DOKEZO Kuhusu Mgombea wa nafasi ya Uweka Hazina Taifa Chama cha Walimu Tanzania Protas Magesa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

HaMachiach

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
3,399
6,077
Ndugu walimu na wanajamii kwa ujumla wa Taifa hili Tukufu, nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Naomba nianze kuweka bayana taarifa ambazo huenda hamzifahamu kuhusu Mgombea wa nafasi tajwa hapo juu Mwalimu Protas Magesa.

Huyu ni mwalimu mwakilishi kwenye Kamati ya Utendaji ya Taifa CWT Mkoa wa Mara aliyechaguliwa kujaza nafasi ya Munubi Sabato aliyeenguliwa kutoka kwenye nafasi hiyo kutokana na kugunduliwa na cheti feki, ambapo mwenye cheti chake ni Afisa mifugo Mwanza. Na Sabato alikua ni muhitimu wa Darasa la 7, kwa sababu ya ubobezi wake kwenye ushirikina aliyekua Katibu Mkuu wa CWT Deus Seif alimuajiri bila usaili Sabato na Kumpeleka Mpanda kama Katibu wa CWT.

TAKUKURU walipolibaini hili haraka Deus alimuondoa kwenye nafasi hiyo na kwa sasa ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Deus Seif na Protas Magesa. Mke wa Sabato alipewa pia ajira bila usaili kuwa Katibu wa Wilaya ya Bunda.

Magesa pamoja na kuwa mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Taifa (KUT) Mara, KUT ilimteua kuwa Kaimu Mwekahazina wa Taifa kwa mujibu wa Katiba ya CWT baada ya kufungwa gerezani kwa aliyekuwa mwekahazina wa Taifa Abubakari Alawi kwa kosa la wizi wa Fedha za Walimu na Matumizi mabaya ya Madaraka.

Pamoja na vyeo tajwa hapo juu, Protas Magesa sio mwalimu wa darasani, ni mwajiriwa wa Tume ya Utumishi ya Walimu (Teachers Service Commission), mwajiri wake ni Katibu Mkuu Utumishi, yeyote atakayemuhitaji Magesa ni lazima kwanza awasiliane na Katibu Mkuu wa Tume ya Utumishi ya Walimu Bi. Paulina Nkwama ambaye yupo Ofisi ya Rais Utumishi.

Magesa hawajibiki kwa DED wala kwa RAS. Mwenye mamlaka naye ni Katibu Mkuu wa Tume kwa hiyo yuko mbali sana na Walimu. Hawezi kuwatumikia kwa haraka wala kikamilifu. Isitoshe, yeye ndie anayewahukumu walimu wanapokosea kwa nafasi yake na wala adha za walimu hazijui.

Pia kwa wasiofahamu Bw. Protas Magesa anayo mamlaka kisheria kujiunga na chama chochote cha wafanyakazi anachokitaka kati ya TUGHE, CWT na TALGU kwa nafasi aliyonayo na wala hazuiliwi ilimradi amuandikie Bi. Paulina Nkwama barua na kumuelekeza akate ada ya uwanachama na kwa chama alichomuelekeza yeye kuwepo.

"Naomba nikuulize swali wewe mwalimu je, wewe una mamlaka ya kuchagua kujiunga na chama chochote unachotaka zaidi ya CWT?

Pia ni hivi karibuni tu baada ya Rais wa CWT Bi. Leah Ulaya na Katibu Mkuu wa sasa Bw. Japhet Maganga kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nafasi za Ukuu wa Wilaya ndipo vituko vya Magesa vilipoanza.

Hata kabla ya viongozi hawa kupata barua za uteuzi, Magesa kwa kushirikiana na aliyekuwa Afisa Habari wa Chama Marehemu Batholomeo Chilwa waliitisha vyombo vya habari na kutangaza Kwamba chama hakina uongozi isipokua yeye peke yake na hivyo kusababisha taharuki Kubwa kwenye taasisi na jamii kwa ujumla huku akijua wazi kuwa hana mamlaka hiyo kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama cha Walimu.

Aliita vyombo vya habari waziwazi na akazungumza wakati anajua mwenye mamlaka ya kuisemea taasisi kitaifa ni Rais wa chama na wala sio vinginevyo. Mbaya zaidi wakati anaongea na waandishi wa habari Rais wa chama alikuwa kazini kwake Tabora na Katibu Mkuu alikua ofisini anaendelea na majukumu yake kwenye jengo hilo hilo.

Vyanzo vya taarifa vinabainisha kuwa viongozi wa juu wa chama hawakuwa na taarifa za Press Conference hiyo na wao walizisikia kupitia vyombo hivyo. Kwa Ufupi Magesa alifanya uhaini kwa dhamira ya kufanya Mapinduzi. Swali la kujiuliza alitumwa na nani? Jibu ni kwamba Magesa anafanya kazi kuhakikisha kwamba waliokiibia chama fedha na mali Deus Seif na Abubakari Alawi wanafanikisha mambo mawili.

(1) kushinda rufaa yao ya tarehe 10 Machi 2023 kwa kufutiwa kesi.

(2) Kushinda kesi yao dhidi ya maamuzi ya Mkutano Mkuu ya kuwafuta uwanachama na kisha warejee madarakani.

Kwa nini wanataka kurejea madarakani? Hapa kuna sababu mbili tu;

(1) Ili waendelee kufisidi fedha na mali za chama, kosa lililowasababishia kifungo gerezani.

(2) Kukidhi matakwa ya baadhi ya wanasiasa waandamizi na viongozi wa serikali ambao wamekuwa wakifaidika na fedha za wanachama wakati wa Uongozi wao.

Hii ndio maana viongozi hao walitoa shinikizo kubwa na hata vitisho kwa Rais na Katibu Mkuu wa chama waende kuapishwa kama Wakuu wa Wilaya ili kwenye nafasi za juu za uongozi wa chama waweke watu wao. Mmoja wa watu hao kwa sasa ni Protas Magesa.

Yapata mwezi mzima sasa, Magesa hayuko kazini kwake anapita kila mkoa kukutana na uongozi wa ngazi za wilaya na mikoa na kuwapatia wajumbe Rushwa ili tarehe 17 Machi 2023 achaguliwe kuwa mwekahazina wa Taifa wa CWT na wajumbe wa mkutano mkuu wa CWT akidhi yaliyobainishwa hapo juu.

Lakini pia ni vizuri kujiuliza, gharama za safari yake na fedha anazohonga anazipata wapi? Ni lazima awe amezikopa au amepewa na wanasiasa na anategemea kuzilipa kutoka kwenye fedha za ada za wanachama wa CWT. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema "Ukiona watu wanatumia fedha kuingia madarakani jiulize wanakwenda kufanya biashara gani. Na kama hiyo hela wameikopa kuhonga watu, je, watailipaje hiyo hela? Maana ukweli ni kuwa hakuna biashara kwenye taasisi?"

Sasa hivi hata financial transactions ndani ya ofisi amezisimamisha kwa sababu hakai ofisini. Ni lundo la mafaili ya malipo liko idara ya uhasibu wale wenye madai yao mtakua mnaujua ukweli huu.

Nia yake pia ni kuonesha kwamba ofisi ya Makao Makuu ina shida, kumbe shida zenyewe anasababisha yeye kwa kufanya hujuma. Na hii ndio maana kwenye kikao cha Baraza la Taifa Tanga tarehe 16 na 17 Februari 2023 Magesa alinusurika kupigwa na baadhi ya wajumbe kwa kitendo cha kukataa kusaini mishahara ya wafanyakazi wa chama iliyokuwa imecheleweshwa sana.

Awashukuru Rais na Katibu Mkuu wa chama waliozuia mpango huo. Pia ikumbukwe kwamba Magesa ndiye aliyekua akiwarekodi Rais na Katibu Mkuu wa chama kwenye kikao cha kamati ya utendaji mwezi Februari jijini Tanga na kurusha katika mitandao ya kijamii.

Huyu siyo muadilifu maana yanayojadiliwa vikaoni kwa maslahi ya walimu yanabaki ni ya wajumbe wa vikao hivyo na sio kurusha kwenye mitandao ya kijamii hiyo ni kazi yetu sisi wenye jukumu la kusemea maslahi ya wanyonge.

Mwisho kabisa tungependa kutoa rai kwamba Magesa hatakipeleka chama mbele bali kukirudisha nyuma. Deus Seif na Abubakari Alawi ni vizuri waachane na Mambo ya Chama wasubiri hukumu yao Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam tar 10/7/2023, sanjari na aliyekuwa mwekahazina wa zamani mkuu wa wilaya ya Mvomero Mohammed Utali.

Kwanza ajiulize kwa nini kwenye mkeka wa Mama wa hivi karibuni hayupo na haitatokea akumbukwe kwani mabaya aliyoyafanya Mvomero kumbukumbu yake ipo.

Mwingine ni kwa mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Protas Magesa, Munubi Sabato, aridhike na mshahara wa mkewe aliyeajiriwa kama Katibu na Deus bila usaili.

Mwisho kabisa, tunapenda kuwaasa viongozi wa kiserikali na wanasiasa wanaogharamia kampeni za watu waovu ndani ya chama tunaamini wanajua tunawajua, ni kwa kuheshimu Mamlaka iliyowateua ndio maana hatuwataji bayana hapa ila mapambano dhidi ya wahuni na wabadhilifu kwenye vyama vya wafanyakazi ni ya kudumu huu ni mwanzo tu.
 
Dah walimu halafu mkidharauliwa hadi na bodaboda mnalalamika?kwa hali hii mtadharaulika Sana 😅 wote mnagombea ulaji wa hela za walimu wenzenu 😅
 
Wote nyie wezi tu mpo hapa kutaka kutafuna fedha za wana mpwayungu village kwani ukijiunga na chakuhawata utapungukiwa nini?
Chakuwahata ni chama cha walimu wa Kigoma, kama hauko Kigoma itabidi ujue unajiunga na kipi. Makao makuu yako wapi tuje tujiunge? Msiwahadae walimu kwa shilingi 5,000 chama hakiwezi kufanya kazi kwa hela hiyo. mtakua wapigaji zaidi ya CWT.
 
Back
Top Bottom