wanafunzi upimwa pia na kupewa alama za ushindi au kushindwa.....hatutegemei ktk mazingira hayo mtu awe na PhD asiongee na kufanya mawasilisho yake ktk lugha fasaha za kiingereza na kisw.

hata ivyo nikubaliane na wengi kuwa lugha yetu ni kiswa....tuipende na tuitumie....

Rais ana nafasi ya kuboresha kiingereza chake...Kabila amefanya hivyo ktk lugha ya kifaransa....kujifunza hakuna mwisho....
Wasomi wa sayansi wengi huwa Kingereza cha kuongea ni shida kutokana na masomo Yao kujaa Kingereza ambacho hakipo kwenye lugha za kawaida kwenye jamii , si lazima Rais aongee Kingereza fasaha kiswahili kitakuwa hakikui lakini Rais akionyesha kukithamini Kwa nguvu kitakua Kwa kasi barani Afrika .
 
E
Mtanzania sijui utamweleweshaje mpaka akubali kuwa kujua kiingereza sio kuonyesha mtu ni bora na ana akili. Sijui ni madhara ya kutawaliwa au nini lakini mimi nafikiri ni kwa sababu ya elimu duni tuliyoipata kwenye shule zetu hivyo inatufanya tusijiamini. Magufuli kiingereza chake ni kizuri na kinaeleweka. Kuna marais na viongozi wa nchi nyimgine ukisikia kiingereza chao ni majanga lakini huwezi kukuta wananchi wao wanapoteza muda kuwajadili kama sisi.
Mahaba yanawafanya mnakuwa blind kabisa! Hakuna anayesema kujua kiingerezs ni kuwa na akili. Tunasema kwa mazingira ys Tanz ambapo kiingereza ni official language ya serikali inashangaza kwamba mkuu wa nchi hawezi kuizungumza hiyo luha kifasaha!Tunashauri azungumze tu kiswahili!
 
ndio,wanaongea aidha kifaransa,kiitaliano,kiarabu,kijerumani,kihispania au kireno!nchi nyingi ulizozitaja hapo juu hasa za Latina America zinaongea aidha kihispania,au kireno lugha za wakoloni walio watawala!mnapiga kelele humu kwa kuwa magufuli kiingereza hajui,angekuwa anajua povu lote hili lisinge watoka
mimi ni mpinzani namba moja wa Magufuli lakini hapo kwenye Kingereza nitamtetea kwani tusipokithamini kiswahili kitapotea kabsa kuabudu Kingereza ni kuabudu utumwa mbona Urusi Rais wao anajua Kingereza lakini akisafiri kwenda Nchi zingine huongea kirusi . Ulimbukeni wa kuendekeza Kingereza utakwisha lini?
 
Hata Rais wa Vietnam Kiingereza kimempita kushoto. Nchi yao ina uchumi wa kati na Rais hajui Kiingereza TAFAKARI CHUKUA HATUA!!! Kwa hisani ya watu wa Marekani.

Queen Esther

lugha mama ya kwetu imeathiri,tuna tatizo kubwa la "L"/"R",ila tunarudi kule kule,magufuli kiingeleza kimempitia kushoto
 
Kama tunauzalendo na Kiswahili basi tukizungumze, siyo tuchomekee chomekee ung'eng'e
 
mimi ni mpinzani namba moja wa Magufuli lakini hapo kwenye Kingereza nitamtetea kwani tusipokithamini kiswahili kitapotea kabsa kuabudu Kingereza ni kuabudu utumwa mbona Urusi Rais wao anajua Kingereza lakini akisafiri kwenda Nchi zingine huongea kirusi . Ulimbukeni wa kuendekeza Kingereza utakwisha lini?
basi tubadilishe ya 1977,inayosema lugha rasmi ni kiswahili na kiingeleza,tutoe kiingeleza tubakie na kiswahili!ila kama katiba itabaki hivyo,basi ni aibu kwa mkulu wetu wa nchi kushindwa kuimudu lugha yake ya taifa
 
E

Mahaba yanawafanya mnakuwa blind kabisa! Hakuna anayesema kujua kiingerezs ni kuwa na akili. Tunasema kwa mazingira ys Tanz ambapo kiingereza ni official language ya serikali inashangaza kwamba mkuu wa nchi hawezi kuizungumza hiyo luha kifasaha!Tunashauri azungumze tu kiswahili!
Majipu yanatumbuliwa Kwa kiswahili , Amri na utendaji mwingi ni Kwa Kiswahili ni si kweli kwamba Magufuli hajui Kingereza bali tunamwomba akipende Kiswahili aje na style yake asikariri Akili za malimbukeni .
 
Tunapaswa kujifunza kupenda,kuthamini na kutumia vyetu,sio lugha tuu! Uzalendo unaanza kwa kufurahia chako na kukiboresha zaid.
Habari ya kujadili kiingreza ni tabia ya kish..nz
 
hajui kiiengereza,ndio maana ili kuficha aibu zenu,mpo umu kuimba mapambio kwa magufuli kuongea kiswahili
Kwel hajui kiingereza kutokana na uelewa wako mfinyu!!! Kwan kutokujua kiingereza ndio aibu Marais wangap hawajui kiingereza, je Akina Ronaldo, Messi nk wanajua kiingereza, acha ushamba ww
 
basi tubadilishe ya 1977,inayosema lugha rasmi ni kiswahili na kiingeleza,tutoe kiingeleza tubakie na kiswahili!ila kama katiba itabaki hivyo,basi ni aibu kwa mkulu wetu wa nchi kushindwa kuimudu lugha yake ya taifa
Bora iwe hivyo lakini huwa anaeleweka pindi akiongea .
 
E

Mahaba yanawafanya mnakuwa blind kabisa! Hakuna anayesema kujua kiingerezs ni kuwa na akili. Tunasema kwa mazingira ys Tanz ambapo kiingereza ni official language ya serikali inashangaza kwamba mkuu wa nchi hawezi kuizungumza hiyo luha kifasaha!Tunashauri azungumze tu kiswahili!
Nadhani asilimia 90 ya watanzania wameathirika na siasa za chama tawala vs upinzani kiasi ambacho wanadhani kuna watanzania wa aina mbili tu. ie wa chama tawala na upinzani. Na ndio sababu iliyokufanya uone mimi nina mahaba na Magufuli. Mimi nazungumzia ukweli kuhusu lugha. Kiingereza cha Magufuli kinatosha kabisa kuzungumza popote pale duaniani na akaeleweka. Ungekuwa umewahi kuishi nchi ambazo kiingereza sio lugha yao ungeelewa nachomaanisha. Lakini nina uhakika hujawahi hivyo huwezi kunielewa!
 
Nimesoma training fulani na wavietnam, wanaongea kiingereza fasaha kabisa kuliko Watanzania wengi. Hata walipokuwa wakiongea wao wenyewe, bado walitumia kiingereza. Tutazunguka sana, lakini kiingereza ni muhimu sana kutumika hasa kwa biashara za kimataifa. Watu humu wanataka kuhalalisha kwa nguvu zote umbumbumbu wetu wa kutojua kiingereza. Eti mfanyabiashara amefunga safari ya zaidi ya masaa 12 kwenye ndege, halafu unakuja kumzungumzia kiswahili?
 
Hata Rais wa Vietnam Kiingereza kimempita kushoto. Nchi yao ina uchumi wa kati na Rais hajui Kiingereza TAFAKARI CHUKUA HATUA!!! Kwa hisani ya watu wa Marekani.

Queen Esther
tofauti ya huyo mviet na magufuli ni kuwa,mvietnam katiba yao inatambua kievtanam kama lugha rasmi ya taifa,uku magufuli katiba ya 1977,inatambua lugha 2,english and kiswahili!sasa hapo unaongea nini?hajui kiingeleza,fullstop!
 
Weka hicho kipengele cha katiba humu acha uongo!!!

Queen Esther

tofauti ya huyo mviet na magufuli ni kuwa,mvietnam katiba yao inatambua kievtanam kama lugha rasmi ya taifa,uku magufuli katiba ya 1977,inatambua lugha 2,english and kiswahili!sasa hapo unaongea nini?hajui kiingeleza,fullstop!
 
Tunapaswa kujifunza kupende,tuthamini na tutumie vyetu,sio lugha tuu! Uzalendo unaanza kwa kufurahia chako na kukiboresha zaid.
Habari ya kujadili kiingreza ni tabia ya kish..nz
Uganda wanajua Kingereza vizuri, malawi, Zambia , zimbabwe lakini hawana maendeleo kuizidi Tanzania , Ulimbukeni wa Kingereza Sasa unafaa ukemewe live.
 
Majipu yanatumbuliwa Kwa kiswahili , Amri na utendaji mwingi ni Kwa Kiswahili ni si kweli kwamba Magufuli hajui Kingereza bali tunamwomba akipende Kiswahili aje na style yake asikariri Akili za malimbukeni .
ila mikataba minono minono yenye ten percent kubwa kubwa,mnapo iandika na hao ngozi nyeupe mnaiandika kwa kiingeleza!nyie zungukeni tu,inshort,magufuli aende english course,kama lugha za kibantu anaweza karibu kumi,atashindwa kimombo?
 
Back
Top Bottom