We ndugu haueleweki. Sasa hapa kwani unamuomba nani au unamdai nani hiyo mahakama ya kadhi. Mmesharuhusiwa muanzishe huko kwenye misikiti na taasisi zenu. Hamjakatazwa! Ila kwa kuwa katiba inaongelea watu wa dini,kabila,rangi na jinsia zote,mahakama ya kadhi haitoingizwa. Anzisheni kama wakristo,wahindu,mabudha,wapagani,machifu,wapagani nk walivyoanzisha mahakama yao na wanaiendesha wenyewe bila kugombana na yeyote. Hata wakristo hawapingi ninyi kuwa na mahakama ya kadhi. Bali muianzishe wenyewe,muiendeshe na muigharamie wenyewe. Hatuitaji kodi za wakristo,wapagani,wahindu,mabohora,mabudha,masingasinga nk ambao hata hawamjui kadhi,eti zilipie mahakama ya kadhi.Musiifanye ni jambo la watanzania wote mpaka eti liwekwe kwenye katiba.Mfano: Kwa wakatoliki na madhehebu mengi ya kikristo mwanamme akimuacha mkewe wa ndoa na kuchukua mwanamke mwingine,mwanamke akishtaki kanisani na mwanamme akionekana ana makosa,huwa anafungiwa kushiriki huduma zote za kanisa. Mwanaume huyu hata aende mahakama za serikali hatosikilizwa kwa hiyo hukumu. Sasa ninyi mnashindwa nini kuanzisha hiyo kitu mradi tu msikinzane na sheria za nchi? Au mnataka kuja kuwa juu ya sheria za nchi?.Kipi haujaelewa hapo?