Kufungulia Nchi? Kurudi Kujivunia Umaskini?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,255
2,000
Inawezekana wakati mama anaenda kufungulia nchi anaweza kufungulia hizi hisia za kutukuza na kukumbushana juu ya kile kinachoitwa umaskini wetu?

Tunatakiwa kutokujaribu au kuthubutu kufanya makubwa kwa sababu sisi ni masikini? Ndio mwanzo wa kuanza kuombaomba tena...maskini wa fikra hatajiriki na hawezi kutoka kwenye umaskini ambao anaamini unamnufaisha. Inanikumbusha kile kisa cha"Mtumwa Mpendwa" aliyefurahia kupendelewa na bwana wake hadi siku ile yule bwana alipokufa.

Mama ana kazi na kibarua kigumu..maana hata kufoka hawezi na akiwabwatukia watalia hawa kama watoto waliodekezwa, wakadeka, na kudekeka..mtaa mzima utawasikia...na hawanyamazi hadi wapewe "fanta"
 

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
6,971
2,000
China chini ya Deng Xiaoping alifungulia nchi, huku ndiko mama anavyomaanisha.
Kuondoa vikwazo vya kipuuzi vya kuleta investment na kuondoa urasimu kwenye kuanzisha business.

Sasa kufungulia nchi na kuomba mbona haviendani naona mko busy kutwist maneno yake na kuyafanyia spinning ili kupotosha!

So far so good, Nchi inaenda vizuri vhini ya mama Samia, kafanya kazi nzuri sana kwenye siku zake 50 za kushika usukani, aneonyesha njia nzuri mno
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
10,956
2,000
China chini ya Deng Xiaoping alifungulia nchi, huku ndiko mama anavyomaanisha.
Kuondoa vikwazo vya kipuuzi vya kuleta investment na kuondoa urasimu kwenye kuanzisha business.

Sasa kufungulia nchi na kuomba mbona haviendani naona mko busy kutwist maneno yake na kuyafanyia spinning ili kupotosha!

So far do good, Nchi inaenda vizuri vhini ya mama Samia, kafanya kazi nzuri sana kwenye siku zake 50 za kushika usukani, aneonyesha njia nzuri mno
Kwanza unalinganisha nchi tofauti kabisa China ya Xiaping na Tanzania ya Samia, hilo ni kosa lakwanza linaloonyesha hujui mlinganisho hata kabla ya kuzungumzia mengine.
China ya Xiaoping ilikuwa tayari. Hawakufungulia tu holela kila takataka zije kuondoa hicho walichokuwa tayari wamekiweka sawa kiwaletee manufa.

Tanzania ya Samia, hivi ni lini imefungwa, na imefungwa vipi? Wawekezaji walizuwiwa kuja kuwekeza; au nati zilikazwa ili wakija hapa wasitufanye kama shamba la bibi?
Nitaonekana kama shabiki wa Magufuli kwenye mambo haya; lakini sikuwahi kupenda yale maovu yake.

Mama asitupeleke tena kujinadi na kunadi mali za taifa hili kwa hasara ya wananchi wake. Ni wakati angalau ahimize, waTanzania wachangamkie fursa nyingi tu zilizopo hapa na aweke mifumo ya kuwawezesha kuliendeleza taifa hili, na siyo kuonyesha kana kwamba maendeleo ya nchi hii bila ya wawekezaji toka nje haiwezi kuendelea. Huku ni kujidharau kusikofaa kabisa.

Na usije ukanirukia na kusema sitaki wawekezaji wa nje. Waje kwa wingi, lakini kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania na sio kuja kupora mali zao.
 

ANKOJEI

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
1,001
2,000
Nchi ifunguliwe na kupanuliwa, wawekezaji wajae mpka kule Namtumbo, tupate hela ya kula na kunywa, hii ndio ndoto ya mama, kana kwamba wawekezaji walikuwepo tu hapo kenya wanasubiri kuingia tz?

Swali muhimu je ni kweli mama anaamini wawekezaji muhimu wa Tanzania wapo Kenya? au kuna namna alienda kujikinga na kupata mbinu za kupata misaada ya covid19? mana hata askari alibadilishiwa ghafla.
 

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,250
2,000
Kwanini mnalazimisha kuingia kwenye mjadala ambao huna uwezo nao?
China chini ya Deng Xiaoping alifungulia nchi, huku ndiko mama anavyomaanisha.
Kuondoa vikwazo vya kipuuzi vya kuleta investment na kuondoa urasimu kwenye kuanzisha business.

Sasa kufungulia nchi na kuomba mbona haviendani naona mko busy kutwist maneno yake na kuyafanyia spinning ili kupotosha!

So far so good, Nchi inaenda vizuri vhini ya mama Samia, kafanya kazi nzuri sana kwenye siku zake 50 za kushika usukani, aneonyesha njia nzuri mno
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
10,956
2,000
Kumbuka hayo maneno aliyasemea wapi.

Maana yake ililenga hadhira hiyo. Bila shaka baada ya kunogewa aliyoyasikia yakisemwa mahala hapo.

Sasa katika kunogewa huko, asije akajisahau kwamba kazi yake kubwa ni kuwapambania waTanzania na siyo wahusika wa mkutano huo pekee.

Picha ninayoiona kama atatimiza dhamira hiyo ya "kufungua nchi", tutaanza kuona maluweluwe mengi na hadaa chungu nzima huku jamaa wakibeba tunavyotegemea vitunyanyue sisi.
 

samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
8,607
2,000
Tukiacha ushabiki awamu ya tano nchi ilikuwa imejifunga na hali ya mzunguko wa hela ilikuwa ngumu kuanzia kwa wafanyabiashara mpaka wafanyakazi.... ushahidi ni pale JPM mwenyewe kila meimosi alipogoma kuongeza mishahara na kusema mpaka miradi iishe, upande mwingine makampuni kadhaa yalifunga biashara na confidence ya uwekezaji ikawa imeshuka kabisa.. Serikali awamu ya tano ilitoa watu kazini maelfu kwa kisingizio cha vyeti feki na haikuajili kureplace hao waliotoka, Serikali iliacha kuajili maelfu kwa malaki wakabaki mtaani hawana kazi.

Mbinu zilizotumika awamu ya tano kwa kuwataka watu wafunge mikanda ndio maendeleo yaje, ni mbinu za kizamani, karne ya sasa modal za uchumi ni kuleta maendeleo kwa pamoja kwa maana ya maisha ya watu na vitu kwa pamoja hiyo ndio akili.... na ndio tunaposema nchi imefunguka.

Uchumi wa Tanzania ni mdogo, uzarishaji wa Tanzania ni mdogo, watanzania ni masikini wa akili na kipato huu ndio ukweli bila propaganda..Kuifungua nchi ni kufanya wepesi wa mitaji kuja na watanzania kuingia kwenye mzunguko, watu kuja watanzania kupata uzoefu na exposure, investments kubwa kufanyika maelfu na malaki wapate ajira serikali iingize kipato.

Mwisho kabisa, nitajie awamu moja toka uhuru ambayo haijawahi kusaidiwa, kukopeshwa au kupewa msaada.
 

WALOLA VUNZYA

JF-Expert Member
Nov 20, 2020
662
1,000
Inawezekana wakati mama anaenda kufungulia nchi anaweza kufungulia hizi hisia za kutukuza na kukumbushana juu ya kile kinachoitwa umaskini wetu? Tunatakiwa kutokujaribu au kuthubutu kufanya makubwa kwa sababu sisi ni masikini? Ndio mwanzo wa kuanza kuombaomba tena...maskini wa fikra hatajiriki na hawezi kutoka kwenye umaskini ambao anaamini unamnufaisha. Inanikumbusha kile kisa cha"Mtumwa Mpendwa" aliyefurahia kupendelewa na bwana wake hadi siku ile yule bwana alipokufa...

Mama ana kazi na kibarua kigumu..maana hata kufoka hawezi na akiwabwatukia watalia hawa kama watoto waliodekezwa, wakadeka, na kudekeka..mtaa mzima utawasikia...na hawanyamazi hadi wapewe "fanta"
Unyonge Unyonge sasa basi.
 

sonofobia

JF-Expert Member
Jun 21, 2015
480
1,000
Inasikitisha sana ukifuatilia page na post mbalimbali za Chadema wanavyotukanwa kwenye comments na wachangiaji.
Kuna group linaitwa Chadema in blood kule facebook yani kila wanachopost ni kutukanwa tu na watu, huko instagram ndiyo balaa kabisa, njoo Jamii forum hali ni hiyo hiyo!

Nimeangalia comments za kwenye hotuba ya Mbowe aliyoitoa akisema vibaya utawala wa hayati Magufuli, kwa kweli ni huzuni raia walivyomtukana Mbowe. Swali la kujiuliza Chadema imefikaje huku?

Enzi za Dr Slaa ulikuwa unavaa gwanda la Chadema kwa maringo yote ,leo tuvae kwa aibu ya kujifichaficha?
Je Tundu Lisu ameharibu image ya chama baada ya kuanza kutetea mabeberu?

Je ni Mbowe ameharibu image ya chama baada ya kuwa anaangushwa na konyagi anasingizia amepigwa na wasiojulikana?, au ule uongo wake wa kuibia familia inapompeleka mahakamani anasingizia amefungiwa akaunti zake na serikali??

Kiukweli inahitajika tathimini ya haraka sana kuikoa na kuirudisha Chadema kwa wananchi ili waiamini tena kama zamani.
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,905
2,000
Jiwe alikopa kupitiliza kiasi kwamba wanaomrithi wanabeba mzigo wa madeni na kuathiri mipango na malengo yao kwa nchi.

Umesahau Jiwe alimuomba Mfalme wa Morocco atujengee msikiti na uwanja wa mpira kule Dodoma?

CCM karibu wote ni failure kwenye kila kitu na hakuna mwenye haki ya kumlaumu mwingine.

Acheni unafiki, Magu kaharibu sana hii nchi .
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom