Rais Magufuli, tutawezaje kuikuza lugha ya Kiswahili wakati wewe mwenyewe ndiyo unapenda kutumia KiswaEnglish?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,480
30,152
Rais Magufuli amekuwa mstari wa mbele katika kuitangaza na kuikuza lugha ya kiswahili iwe lugha ya kimataifa. Lakini wakati huo huo yeye mwenyewe ndiyo amekuwa mstari wa mbele katika kuikuza lugha ya kiingereza kwa kutumia kile kinachoitwa kiswaenglish!

Ni vigumu sana unapomsikiliza Rais Magufuli akihutubia kumsikia akiongea sentensi moja bila kuchanganya lugha ya kiswahili na kiingereza

Je kwa kuchanganya lugha mbili za kiswahili na kiingereza, katika hotuba zake ndiyo tutakuwa tunakikuza kiswahili??

Je kwa kutenda hivyo si tunakuwa tunakienzi na kudumisha lugha ya mabeberu ya kiingereza??

Hilo ni swali tu wadau, ningependa nijibiwe
 
Ni kwamba hajui kuongea kingereza, sasa Mr. One Man Show anajaribu kuchomeka na maneno ya kingereza yale ya kufundisha Secondary ili ajionyeshe kuwa anajua kimombo, inshort hajui kuzungumza hiyo lugha. Hata mimi kuizungumza vizuri sijui kama nnavyozungumza kisambaa, kiswahili na kipare, ila namzidi japo sina PHD kama yeye.
 
Sasa kama yeye mwenyewe anajijua kuwa siyo mzuri sana katika kuiongea lugha hiyo ya kiingereza, kwa hiyo ni vyema akawa anaongea lugha ya kiswahili kiufasaha?
 
Chadema kwasasa Hanna hoja za msingi,kwahy inabidi tu muongeee chochote ili mradi muonekane wapinzani ....hili jina wapinzani likataeni ndo limebeba ujinga wenu.
 
Najiulizaga swali hili kila mara, yaan hawez kuongea maneno kumi bila kuweka neno la kingereza, ni kiswahil gan anachokipigia chapuo??
Hebu tujiulize, hivi umewahi kumsikia Jing Ping, yule kiongozi wa China, akihutubia achanganye kichina na kiingereza??

Umewahi pia kumsikia yule mama Angela Markel, naye anapohutubia, achanganye kijerumani na kiingereza??

Hao ndiyo wanaozienzi na kuzikuza lugha zao za kichina na kijerumani, siyo huyu wetu ambaye anawaponda mabeberu, huku akizihisudu lugha zao, ingawa kiingereza kinampiga chenga kukiongea!
 
Rais Magufuli amekuwa mstari wa mbele katika kuikuza lugha ya kiswahili na kuwa lugha ya kimataifa, lakini wakati huo huo yeye mwenyewe ndiyo amekuwa mstari wa mbele katika kuikuza llugha ya kiingereza kwa kutumia kile kinachoitwa kiswaenglish

Ni vigumu sana unapomsikiliza Rais Magufuli akihutubia kumsikia akiongea sentensi moja bila kuchanganya lugha ya kiswahili na kiingereza

Je kwa kuchanganya lugha mbili za kiswahili na kiingereza, katika hotuba zake ndiyo tutakuwa tunakikuza kiswahili??

Je si ndiyo tunakuwa tunakienzi na kudumisha lugha ya mabeberu ya kiingereza??

Hilo ni swali tu wadau, ningependa nijibiwe

Kwani Yeye hata kama anaongea hicho ' Kiswanglishi ' ndiyo amekuzuia Wewe usizungumze Kiswahili chako Fasaha? Kwani Viongozi wetu wa Dini ( wa Kiroho ) pale wanapokuwa wanatuambia tuache Dhambi ina maanisha kuwa Wao kama Binadamu hawafanyi Dhambi? Hoja yako ina ' Udhaifu ' kidogo japo pia ina ' Ukweli ' fulani kwa mbali hivi.
 
Lakini umeelewa kweli hoja yangu??

Nilichosema Mimi ni kuwa Rais wetu pamoja na kutuomba watanzania tukienzi na kukitangaza kimataifa lugha yetu ya kiswahili, lakini yeye mwenyewe amekuwa mstari was mbele kukitangaza kiingereza kwa kutumia kile kitu tunachokiita kiswaenglish
 
Lakini umeoelewa kweli hoja yangu??

Nilichosema Mimi ni kuwa Rais wetu pamoja na kutuomba watanzania tukienzi na kukitangaza kimataifa lugha yetu ya kiswahili, lakini yeye mwenyewe amekuwa mstari was mbele kukitangaza kiingereza kwa kutumia kile kitu tunachokiita kiswaenglish

Nadhani Wewe ndiyo hujanielewa na ndiyo maana bado unaendelea Kuhangaika na hiyo ' post ' yangu ya awali Kwako. Pole sana.
 
Umemwambia ukweli mtupu huyo jamaa

Mimi sina chama nilichojiunga nacho, ila naongelea masuala mbalimbali yanayohusu nchi yangu

Kwa tafsiri yake huyo jamaa, watanzania wote tunapaswa tujiunge na kile kikundi cha "kusifu na kuabudu" kwa ajili ya Mtukufu Mheshimiwa Rais na kwa yeyote atakayemsema vibaya Mtukufu, hata kama ni kwa nia njema ya kujenga, basi ataitwa yuko Chadema!
 
Ona hii

Wote ni Nyani ila Nyani wa Ramadi Simiyu si sawa na Nyani wa Mississipi au Amazon ki-hulka na Kitabia.....Na ikitokea kwa bahati ya kipekee, Nyani wa Ramadi akapewa uenyekiti msituni Amazoni, tegemea mara nyingi kutenda kwa kudhani Yupo Ramadi.
 
Umemwambia ukweli mtupu huyo jamaa
Mimi sina chama nilichojiunga nacho, ila naongelea masuala mbalimbali yanayohusu nchi yangu
Kwa tafsiri yake huyo jamaa, watanzania wote tunapaswa tujiunge na kile kikundi cha "kusifu na kuabudu" kwa ajili ya Mtukufu Mheshimiwa Rais na kwa yeyote atakayemsema vibaya Mtukufu, hata kama ni kwa nia njema ya kujenga, basi ataitwa yuko Chadema!
Hao ndiyo wakilala huota namna bora ya kuharibu mashamba ya Mbowe.👏👏😄😄😄😄
 
Rais Magufuli amekuwa mstari wa mbele katika kuitangaza na kuikuza lugha ya kiswahili iwe lugha ya kimataifa. Lakini wakati huo huo yeye mwenyewe ndiyo amekuwa mstari wa mbele katika kuikuza lugha ya kiingereza kwa kutumia kile kinachoitwa kiswaenglish!

Ni vigumu sana unapomsikiliza Rais Magufuli akihutubia kumsikia akiongea sentensi moja bila kuchanganya lugha ya kiswahili na kiingereza

Je kwa kuchanganya lugha mbili za kiswahili na kiingereza, katika hotuba zake ndiyo tutakuwa tunakikuza kiswahili??

Je kwa kutenda hivyo si tunakuwa tunakienzi na kudumisha lugha ya mabeberu ya kiingereza??

Hilo ni swali tu wadau, ningependa nijibiwe
Magufuli anataka ajulikane kuwa kasema. Yaani ni ushamba wa kujitakia. Lugha yenyewe haijui lkn anavyojidai kwa kuchomekea. Tuseme tumepata rais mshamba mwenye roho mbaya na chuki isiyoisha
 
Nakubaliana nawe kwa asilimia mia!. Nashauri kwenye huu mkutano ujao wa SADC ajitahidi sana kuongea kiswahili mwanzo mwisho, hata ikiwezekana aandikiwe hotuba yake kwa kiswahili ili asiwe na mwanya wa kuweka maneno ya kiingereza.
 
Back
Top Bottom