Kufuatia Umuhimu wa Ripoti ya CAG, Je, Wajua Rais Wetu Anaamrishwa With Ultimatum?. Ikipita, Rais Anapuuzwa?.

hili bandiko tamu sana brother paschal umetutendea haki sisi tusiojua shelia ata nikisoma katiba huwa sielewi chochote shukuran pia kwa wachangiaji wamejazilizia minofu ya hoja mpaka najiona nimepata elimu kubwa bure. laiti watanzania milioni kumi wangepata elimu hii hakika watawala wangeishi kwa kulazimika kufuata katiba lakini ndio hivyo tumefanywa mazwazwa wakusifu raisi akiteu na kushangilia rais akitengeu tukiwa ntwajiona ufahali kuitwa wanyonge mwisho tunakufia mapokezi kwakukosa huduma bora wakati mkuu wa wanyonge anazurula na gunia la noti akigawa kwa anaemsifia na kumsujudia.
 
Update,
Baada ya Ripoti ya CAG yenye sahihi ya CAG, Prof. Mussa Assad, kuwasilishwa Bungeni kwa mujibu wa Katiba. Uzi huu wa kuhimiza hadhi ya ripoti ya CAG kusingatiwa, umetekelezwa, Ripoti ya CAG, imetendewa haki. Kama Azimio lile la Bunge la kutokufanya kazi na CAG ni azimio halali au batili, limepatikana, ni azimio batili ndio maana limepuuzwa. Ufafanuzi wa Spika kuwa Bunge halitapokea Ripoti ya CAG kama imesainiwa na CAG mwenyewe Prof. Assad, ila itapokelewa kama itasainiwa na mtu mwingine pia ni batili, na imepuuzwa, Ripoti ya CAG iliyowasilishwa Bungeni imesainiwa na CAG, Prof. Assad,

Kiukweli kabisa, kuna mabandiko tunaweka humu JF, yanawasaidia sana watawala wetu, japo huwa hawasemi, ila tunapima kwa matokeo. Hivyo ndugu zangu wana jf, huu mjadala nimeufunga rasmi.
Hongera kwa Bunge letu kufuata Katiba.
P.
 
Back
Top Bottom