Kuhusu Rais kutumia lugha ya Kiingereza

Kasongo

JF-Expert Member
Jul 29, 2007
3,150
2,273
Siku kadhaa kulikuwepo na ubishani mkali sana humu 'ukumbini' kuhusu ufaha wa lugha ya kiingereza kwa Mheshimiwa Rais.

Mimi nawamegea hii niliyokutana nayo leo LIVE kwenye mkutano wa wawekezaji wa VIETNAM na Tanzania (Business Forum) kwenye Ukumbe wa mikutano wa Mwalimu Nyerere (nilihudhuria!).

Ujumbe wa Vietnam uliongozwa na Rais wao Trương Tấn Sang.Kwa upande wa TZ kiongozi mkuu alikuwa ni PM na waziri wa viwanda Mhe.Mwijage.Shughuli za ufunguzi zikaanza kwa Kimombo,Mhe.Waziri wa viwanda=Kimombo,PM= Kimombo,MC=kimombo,Dr.wa IPP Ltd= Kimonbo.

Sasa ikafika zamu ya H.E Rais wa Vietnam!Akaanza kuhutubia kwa Ki-Vietnam,wasaidizi wake nao lugha yao,wauliza maswali nao kivietnam isipokuwa MD wa Halotel Tz ambaye alisoma hotuba yake kwa kiingereza na haikueleweka vizuri kwa sababu hajakulia kwenye kizungu.

HADITHI HII INATUFUNDISHA NINI?
 
Chamsingi kama ujumbe ulieleweka kwa tafsiri ya wasaidizi wake sio tatizo. Far East, English ni tatizo kubwa, sehemu pekee unaweza kuongea lugha hiyo na wenyeji wengi ni Hong Kong na Singapore (Kwa uzoefu wangu), mataifa mengi ya kule yanaamini katika lugha yao.
 
English is the most popular language in Vietnam afterVietnamese, and in the cities, even when you try to communicate in Vietnamese, the local younger people will just respond to you in English.
 
Siku kadhaa kulikuwepo na ubishani mkali sana humu 'ukumbini' kuhusu ufaha wa lugha ya kiingereza kwa Mheshimiwa Rais.Mimi nawamegea hii niliyokutana nayo leo LIVE kwenye mkutano wa wawekezaji wa VIETNAM na Tanzania (Business Forum) kwenye Ukumbe wa mikutano wa Mwalimu Nyerere (nilihudhuria!).Ujumbe wa Vietnam uliongozwa na Rais wao Trương Tấn Sang.Kwa upande wa TZ kiongozi mkuu alikuwa ni PM na waziri wa viwanda Mhe.Mwijage.Shughuli za ufunguzi zikaanza kwa Kimombo,Mhe.Waziri wa viwanda=Kimombo,PM= Kimombo,MC=kimombo,Dr.wa IPP Ltd= Kimonbo.Sasa ikafika zamu ya H.E Rais wa Vietnam!Akaanza kuhutubia kwa Ki-Vietnam,wasaidizi wake nao lugha yao,wauliza maswali nao kivietnam isipokuwa MD wa Halotel Tz ambaye alisoma hotuba yake kwa kiingereza na haikueleweka vizuri kwa sababu hajakulia kwenye kizungu.HADITHI HII INATUFUNDISHA NINI?
Tutumie lugha yetu kama ya kigeni imekupitia kushoto na tuache kujiaibisha bure.
 
Ukiona mtu anatumia lugha yake ya kuzaliwa kujadili mambo na watu wasio tambua hiyo lugha jua kua hiyo ndo lugha aliyofundishiwa kupata elimu yake.Sasa hapa kwetu lugha ya kufundishia nakupa hizo mnazo ziita phd ni kiingereza.Ukijadili na wasiokijua kiswahili lazima uongee kiingereza
 
Inashangaza sana kuona Tanzania ambayo ndio chimbuko la Kiswahili na zaidi sana kuwa lugha ya saba ulimwenguni,Lugha ya pili Afrika kuzungumzwa baada ya kiarabu bado tunajadili lugha ambayo wanapaswa kutumia viongozi wetu.Ingependeza sana kama katika awamu hii ya tano ya JPM kitumike kiswahili bila kuhangaika na kiingereza kwenye hafla kama mtoa mada alivyojaribu kutuonyesha.Hii ni fursa kwa waliobobea kwenye kiswahili ili waanze ukalimani katika mikutano na hafla kama hizo.Hizi kasumba za kulazimisha kiingereza kutumika eti kwa kuwa kiingereza ndio lugha ya ulimwengu imepitwa na wakati.
 
Hapa Tz tunajichanganya tuu, Na unataka kujua kuwa Watu wanajichanganya ni kuangalia ni kiasi gani topic hizi Za kujua kiingireza au kutojua zitakavo kuwa hazitomaliza humu jf. Sababu kubwa ni wale wanaojiona wanakijua hiki kieng Na wale wasiokijua. Tu ache mambo haya hayana msingi wala Tija Kwa muda huu. Kama mtu Kakosa kukijua usilaumu sana ni utaifa umetufanya hivi. Tupongezane, tutiane moyo kilakitu kitakaa sawa. Na ninaamini viongozi wetu watagundua wapi tumeteleza, kwakua hatujachelewa tuwape muda.
 
Hapo wa kuulizwa ni waandaji wa mkutano
waliaandaa wakalimani wa lugha zipi?
 
Mtatafuta kila kigezo kuhalalisha ungumbaru wetu wa kiingereza, lakini suala la kujifunza kiingereza fasaha halina mjadala. Na hasa kwa rais wetu.
 
English is the most popular language in Vietnam afterVietnamese, and in the cities, even when you try to communicate in Vietnamese, the local younger people will just respond to you in English.

Hata Mmarekani au Muingereza hawezi kukiteteta kiingereza ambacho ni lugha yao kama wewe unavyofanya, unatumia nguvu nyingi mpaka unapoteza hata hoja ya hasa kile kinachojadiliwa wakati usichokijua ni kwamba hata wewe pia Mmarekani anakuona bado haujui kiingereza na siajabu hakutofautishi na Mvietnam au Mkongo na ukitaka kwenda Marekani pamoja na kujifanya kwako Muingereza bado Mmarekani atakwambia ufanye TOEFL au test of english as a foreign language, na hiyo wewe unayejifanya unajua sana Kiingereza au Mimi nisiyejua wote ni lazima tufanye, kwa Mzungu hakuna tofauti ya wewe na mimi hivyo kiingereza chako kitaishia hapa hapa JF tu!
 
comment yako hii,ina uhusiano wwt na mada na uyo mdau unayemjibu?
 
RAIS WA VIETNAM ANATUMIA LUGHA YAO NA SIO ENGLISH!!! SASA KWANINI NA SISI TUSIJIVUNIE LUGHA YETU???

Queen Esther

English is the most popular language in Vietnam afterVietnamese, and in the cities, even when you try to communicate in Vietnamese, the local younger people will just respond to you in English.
 
Hadithi hii inatufundisha kuwa tusiwe watumwa kama kiinchi kidogo ambacho kilikuwa masikini na sasa ni tajiri tena bila hata ya kuweka mbele lugha ya mkoloni ya kikoloni.
 
Back
Top Bottom