Kufungulia Nchi? Kurudi Kujivunia Umaskini?

China chini ya Deng Xiaoping alifungulia nchi, huku ndiko mama anavyomaanisha.
Kuondoa vikwazo vya kipuuzi vya kuleta investment na kuondoa urasimu kwenye kuanzisha business.

Sasa kufungulia nchi na kuomba mbona haviendani naona mko busy kutwist maneno yake na kuyafanyia spinning ili kupotosha!

So far so good, Nchi inaenda vizuri vhini ya mama Samia, kafanya kazi nzuri sana kwenye siku zake 50 za kushika usukani, aneonyesha njia nzuri mno
Mtulivu.
Ana hekima
Busara
Hana maneno makali
Anathamini utu wa wengine
Anatengeneza urafiki na kila mtu.

HAYA YALIMSHINDA JOHN, HATA ALIPOELEKEZWA HAKUKUBALI
 
M
1. Huogopi kuitwa MATAGA?

2. Wewe ni Sukuma Gang!

3. Utaambiwa unamchukia Mama 🤣.

4. Usisahau kuwa huyu Mama hakosolewi! Ukithubutu tu, utaambiwa unamtaka Magufuli ila bahati mbaya harudi tena!
Mzee mwenzangu baada ya miaka zaidi ya ishirini ya kuitwa Kila majina kwenye mitandao sidhani kama hawa wanaweza kunishtua.... Ila tunao hawa.
 
China chini ya Deng Xiaoping alifungulia nchi, huku ndiko mama anavyomaanisha.
Kuondoa vikwazo vya kipuuzi vya kuleta investment na kuondoa urasimu kwenye kuanzisha business.

Sasa kufungulia nchi na kuomba mbona haviendani naona mko busy kutwist maneno yake na kuyafanyia spinning ili kupotosha!

So far so good, Nchi inaenda vizuri vhini ya mama Samia, kafanya kazi nzuri sana kwenye siku zake 50 za kushika usukani, aneonyesha njia nzuri mno
Usingetolea mfano wa 邓小平 kwa sababu haviendani na utaratibu wa nchi yetu kiuchumi.acheni kuwa mnatolea mlinganyo wa mataifa yenye njia tofauti za uchumi na uthubutu.
 
1. Huogopi kuitwa MATAGA?

2. Wewe ni Sukuma Gang!

3. Utaambiwa unamchukia Mama .

4. Usisahau kuwa huyu Mama hakosolewi! Ukithubutu tu, utaambiwa unamtaka Magufuli ila bahati mbaya harudi tena!
Ukikosoa tu utashambuliwa na makundi makubwa yakiwemo MATAPA, akina bwa shee, wanawake (wale wa gruuu), baadhi ya wanadini na upande wa pili ukivuka maji.
 
Kwanza unalinganisha nchi tofauti kabisa China ya Xiaping na Tanzania ya Samia, hilo ni kosa lakwanza linaloonyesha hujui mlinganisho hata kabla ya kuzungumzia mengine.
China ya Xiaoping ilikuwa tayari. Hawakufungulia tu holela kila takataka zije kuondoa hicho walichokuwa tayari wamekiweka sawa kiwaletee manufa.

Tanzania ya Samia, hivi ni lini imefungwa, na imefungwa vipi? Wawekezaji walizuwiwa kuja kuwekeza; au nati zilikazwa ili wakija hapa wasitufanye kama shamba la bibi?
Nitaonekana kama shabiki wa Magufuli kwenye mambo haya; lakini sikuwahi kupenda yale maovu yake.

Mama asitupeleke tena kujinadi na kunadi mali za taifa hili kwa hasara ya wananchi wake. Ni wakati angalau ahimize, waTanzania wachangamkie fursa nyingi tu zilizopo hapa na aweke mifumo ya kuwawezesha kuliendeleza taifa hili, na siyo kuonyesha kana kwamba maendeleo ya nchi hii bila ya wawekezaji toka nje haiwezi kuendelea. Huku ni kujidharau kusikofaa kabisa.

Na usije ukanirukia na kusema sitaki wawekezaji wa nje. Waje kwa wingi, lakini kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania na sio kuja kupora mali zao.
Umemaliza kila kitu. Asante.
 
China chini ya Deng Xiaoping alifungulia nchi, huku ndiko mama anavyomaanisha.
Kuondoa vikwazo vya kipuuzi vya kuleta investment na kuondoa urasimu kwenye kuanzisha business.

Sasa kufungulia nchi na kuomba mbona haviendani naona mko busy kutwist maneno yake na kuyafanyia spinning ili kupotosha!

So far so good, Nchi inaenda vizuri vhini ya mama Samia, kafanya kazi nzuri sana kwenye siku zake 50 za kushika usukani, aneonyesha njia nzuri mno
Unasema ukweli mtupu hii nchi ilitolewa kabisa katika utaratibu tulijitenga na kila nchi iliyotuzunguka na ndani nchi ilikuwa ikiongozwa kwa amri za magufuli hakuna sheria wala katiba tunashuku mungu kututowa katika madhila yale.
 
Inawezekana wakati mama anaenda kufungulia nchi anaweza kufungulia hizi hisia za kutukuza na kukumbushana juu ya kile kinachoitwa umaskini wetu?

Tunatakiwa kutokujaribu au kuthubutu kufanya makubwa kwa sababu sisi ni masikini? Ndio mwanzo wa kuanza kuombaomba tena...maskini wa fikra hatajiriki na hawezi kutoka kwenye umaskini ambao anaamini unamnufaisha. Inanikumbusha kile kisa cha"Mtumwa Mpendwa" aliyefurahia kupendelewa na bwana wake hadi siku ile yule bwana alipokufa.

Mama ana kazi na kibarua kigumu..maana hata kufoka hawezi na akiwabwatukia watalia hawa kama watoto waliodekezwa, wakadeka, na kudekeka..mtaa mzima utawasikia...na hawanyamazi hadi wapewe "fanta"
Mzee wangu Mwanakijiji leo unahasira, ni Sawa kabisa kwani hata mimi mjukuu wako ninazo pia tena pima, zimejaa pomoni, ile nuru imezima katikati ya tafrija, maandishi yakambeba mama, akakiri kuwa na jinsi ya kike lakini yeye ndiye rais na salam mpya kutufundisha. HEWALA SI UTUMWA.

Unayo haki ya kukasirika, nchi haiendeswi kwa huruma, hii si familia bali nchi. Tumepiga U-TURN bahati mbaya hatujui sababu.

Naumia sana kuona nchi yangu ikirudi hatua 10 nyuma na bila kujali watu wanapiga makofi ya hongera.

WACHA TUISHI, NDIO TUISHI KWA KUWA KUISHI NI KAZI NGUMU KULIKO KUFA.
 
Sijui kwanini Wasukuma wana mambo ya kishamba kiasi hiki, Huyu Jamaa alikua kutwa kucha kumsifia Magufuli! Anashindwa kabisa kuzuia hisia zake na haamini kuwa Magufuli amekufa.

Such a nonsense article, ni wapi kufungulia nchi ndio kufungulia umaskini?
Kwani lini Tz ilikua tajiri? na lini ilifilisika?
 
Inawezekana wakati mama anaenda kufungulia nchi anaweza kufungulia hizi hisia za kutukuza na kukumbushana juu ya kile kinachoitwa umaskini wetu?

Tunatakiwa kutokujaribu au kuthubutu kufanya makubwa kwa sababu sisi ni masikini? Ndio mwanzo wa kuanza kuombaomba tena...maskini wa fikra hatajiriki na hawezi kutoka kwenye umaskini ambao anaamini unamnufaisha. Inanikumbusha kile kisa cha"Mtumwa Mpendwa" aliyefurahia kupendelewa na bwana wake hadi siku ile yule bwana alipokufa.

Mama ana kazi na kibarua kigumu..maana hata kufoka hawezi na akiwabwatukia watalia hawa kama watoto waliodekezwa, wakadeka, na kudekeka..mtaa mzima utawasikia...na hawanyamazi hadi wapewe "fanta"
Kwa kifupi mama anairudisha nchi nyuma, period
 
Watanzania tunataka nini?
Siku ukiielewa kauli hii ndio utajua ni nini hawa watu walitaka.

...............Safi sana Mama kasema mwendo ni ule ule, lazima waisome namba.

Hapo utajiuliza, ina maana kazi ya Rais ni kusomesha namba watu, kuumiza watu, kutaabisha watu au kuteka na kuua watu.

Then, utakuja kugundua kuna watu ambao furaha yao huwa ni kuona watu wanaumizwa, kuuawa na kutaabishwa na bahati nzuri walifanikiwa kuwa na mtu wao Ikulu miaka 5 iliyopita na mpaka sasa hawaamini kilichotokea.

Ukisikia ile stori ya malaika kumtokea mtu mmoja na kumwambia aombe kitu kimoja ambacho, akipewa jirani yake atapata mara mbili. Huyo mtu akaamua kuomba atolewe jicho moja, ili jirani yake atolewe macho yote awe kipofu ndio utawaelewa vizuri watu wa aina hii.

Ni watu ambao siku zote wanafurahia makatili kama kina Sabaya, Makonda, Chalamila. Huwezi kuwakuta wanamfagilia kiongozi kama Antony Mtaka au Anna Mgwira.

Wao wako tayari kuvumilia hata mateso au sheria kandamizi ili mradi tu hizo sheria zinawaumiza watu wengine pia.

Na binafsi huwa naona ndivyo walivyo kimaumbile, hawawezi kuwa tofauti hata kama wakijifanya watu wa dini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom