Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,506
- 113,623
Wanabodi,
With 3 days to go, itimie ile ultimatum ya kuwasilishwa mezani kwa Spika kwa Ripoti ya CAG, leo naendelea na zile makala zangu za uelimishaji umma kuhusu Katiba ya JMT, kwa mtazamo wa mtunga katiba alidhamiria nini kuweka kifungu fulani.
Makala hizi naziendesha kwa mtindo wa maswali ili kutoa fursa kwa mabingwa wa katiba kutufafanulia zaidi, swali la leo ni
"Kufuatia Umuhimu wa Ripoti ya CAG, Jee Wajua Kuwa Rais Wetu Anaamrishwa na Katiba Kuipokea Ripoti Hiyo?, Na Sio Amri Kavu Kavu tuu, bali ni Amri With Ultimatum?. Jee Wajua Hiyo Ulmatum Ikipita, Katiba Inaelekeza Rais Apuuzwe, Ripoti Hiyo Iwasilishwe na CAG mwenyewe?.
Hivyo wajameni, with three days to go, lets rest assured Katiba itafuatwa, na Ripoti ya CAG yenye sahihi ya CAG Prof. Mussa Assad, itawasilishwa mezani kwa Spika kwa mujibu wa katiba.
Nawatakia Jumatatu Njema.
Paskali
KaShivjiKadogo.
Update,
Baada ya Ripoti ya CAG yenye sahihi ya CAG, Prof. Mussa Assad, kuwasilishwa Bungeni kwa mujibu wa Katiba. Uzi huu wa kuhimiza hadhi ya ripoti ya CAG kusingatiwa, umetekelezwa, Ripoti ya CAG, imetendewa haki. Kama Azimio lile la Bunge la kutokufanya kazi na CAG ni azimio halali au batili, limepatikana, ni azimio batili ndio maana limepuuzwa. Ufafanuzi wa Spika kuwa Bunge halitapokea Ripoti ya CAG kama imesainiwa na CAG mwenyewe Prof. Assad, ila itapokelewa kama itasainiwa na mtu mwingine pia ni batili, na imepuuzwa, Ripoti ya CAG iliyowasilishwa Bungeni imesainiwa na CAG, Prof. Assad,
Kiukweli kabisa, kuna mabandiko tunaweka humu JF, yanawasaidia sana watawala wetu, japo huwa hawasemi, ila tunapima kwa matokeo. Hivyo ndugu zangu wana jf, huu mjadala nimeufunga rasmi.
Hongera kwa Bunge letu kufuata Katiba.
P.
With 3 days to go, itimie ile ultimatum ya kuwasilishwa mezani kwa Spika kwa Ripoti ya CAG, leo naendelea na zile makala zangu za uelimishaji umma kuhusu Katiba ya JMT, kwa mtazamo wa mtunga katiba alidhamiria nini kuweka kifungu fulani.
Makala hizi naziendesha kwa mtindo wa maswali ili kutoa fursa kwa mabingwa wa katiba kutufafanulia zaidi, swali la leo ni
"Kufuatia Umuhimu wa Ripoti ya CAG, Jee Wajua Kuwa Rais Wetu Anaamrishwa na Katiba Kuipokea Ripoti Hiyo?, Na Sio Amri Kavu Kavu tuu, bali ni Amri With Ultimatum?. Jee Wajua Hiyo Ulmatum Ikipita, Katiba Inaelekeza Rais Apuuzwe, Ripoti Hiyo Iwasilishwe na CAG mwenyewe?.
- Rais wa JMT ndie mtu mwenye mamlaka makubwa zaidi kuliko mtu mwingine yoyote ndani ya JMT kwa sababu rais wa JMT ndie Mkuu wa Mkuu wa nchi, Head of State, Mkuu wa Serikali, Head of Government, na Amiri Jeshi Mkuu, hivyo kila kitu kinachofanywa na kiongozi yoyote wa serikali, idara au wakala, kinafanywa kwa niaba ya rais wa JMT, hata CAG anafanya ukaguzi kwa niaba ya rais wa JMT, hata Ripoti ya CAG ni Ripoti ya rais wa JMT, hivyo rais JMT ndio kila kitu.
- Ibara ya 37 ya Katiba inaelekeza katika jambo fulani, Rais wa JMT anaweza kushauriwa na yeyote lakini katika kufikia maamuzi, rais anafikia maamuzi yeye mwenyewe kama rais, bila kulazimika kufuata ushauri wa yoyote "in the performance of his duties and functions, the President shall be free and shall not be obliged to take advice given to him by any person, save where he is required by this Constitution or any other law to act in accordance with the advice given to him by any person or authority.
Act " hivyo rais Magufuli alipotamka kuwa hapangiwi, he was right rais wa JMT hapangiwi kitu na mtu. - Ila hili la rais kutopangiwa kitu na mtu yoyote linamfanya rais wa JMT kuwa ndiye mtu mwenye mamlaka kuu kuliko mtu yoyote mtu yoyote ndani ya JMT ila pia mamlaka hizo sio juu ya Katiba bali ni ndani ya katiba. Hivyo tunapozungumzia ukuu wa Katiba, Katiba ya JMT ndio mamlaka kuu kuliko mamlaka nyingine zote, na rais yuko chini ya Katiba, ndia maana hata rais wa JMT anaapishwa kwa mujibu wa Katiba na kuapa kuilinda, kuitetea na kuitekeleza katiba ya JMT, na jambo lolote linalokwenda kinyume cha Katiba ya JMT, jambo hilo ni batili, ndio maana nikasema Bunge haliwezi kutoa Azimio linalikwenda kinyume cha Katiba ya JMT, azimio hilo ni batili ab-initio, hivyo na ufafanuzi wa Spika pia ni batili.
- Japo rais wetu haamrishwi na yoyote, lakini kuna vipengele vya katiba, rais wa JMT anaamrishwa tena sio amri kavu kavu tuu, bali amri zenye ultimatum, na hiyo ultimatum ikipita, katiba inaelekeza rais apuuzwe, hilo jambo lifanyike.
- Moja ya mambo ambayo katiba inatoa amri kwa rais, ni uwasilishaji wa Ripoti ya CAG Bungeni. Kutokana na umuhimu wa ripoti hiyo, rais wa JMT, anapangiwa cha kufanya, anaamrishwa, anapewa na ultimatum, asipotekeleza, anapuuzwa na kuwa bypassed, ripoti inatua mezani kwa Spika.
- Kwanza tumjue mtu anayeitwa CAG, anazungumzwa katika ibara ya 143.-(1), huyu jamaa ana powers za ajabu. Miongoni mwa powers zake katika kutimiza majukumu yake, baada ya bajeti ya serikali kupitishwa na Bunge, ni mtu huyu ndiye pekee anayeidhinisha fedha kutoka mfuku mkuu wa hazina kutumika, zikiwemo fedha za Ikulu, fedha za Bunge, na vote nyingine zote, akigoma kuidhinisha, fedha haitoki na hapa ndipo ugomvi mkubwa wa CAG na serikali unapoanzia, serikali unajichotea tuu fedha kutoka mfuko mkuu wa hazina na kufanya matumizi ambayo hayajaidhinishwa na Bunge na CAG.
- Baada ya kuidhisha matumizi, CAG anatakiwa kufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha hizo na kutoa hiyo Ripoti ya CAG ambayo sasa ndio mzizi wa fitna hii yote inayoendelea. Kwenye Ripoti ya CAG, CAG anatoa mapendekezo kwa Bunge, kuisimamia serikali, Bunge limekuwa likionyesha udhaifu katika utekelezaji wa mapendekezo ya CAG, CAG kaulizwa swali kajibu ukweli wa mambo na hali halisi, limekuwa kosa!.
- Naomba kukiri bandiko hili, linetokana na hoja ya mwana jf huyu
Inawezekana report ya CAG ya mwaka huu imeibua madudu mengi ambayo serikali haitaki wananchi wayajue hivyo kuanzisha zengwe kupitia spika kwamba bunge halitafanya kazi na CAG. Report isipopelekwa bungeni ni kinyume cha katiba lakini hata ikipelekwa haitajadiliwa na isipojadiliwa maana yake sisi walipa kodi tunanyimwa nafasi ya kujua serikali inatumia vipi kodi zetu.
[*]Timing ya kuwasilishwa report ya CAG kwa Rais na muda wa kutolewa azimio la bunge kutokufanya kazi na CAG inaonyesha ni vitu ambayo serikali na bunge walivipanga. Hivi kuna uwezekano wa report hiyo kuwekwa kitandani tuone ambacho nguvu nyingi zinatumika kisijulikane? Hatujasahau trion 1.5 mjue!!!!Tiba - Mkuu Tiba, Kwanza nakubaliana na wewe, you cant rule out possibility ya serikali kujua Azimio la batili la Bunge, prior, ndio maana Ripoti ya CAG ilipokelewa kimya kimya, kwa Bunge linalomuuliza rais tumteue nani kuongoza kamati teule, then anything is possible.
- Ripoti ya CAG ndio ripoti muhimu kuliko ripoti yoyote ndio maana inaandamana na maamrisho, Kwanza CAG anaamrishwa na Katiba kukabidhi ripoti kwa mujibu wa Ibara ya 143 (4) The Controller and Auditor-General shall submit to the President every report he makes. hilo neno shall ni amri.
- Rais akiisha kabidhiwa, Ripoti ya CAG, kinachofuatia ni rais naye anaamrishwa kwa amri zenye ultimatum, hakuna pengine popote rais wa JMT anapewa Ultimatum ya siku 7, aikabidhi ripoti hiyo Bungeni 143 (4)."Upon receipt of such report the President shall direct the persons concerned to submit that report before the first sitting of the National Assembly which shall be held after the President has received the report and it shall have to be submitted to such sitting before the expiration of seven days from the day the sitting of the National Assembly began"
- Ripoti hiyo inakabidhiwa kwanza kwa rais ili kupata mamlaka ya kiraisi, yaani presidential status, hivyo ripoti hiyo ikiisha kabidhiwa inakuwa ni president report of CAG, inaingia Bungeni as presidential document with presidential powers, ndio maana Bunge halina uwezo wala mamlaka kuikataa na likiikataa linapaswa kuvunjwa.
- Rais akiisha ipokea Ripoti ya CAG, hana mamlaka kubadili chochote kwenye ripoti hiyo,bali ana haki ya kupewa tuu ufafanuzi wowote.Rais anaamrishwa na Katiba kuiwasilisha Bungeni ndani ya siku 7 bila option ya kuchagua kama aiwasilishe ama laa.
- Kufuatia umuhimu wa ripoti hiyo, mfano inaweza kuwa na qualified option kuhusu matumizi ya Ikulu, hivyo rais akaamua asiiwasilishe Bungeni, katiba kwa kulijua hilo, inatoa maelekezo rais apuuzwe kwa kumuelekeza CAG, kuwa siku 7 zikipita bila rais kuiwasilisha Bungeni Ripoti ya CAG, then CAG ampuuze rais na badala yake aichukue ripoti yake na kuiwasilisha yeye Bungeni, 143 (4) If the President does not take steps of submitting such report to the National Assembly, then the Controller and Auditor-General shall submit the report to the Speaker of the National Assembly"
- Amri kuhusu Ripoti ya CAG hazikuishia kwa Rasi tuu wa JMT, bali hadi Spika ameamrishwa kuwa akipokea Ripoti ya CAG ni lazima aiwasilishe Bungeni 143 (4) the Controller and Auditor-General shall submit the report to the Speaker of the National Assembly who shall submit the report to the National Assembly. Spika hakupewa option ya kuchagua kuipokea ripoti hiyo au asipokee, hii amri ya Katiba, kama hata rais asipoipeleka, rais anapuuzwa, who is Spika kuweza kuchagua kuipokea au laa, tena kuchagua usisainiwe na nani ndipo ipokelewe?. Hivyo as far as Ripoti ya CAG is concerned, CAG ni zaidi ya rais katika uwasilishaji wa ripoti hiyo endapo rais wa JMT atapata kigugumizi cha kutoiwasilisha na Spika ameelekezwa lazima aiwasilishe mezani.
- Ripoti hiyo ikiisha wasilishwa rasmi mezani kwa Spika, hapo hapo, inageuka kuwa a public document na kufuatia maendeleo ya technology, ripoti hiyo ikisainiwa inapanda online kwenye mtandao wa NAO, pale Bungeni copies zikawekwa kwenye pigeon holes za Wabunge, sisi waandishi tunapewa copies hard na soft.
Hivyo wajameni, with three days to go, lets rest assured Katiba itafuatwa, na Ripoti ya CAG yenye sahihi ya CAG Prof. Mussa Assad, itawasilishwa mezani kwa Spika kwa mujibu wa katiba.
Nawatakia Jumatatu Njema.
Paskali
KaShivjiKadogo.
Update,
Baada ya Ripoti ya CAG yenye sahihi ya CAG, Prof. Mussa Assad, kuwasilishwa Bungeni kwa mujibu wa Katiba. Uzi huu wa kuhimiza hadhi ya ripoti ya CAG kusingatiwa, umetekelezwa, Ripoti ya CAG, imetendewa haki. Kama Azimio lile la Bunge la kutokufanya kazi na CAG ni azimio halali au batili, limepatikana, ni azimio batili ndio maana limepuuzwa. Ufafanuzi wa Spika kuwa Bunge halitapokea Ripoti ya CAG kama imesainiwa na CAG mwenyewe Prof. Assad, ila itapokelewa kama itasainiwa na mtu mwingine pia ni batili, na imepuuzwa, Ripoti ya CAG iliyowasilishwa Bungeni imesainiwa na CAG, Prof. Assad,
Kiukweli kabisa, kuna mabandiko tunaweka humu JF, yanawasaidia sana watawala wetu, japo huwa hawasemi, ila tunapima kwa matokeo. Hivyo ndugu zangu wana jf, huu mjadala nimeufunga rasmi.
Hongera kwa Bunge letu kufuata Katiba.
P.