Kuhusu Mahafali ya 11 ya Chuo cha ulinzi wa Taifa- NDC, Kuna Jambo sijalielwa. Si cha kijeshi tu?

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,232
6,479
Nafuatlia Mahafali ya kumi na moja ya Chuo Cha Cha ulinzi wa Taifa-NDC kupitia TBC. Mimi nimekuwa nikivutiwa na mambo ya Jeshi mfano gwaride na tifaki mbalimbali za Kijeshi.

Sasa leo nachukua Rimoti nashusha kila channel nakuta mambo niyapendayo. Nakuta Mahafali ya Chuo chetu Cha ulinzi wa Taifa-NDC.

Mimi siku zote nilijua hiki ni chuo cha kijeshi tu. Nimeona watu mbalimbali kutoka JWTZ, Tanzania Police, Uhamiaji, Magreza, Zima Moto, Majeshi ya nchi jirani na mbali kutoka China, India, Thailand, Egypt nk wakitunukiwa uhitimu chuoni hapo.

Sasa kilichonishangaza ni kuwaona raia kutoka Wizara zetu mbalimbali Kama kilimo, Ujenzi, mifugo, uvuvi nk nao wakitunukiwa uhitimu chuoni hapo. Je imekaaje hili?

National Defence College maana yake ni Chuo Cha ulinzi wa Taifa-NDC. Mgeni Rasmi ni Makamu wa Rais.

Nisaidieni ni kwanini hao watumishi au raia wa kawaida wanaofanya kazi wizarani, inakuwaje wamesoma na kuhitimu pamoja na maafisa wa Kijeshi?
 
Jukumu la ulinzi ni la kila raia hivyo usishangae. wengi mnajua ulinzi ni mitutu ya bunduki na mizinga tu. Dhana ya ulinzi wa Taifa ni pana sana. Hivyo usishangae siku ukiona Padre au Shehe fulani au Msanii fulani aki graduate pale
 
Hussein Bashe, Tulia Ackson, Zitto Kabwe, Jumaa Aweso na Sophia Mgema walimaliza masomo ya TISS siku moja. Usishangae kuwaona. Baadhi ya watunukiwa kutoka nchi za kigeni sio wahitimu 100%. Wengi wao wanatusaidia kufundisha mbinu za medani na ujasusi wala sio wanafunzi wa Chuo. Kumbuka TISS Iko chini ya ofisi ya Makamu wa Rais na si Rais Hadi sheria Mpya ya juzi ya idara hiyo.....
 
Back
Top Bottom