Chifu mkuu
JF-Expert Member
- Jan 6, 2025
- 552
- 650
TANZANIA HAINA MUFTI !
TANZANIA HANA SHEKH MKUU!
Kwa muda mrefu tumekuwa tukisikia kiongozi mkuu wa taasisi ya kidini iitwayo Baraza kuu la waislamu wa Tanzania bara akitajwa kama mufti na sheikh mkuu wa Tanzania na mtazamo huu ni makosa makubwa sana na uamebeba maudhui ya upotoshaji kwa kumvika mtu cheo ambacho kiuhalisia hakipo na hakiwezekani kuwepo kwa sababu zifuatazo;
1️⃣ Unapozungumzia Tanzania ni pamoja na visiwa vya unguja na Pemba ambavyo vipo chini ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ndani ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa sababu kimataifa tunajulikana kama taifa moja tunaotumia sarafu moja na passport moja iliyoandikwa TANZANIA.
Zanzibar hawana passport maalumu kwa ajili yao kwakuwa wao ni watanzania na wanatumia Passport ya Tanzania.
Lakini pamoja na hayo upande wa maswala ya kidini taasisi za kiislamu za Tanzania bara hasa bakwata ni kama vile haziruhusuwi kuwa na office katika visiwa vya unguja na Pemba.!.
Waislamu wa Zanzibar wanaye mufti wao anayeteuliwa na mh Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi na yeye mufti na wasaidizi wake ambao baadhi yao huteuliwa na mh waziri wa katiba na sheria wa Zanzibar hufanya kazi chini ya wizara ya katiba na sheria ya Zanzibar .
Ofisi ya Mufti wa Zanzibar inafanya kazi chini ya serikali ya Zanzibar na BAKWATA hawana office katika visiwa vya unguja na pemba jambo linaloonyesha kwamba kama bakwata ingekuwa taasisi ya kisiasa tungesema BAKWATA sio katika mambo ya muungano kwakuwa majukumu ya bakwata ni upande wa Tanzania bara tu!
Sasa ikiwa hali iko hivyo BAKWATA wanajiitaje Baraza kuu la waislamu Tanzania wakati hawana ofisi upande wa Zanziba?!.
Na tunasemaje kiongozi mkuu wa BAKWATA ni mufti na sheikh mkuu wa Tanzania wakati hana wawakilishi wanaofanya kazi chini yake upande wa Zanzibar kama ilivyo katika mikoa , wilaya na kata za Tanzania bara?!
2️⃣ Sababu ya pili kwanini Tanzania haina Mufti wala sheikh mkuu ni kwakuwa serikali ya Tanzania imetoa uhuru wa kuabudu na imeruhusu uwepo wa taasisi nyingine za kiislamu kuanzishwa.!
Kupitia ruhusa hiyo na kwakuwa kuna baadhi ya waislamu ambao hawakubaliani na itikadi, fikra , sera na misimamo ya Bakwata wameanzisha taasisi nyingine za kiislamu na kuweka viongozi wanaowakubali ambao kulingana na katiba ya kila taasisi viongozi hao nafasi zao huwa na majina tafauti tafauti kama vile MUDIRU, AMIRI, MWENYEKITI, KATIBU MKUU NK na kimajukumu unakuta kila kiongozi mkuu ndani ya taasisi yake anafanya kazi sawa na zilezile anazozifanya sheikh mkuu wa BAKWATA na pia kila taasisi ya kiislamu inajitegemea katika kujiendesha bila kutegemea wala kuingilia mambo ya taasisi nyingine!
Ingekuwa Mufti wa BAKWATA ndiye msimamizi na kiongozi mkuu wa waislamu wote Tanzania serikali isingeruhusu kuanzishwa taasisi nyingine za kiislamu kufanya kazi zilezile zinazofanywa na BAKWATA kwasababu uwepo wa taasisi hizi kunasababisha migongano baina ya waislamu.
Ndio maana kila unapoingia na kumalizika mwezi wa Ramadhani utamsikia mufti wa BAKWATA akiwalalamikia watu wanaotangaza kuandama kwa mwezi wa kuingia Ramadhani au kumaliza Ramadhani kwa kuwa yeye Mufti anaamini kwamba ni shehe wa waislamu wote na kwamba haitakiwi mtu mwingine atangaze habari za kuingia au kumalizika Ramadhani kabla yake na AMEKUWA AKIICHOCHEA SERIKALI KUWACHUKILIA HATUA WATU WANAOTANGAZA MWEZI KABLA YAKE LAKINI SERIKALI IMEKUWA IKIMPUUZA KWAKUWA SIO KAZI YA SERIKALI KUINGILIA MAMBO YA IBADA ZA WATU KATIKA NCHI HII.
Kwahiyo yeye anatakiwa atambulike kama Mufti na sheikh mkuu wa BAKWATA na siyo sheikh wa Tanzania kwa sababu ndani ya nchi hii Kuna waislamu wengi ambao hawakubaliani na madhehebu, fikra na sera za bakwata na wana viongozi wao wanaowakubali kulingana na itikadi zao za kimadhehebu na wanazo taasisi ambazo serikali inazitambua.