Kaka tatizo si Chama wala siasa kwenye uzi huu, suala ni tuhuma dhidi ya Manji, walienda wawili tuu mkafunga barabara central, je wangeitwa watafuna nchi kumi siku moja si Dar nzima ingesimama? Tuwe na subira jamani.
Aliyeleta uzi, alisema "Wapinzani", naomba usiwe mwepesi kusahau na mgumu kuelewa.
Hao waliofungiwa barabara na wananchi, walifungiwa kwa sababu ni waharifu ila tu hatutaki washughulikiwe?
Sifunze kuelewa mada. Tatizo ni kukiukwa kwa taratibu. Mchakato mzima alivyoupeleka huyu jamaa, sasa umewafanya waharifu wengi kuharibu ushahidi. Siyo kila kitu ni kusema "Ndiyooooo" au Hapanaaaa. Yapo masuala ya kitaalamu, yanahitaji taaluma. Lakini pia taaluma ina maadili yake makubwa ambayo ni kweli na haki. Kwa kufanyika vibaya kwa kazi hapatakuwa na matokeo ambayo yangepatikana kama zoezi lingefanywa kitaalam na kwa nia njema.
Hivi wewe unamtaja Mbowe kwa sababu za kisiasa, Gwajima kwa chuki za kitemi, wakati huo huo unawakwepesha makusudi watu wanaofahamika kimataifa, halafu unalazimisha tupige makofi tukisema "kazi ni njema"?
BTW, Watu waliandamana polisi ajili ya Gwajima. Gwajima aliyetajwa unayemsema ni adui, je ni kweli sasa ni shabaha sahihi? Kazi zingine hazihitaji ushabiki na wala hazina kura. Ni suala la kweli, na haki kwa mujibu wa sheria. Makonda ana mamlaka gani ya kuwaita watu kwenda kituo cha polisi?
Jifunze kuchambua, kutofautisha na kuwaelewa watu kile wanachokisema. Epuka sana kubeba mambo mzobemzobe kwa bei ya jumla kwa sababu unanunua mauti ililyopambwa kwa marham!.