National Defense College (NDC) Watembelea Wilaya ya Ludewa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

National Defense College (NDC) watembelea Wilaya ya Ludewa

Washiriki wa kozi ya Ulinzi na Usalama ambao ni wanakozi kutoka katika vyombo vya Ulinzi na Usalama na taasisi mbalimbali za mataifa 8 Duniani, ikiwemo wenyeji Tanzania ambao wapo mafunzoni katika Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (National Defence College- NDC) kilichopo jijini Dar-es- Salaam wamewasili Wilayani Ludewa mkoani Njombe kwa ziara ya mafunzo.

Ziara huyo ilihusisha Kutembelea Miradi ya kiserikali (TANROAD) na kiuchumi mbalimbali ambapo wamepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva aliye ambatana na Kamati ya Usalama pamoja na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Sunday Deogratius.
Ziara hiyo ya NDC imeongozwa na Brigedia Jenerali EE Mhoro ambapo walipata fursa ya kujifunza kutoka Ludewa, Mkoani Njombe.

Uongozi wa Wilaya ya Ludewa- ulishirikiana bega kwa bega na ziara yao iliyohusisha kutembelea kiwanda kidogo cha kufua Umeme cha Kisangani, na Kuyeyusha Chuma- Kisangani.
Mwisho wa Ziara hiyo- NDC walitoa zawadi za Chuo hicho kwa uongozi wa Wilaya na Uongozi wa Wilaya ulipata fursa ya kutoa zawadi ya Asali bora ya Ludewa kwa washiriki wote wa kozi kama sehemu ya kuwashukuru na kuwakaribisha tena katika Wilaya ya Ludewa.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-01-21 at 12.17.15(2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-21 at 12.17.15(2).jpeg
    116.9 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-01-21 at 12.17.13.jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-21 at 12.17.13.jpeg
    127.9 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-01-21 at 12.17.13(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-21 at 12.17.13(1).jpeg
    121.4 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-01-21 at 12.17.13(2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-21 at 12.17.13(2).jpeg
    137.7 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-01-21 at 12.17.14.jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-21 at 12.17.14.jpeg
    149 KB · Views: 5
Back
Top Bottom