Kuhusu cheo cha Mufti na Ayatollah

Kuhusu cheo cha Mufti na Ayatollah

Ninavyojua ni kuwa Iran ni nchi ya kiislam Kwahiyo Ayatollah anakuwa kiongozi mkuu wa dini na serikali tofauti na wabongo yeye yupo kwa ajili ya waislam tu kuwaongoza kwa mambo ya dini
Hapana ndugu, wako ma Ayatullah wengu hata nje ya Iran. Ayatullah ni daraja la kisomi mtu anafikia kwa kusoma kama vile mtu anafikia kua Daktari wa falsafa. Mfano kuna waliopo India, Lebano au Itaq
 
Ayatollah anachaguliwa na Baraza la wataalamu.
'Baraza la wataalamu' badala ya raia wote, halafu anakuwa ni sauti ya mwisho kuliko Rais aliyechaguliwa kidemokrasia na hawajibishwi na yeyote na hana ukomo wa utawala!

Kuna tofauti gani na Mfalme ama Sultani?
 
Hapana ndugu, wako ma Ayatullah wengu hata nje ya Iran. Ayatullah ni daraja la kisomi mtu anafikakia kwa kusoma kama vile mtu anafikia kua Daktari wa falsafa. Mgano kuna waliopo India, Lebano au Itaq
Mbona wanachagua ayatollah mpya kama wapo wengi kiongozi

Inawezekana kweli wapo wengi mimi sijui hilo ila kwa Iran ninavyojua ni kiongozi mkuu
 
Wakuu hivi cheo alicho kuwa nacho ayatollah yule jamaa aliepigwa bomu ndo sawa na cheo cha mufti wetu hapa Tanzania?

Asante
Ayatollah anakuwa msomi wa juu wa dini ya Kiislamu kwa dhehebu la Shia, sio mjinga wala kichwa maji. Anakuwa amesoma kwenye sheria za kidini na miongozo yake kwa elimu ya kidunia ni sawa kabisa kabisa na Professor.

Hayupo Ayatollah mmoja wapo wengi tu kidini ila kisiasa ndio anachaguliwa mmoja pale Iran na Assembly of Experts, ambalo hili huchaguliwa na wananchi kwa muhura wa miaka nane. Kwahiyo Ayatollah hachaguliwi direct na wananchi bali na "wajuvi wa mambo" waliochaguliwa na wananchi. Haiwezekani wewe muuza uji, na rafiki yako muuza mapera eti mjue sifa za kiongozi mkuu wa nchi wa kuleta teknolojia, kulinda umoja, kukuza uchumi na maslahi mengine ya kitaifa. Lazima mtachagua kilaza ilimradi ni maarufu na anaongea sera nyepesi.

Kwa kuwa wapo Ayatollahs kadhaa, mkuu wa nchi anakuwa Grand Ayatollah. Ila si lazima sana awe alikuwa cheo hicho maana sio cha kusomea bali kuteuliwa kutokana na unavyokubalika na waumini, uwezo mkubwa wa kiakili na utatuzi wako wa migogoro ilivyo. Ni kama ambavyo hakuna chuo cha kufundisha kuwa Professor.

Sasa pale cheo cha chini ya Ayatollah kinaweza kukaguliwa na kuona kinafaa vigezo then mtu huyo akawa Ayatollah na akawa mkuu wa nchi (kumbuka Ayatollahs wana umakini na akili kuna sababu kwanini wanafanya hivi). Ayatollah Khamenei hakuwa Ayatollah wakati anachaguliwa kuwa mkuu, hata mwanae huyu anayetarajiwa na wengi Mujtaba sio Ayatollah kidini yuko cheo cha chini yake.
 
'Baraza la wataalamu' badala ya raia wote, halafu anakuwa ni sauti ya mwisho kuliko Rais aliyechaguliwa kidemokrasia na hawajibishwi na yeyote na hana ukomo wa utawala!

Kuna tofauti gani na Mfalme ama Sultani?
Mfalme au Sultan hachaguliwi kabisa, Bora uchaguzi wa Iran kuliko wa bongo.
 
Back
Top Bottom