Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,866
- 4,252
Habari za mchana.
Leo nimepata nafasi ya kusikiliza hotuba ya bajeti toka kwa Waziri. Pamoja na deni la Taifa kuendelea kukua, hii itupe ishara kwamba tunaenda uelekeo usio sahihi. Sijui ni kwa nini wananchi huku chini wanasononeka ila wakubwa huko juu wako kimya.
Kubwa ninalotaka kulisemea hapa ni kule mwanzo wa utangulizi wa bajeti hasa kuhusiana na usalama na amani ya Taifa letu. Waziri kazungumzia kuhusu viashiria vya uvunjifu wa amani na kwamba vita ya kupiganwa sio ya kutangaza bali ni ya kiintelijensia zaidi. Kiukweli hapo wanjua wao zaidi. Anasema tusiruhusu misingi na nguzo za Taifa letu vitikiswe. Kika nani wanatikisa? Kwa nini wanatikisa? Imefikiaje hadi kujua kuna mitikisiko? Ni lazima kuna sababu.
Kwa nini tusingalie sababu kwanza hadi tuje kukimbilia kuonyana na kupeana maneno ya kuogofya? Kama vyombo vyetu havijawahi kushindwa kwenye figisu kadhaa dhidi ya chokochoko za kimataifa na ndani ya nchi, iweje leo wasiojulikana wanaendelea kutojulikana?
Waziri hakupenda kabisa kugusia suala la utekaji na watu waliopotea katika kipindi cha karibuni. Mtizamo wangu hapa ni kwamba, walioko madarakani wanatamani kuendelea kuwepo hapo. Bila kujali ni madhara kiasi gani yanafanyika kwa kudhibiti hali, hawataki kutizama vyanzo vya shida zote. Yaani, watu wanaona mtu kapigwa shoti na umeme umemg'ag'ania.
Yupo mtu kando ya main switch ambapo angeweza kabisa kuzima umeme wote. Shida ni kwamba hataki kugusa swichi ili waendelee kumwona mwathirika katika mwanga na kutafuta mbinu zingine za kumwokoa. Uwepo wa shoti ni faida kwao. Pale ambapo watu wataendelea kunaswa na juhudi za kuwanasua zikifanyika, tena kwa chini ya kiwango, kwao ni faida mara mbili. Kudumisha tatizo na pili ni ushuhuda kwamba wanapambana kuokoa maisha ya wanaonaswa na umeme.
Kwani mtu akinaswa na mkazima umeme wote mnapungukiwa na nini? Kwani mkizuia watu wasipite njia ya huo umeme mnapungukiwa na nini? Kwani mkiondoa umeme kwenye hiyo njia mnapungukiwa na nini? Kwa bahati mbaya ni njia kuu hivyo haina budi watu kuendelea kupita. Mwisho wapitaji wataujua mchezo na watatafuta namna ya kukabiliana na huo umeme