Kufuatia Umuhimu wa Ripoti ya CAG, Je, Wajua Rais Wetu Anaamrishwa With Ultimatum?. Ikipita, Rais Anapuuzwa?.

This is a Katibalessness if not lawlessness country, hivyo lolote linaweza kufanywa na wenye madaraka! msijisumbue na maandiko yoyote. Asipofanya mtamfanya nini? Bunge ni la kwake, kuna wa kuepeleka motion ya impeachment? 89% ni CCM, itapita na wote wanamuogopa? Shithole country ni yetu kweli kweli!
Mkuu hapo ni mtego umetegwa ni nani kati ya Rais na Bunge atakaenasa kwenye mtego ule??? Hili sio suala dogo Mkuu, kuna fedha za ndani na za Wahisani pia. Tusipofanya lolote kwa uoga wetu basi tegemea nguvu kutoka upande wa pili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Pascal Mayalla, let's say, Rais amegoma kuiwasilisha ripoti ya CAG Bungeni then CAG akaamua kum-bypass na kuiwasilisha yeye kama Katiba inavyomwagiza lakini Bunge likaamua kutoipokea (maana limeshaazimia kutofanya naye kazi) then what next? Ufafanuzi tafadhali.
Kutopokelewa kwa ripoti ya CAG kikatiba inabidi Raisi alivunje Bunge kwani ripoti ya CAG ni Presidential Report...!

Sent from my Redmi S2 using Tapatalk
 
Kutopokelewa kwa ripoti ya CAG kikatiba inabidi Raisi alivunje Bunge kwani ripoti ya CAG ni Presidential Report...!
... hilo nalijua; swali langu ni kwamba Rais hataki kuiwasilisha ripoti ya CAG Bungeni; kuona hivyo, CAG kaamua kuiwasilisha yeye lakini Bunge halitaki kuipokea (kama lilivyoazimia kutofanya naye kazi) na Rais hataki kulivunja Bunge inakuwaje hapo?
 
Na ndicho kinachofanyika. Pesa ya uwanja wa chato na miradi kama ya ndege etc si ilitoka nyumbani kwake alikohamishia hazina. angalia mlolongo wa wanaosimamia fedha za serikali ni ndugu wake wa damu... hazina iko nyumbani kwake na maisha yanaenda!
Tena watu unaowategemea waseme wanampigia makofi pwa pwa pwa pwa.

Yaani,

- Marais waastafu

- Wasomi

- Bunge ( CCM )

- Mahakama.

- Viongozi wa Dini.

Wote wanaliogopa lenyewe, limekuwa zaidi ya mungu.

Liko tayari kukuhukumu mtu usiye na hatia kwa risasi katili 500 mchana kweupeeee huku likitumia "media" kuji-brand zalendo lililotukuta na wewe unatumika na mabeberu.
 
Niliposoma tu kuwa "...Raisi yupo chini ya katiba..." nikaishia hapo, sikuona sababu ya kuendelea kwa sababu umeshindwa kuelewa pointi kubwa na ambayo ndiyo ya muhimu zaidi. Raisi wa Tz yuko juu ya sheria, sheria ikiwemo katiba, hiyo katiba ndiyo iliyompa ukuu pale iliposema kuwa hatashtakiwa kwa chochote atakachofanya kwenye madaraka yake, akiwa raisi au baada ya uraisi.

Hiyo hapo juu ndio mzizi wa fitina, kwa maana anaweza kufanya lolote ikiwemo kutoifuata, kuivunja na kuisigina kabisa hiyo katiba, hakuna mtu, bunge wala mahakama inaweza kumfanya lolote!

Naomba tu nikusaidie,

Anaposema rais yupo chini ya katiba na sheria anamaanisha ni sheria na katiba ndizo zimemuumba mtu anaitwa Rais! Nje ya hapo asingekuwepo!
 
Niliposoma tu kuwa "...Raisi yupo chini ya katiba..." nikaishia hapo, sikuona sababu ya kuendelea kwa sababu umeshindwa kuelewa pointi kubwa na ambayo ndiyo ya muhimu zaidi. Raisi wa Tz yuko juu ya sheria, sheria ikiwemo katiba, hiyo katiba ndiyo iliyompa ukuu pale iliposema kuwa hatashtakiwa kwa chochote atakachofanya kwenye madaraka yake, akiwa raisi au baada ya uraisi.

Hiyo hapo juu ndio mzizi wa fitina, kwa maana anaweza kufanya lolote ikiwemo kutoifuata, kuivunja na kuisigina kabisa hiyo katiba, hakuna mtu, bunge wala mahakama inaweza kumfanya lolote!
Pamoja na hayo Mkuu lkn Mahakama ya DHAMIRA yake itamshitaki atakapomaliza kipindi chake au hata kabla.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
bado kuna swali tuliitaji ufafanuz what will happen km bunge wakiamua kutoijadili na Kuieka kapuni hyo report

MiM
... Katiba haililazimishi Bunge kuijadili ripoti ya CAG; na Bunge likiamua linaweza kuiweka kapuni bila kuvunja Katiba au sheria yoyote. ILA, narudia tena ILA ikishawasilishwa Bungeni automatically inageuka kuwa Public Document rather than CONFIDENTIAL hivyo kuwa wazi kwa umma, media, n.k. kuijadili na hili ndio la muhimu zaidi. Hapa ndipo panapotia watu wazimu utafikiri wameona kifo!
 
kama yeye anapuuza waliomchagua na kitabu chetu anakipuuza, huyu mtu atufai, nashangaa waliokuwa wanampigia makofi na kushangilia kila asemacho, haya hawayaoni wakamwambia....?

hivi katika ile katiba pendekezwa ya mzee warioba ilijadili mamlaka ya raisi ? sio ile ya wapuuzi chenge....
 
Tena watu unaowategemea waseme wanampigia makofi pwa pwa pwa pwa.

Yaani,

- Marais waastafu

- Wasomi

- Bunge ( CCM )

- Mahakama.

- Viongozi wa Dini.

Wote wanaliogopa lenyewe, limekuwa zaidi ya mungu.

Liko tayari kukuhukumu mtu usiye na hatia kwa risasi katili 500 mchana kweupeeee huku likitumia "media" kuji-brand zalendo lililotukuta na wewe unatumika na mabeberu.


Hao wote wamekuwa walamba viatu vya mkubwa kwa kuhofia madudu waliyokuwa wameyafanya wakiwa na wao viongozi, kulinda uraia wao, kulinda biashara zao

Wanaopaswa kumwambia huyo dureva ni wananchi wenyewe ambao uoga walionao hadi uishe
 
Wanabodi,
With 3 days to go, ultimatum ya kuwasilishwa mezani kwa Spika kwa Ripoti ya CAG itimie, leo naendelea na zile makala zangu za uelimishaji umma kuhusu Katiba ya JMT, kwa mtazamo wa mtunga katiba alidhamiria nini kuweka kifungu fulani.

Makala hizi naziendesha kwa mti wa maswali ili kutoa fursa kwa mabingwa wa katiba kutufafanulia zaidi.

Rais wa JMT ndie mtu mwenye mamlaka makubwa zaidi kuliko mtu mwingine yoyote kwa sababu rais wa JMT ndie mkuu wa serikali, mkuu wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu.

Katiba inaelekeza katika kufikia maamuzi, Rais wa JMT anaweza kushauriwa na yeyote lakini katika kufikia maamuzi, rais anafikia maamuzi yeye mwenyewe bila kulazimika kufuata ushauri wa yoyote
ndio maana rais Magufuli aliwahi kutamka hapangiwi na mtu and he was right.

Hili la rais kutopangiwa na mtu yoyote linamfanya rais wa JMT kuwa ndiye mtu mwenye mamlaka makubwa zaidi na mamlaka kuu kuliko mtu yoyote, ila pia sio zaidi ya Katiba.

Katiba ndio mamlaka kuu kuliko mamlaka nyingine zote, na rais yuko chini ya katiba.

Japo rais wetu haamrishwi na yoyote, lakini kuna vipengele vya katiba, rais wa JMT anaamrishwa tena sio amri kavu kavu tuu, bali amri zenye ultimatum, na hiyo ultimatum ikipita, katiba inaelekeza rais apuuzwe, hilo jambo lifanyike.

Moja ya mambo ambayo katiba inatoa amri kwa rais, ni uwasilishaji wa Ripoti ya CAG Bungeni. Kutokana na umuhimu wa ripoti hiyo, rais wa JMT, anapangiwa cha kufanya, anaamrishwa, anapewa na ultimatum, asipotekeleza, anapuuzwa na kuwa bypassed, ripoti inatua mezani kwa Spika.

Naomba kukiri bandiko hili, linetokana na hoja ya mwana jf huyu




Mkuu Tiba,

Kwanza nakubaliana na wewe possibility ya serikali kujua Azimio la batili la Bunge, prior, ndio maana Ripoti ya CAG ilipokelewa kimya kimya, kwa Bunge linalomuuliza rais tumteue nani kuongoza kamati teule, then anything is possible.
Ripoti ya CAG ndio ripoti muhimu kuliko ripoti yoyote ndio maana inaandamana na maamrisho, Rais akiisha kabidhiwa, Ripoti ya CAG, kinachofuatia ni amri zenye ultimatum, hakuna pengine popote rais wa JMT anapewa Ultimatum ya siku 7, aikabidhi ripoti hiyo Bungeni.
Ripoti hiyo inakabidhiwa kwanza kwa rais ili kupata mamlaka ya kiraisi, yaani presidential status, hivyo ripoti hiyo ikiisha kabidhiwa inakuwa ni president report of CAG, inaingia Bungeni as presidential document with presidential powers, ndio maana Bunge halina uwezo wala mamlaka kuikataa na likiikataa linapaswa kuvunjwa.
Rais akiisha ipokea Ripoti ya CAG, hana mamlaka kubadili chochote kwenye ripoti hiyo,bali ana haki ya kupewa tuu ufafanuzi wowote.
Rais anaamrishwa na Katiba kuiwasilisha Bungeni ndani ya siku 7 bila option ya kuchagua kama aiwasilishe ama laa.
Kufuatia umuhimu wa ripoti hiyo, mfano inaweza kuwa na qualified option kuhusu matumizi ya Ikulu, hivyo rais akaamua asiiwasilishe Bungeni, katiba kwa kulijua hilo,inampuuza rais kwa kumuelekeza CAG, kuwa siku 7 zikipita bila Ripoti ya CAG kuwasilishwa Bungeni, siku ya 7, CAG ampuuze rais na kuiwasilisha yeye Bungeni, hivyo as far as Ripoti ya CAG is concerned, CAG ni zaidi ya rais katika uwasilishaji wa ripoti hiyo endapo rais wa JMT atapata kigugumizi cha kutoiwasilisha.
Bunge nalo katika kuopokea Ripoti ya CAG, nalo pia limefungwa mikono, lazima liipokee kwa sababu ni presidential report halina option ya kuamua ama lipokee ama ligomee,
Ripoti hiyo ikiisha wasilishwa rasmi mezani kwa Spika, hapo hapo, inageuka kuwa a public document na kufuatia maendeleo ya technology, ripoti hiyo ikisainiwa inapanda online kwenye mtandao wa NAO, pale Bungeni copies zikawekwa kwenye pigeon holes za Wabunge, sisi waandishi tunapewa copies hard na soft.
Hivyo lile Azimio la Bunge kutofanya kazi na CAG ni batili kwa sababu huwezi kumtenganisha CAG na office ya CAG. Hata ufafanuzi wa Spika pia ni batili, Ripoti ya CAG haiwezi kusainiwa na mtu mwingine isipokuwa CAG kama presidential decree, warrant or acent haiwezi kusainiwa na mtu mwingine yoyote isipokuwa rais, na noti za fedha haiwezi kusainiwa na mtu mwingine isipokuwa Gavana.
Hivyo rest assured Ripoti ya CAG itawasilishwa kwa mujibu wa katiba.

Leo ni three days to go.

Paskali
KaShivjiKadogo.
Hahahhhaa mayala siku tatu sio nyingi lakini,kwa jinsi viongozi wetu wasivyotii katiba na sheria inatia wasiwasi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Paskali unatengeneza hofu isiyokuwepo, hakuna aliyesema ripoti haiendi bungeni. Unanikumbusha jinsi makamanda walivyongojea ''maandamano hewa'' ya damange.
Mkuu Kaka Wakudadavua, mimi sijengi hofu yoyote bali nafafanua kile mtunga katiba alichodhamiria, wakati Bunge lilipopitisha Azimio batili kuwa halitafanya kazi na CAG Prof. Assad, na Spika kufafanua kuwa Prof. Assad tuu as person lakini sio ofisi yake, na kutaka ripoti hiyo isainiwe na mtu mwingine ndipo ipokelewe, naamini kabisa Bunge letu na wabunge wetu, hawakujua Ripoti ya CAG ina hadhi gani, huwezi kumtenganisha CAG na Prof. Assad, Ripoti ya CAG bila saini ya CAG sio ripoti ya CAG.

Amini usiamini, mabandiko kama haya yanasaidia sana taifa letu, Bunge letu na serikali yetu, maana kuna vitu tunavisema humu, hata wenyewe walikuwa hawavijui, mfano mzuri ni angalia tarehe ya bandiko hili,
https://www.jamiiforums.com/threads...ccm-2015-could-be-john-pombe-magufuli.707165/
wakati huo hata Magufuli mwenyewe alikuwa hajui lakini watu humu tulijua.

Hivyo usikute hata Bunge wakati linatoa azimio hilo batili, hawakujua kuwa Bunge kufanyakazi na CAG sio a matter of choice ni utekelezaji wa amri za katiba. Spika aliposema hawapokei Ripoti ya CAG kama ina saini ya CAG Prof. Assad, ila ikisainiwa na mtu mwingine itapokelewa, hakujua kuwa Ripoti ya CAG bila saini ya CAG sio Ripoti ya CAG, na aliposema hawaipokea, alidhani Bunge lina optiion ya kuchagua kuipokea au kuikataa Ripoti ya CAG, katiba imeamrisha ripoti hiyo ipokelewe bila options, kama rais tuu anapuuzwa, ripoti inakuja Bungeni, who is Speaker asiipokee?.
Najua hofu kubwa kwa wengi ni kutojua kuwa Bunge likiikataa Ripoti ya CAG yenye sahihi ya CAG Prof. Assad, Katiba inamuelekeza rais kulivunja Bunge kwa mujibu wa Ibara ya 90 (c).

Nakuomba sana Kaka yangu Wakudadavua, hapa ninafafanua tuu matakwa ya kikatiba, hivyo usiwe na hofu, hata Bunge likivunjwa, likiundwa tena, viti maalum vitaendelea kuwepo, hivyo wale wabunge wa viti maalum, waliohudumu vizuri kwenye nafasi zao za viti maalum na kutoa huduma maalum za viti hivyo maalum, watateuliwa tena kuendelea kuhudumu vitu maalum na kutoa huduma maalum za viti maalum kwa Bunge letu na Watanzania kwa ujumla.

P.
 
Wanabodi,

With 3 days to go, itimie ile ultimatum ya kuwasilishwa mezani kwa Spika kwa Ripoti ya CAG, leo naendelea na zile makala zangu za uelimishaji umma kuhusu Katiba ya JMT, kwa mtazamo wa mtunga katiba alidhamiria nini kuweka kifungu fulani.

Makala hizi naziendesha kwa mtindo wa maswali ili kutoa fursa kwa mabingwa wa katiba kutufafanulia zaidi, swali la leo ni
"Kufuatia Umuhimu wa Ripoti ya CAG, Jee Wajua Kuwa Rais Wetu Anaamrishwa na Katiba Kuipokea Ripoti Hiyo?, Na Sio Amri Kavu Kavu tuu, bali ni Amri With Ultimatum?. Jee Wajua Hiyo Ulmatum Ikipita, Katiba Inaelekeza Rais Apuuzwe, Ripoti Hiyo Iwasilishwe na CAG mwenyewe?.

  1. Rais wa JMT ndie mtu mwenye mamlaka makubwa zaidi kuliko mtu mwingine yoyote ndani ya JMT kwa sababu rais wa JMT ndie Mkuu wa Mkuu wa nchi, Head of State, Mkuu wa Serikali, Head of Government, na Amiri Jeshi Mkuu, hivyo kila kitu kinachofanywa na kiongozi yoyote wa serikali, idara au wakala, kinafanywa kwa niaba ya rais wa JMT, hata CAG anafanya ukaguzi kwa niaba ya rais wa JMT, hata Ripoti ya CAG ni Ripoti ya rais wa JMT, hivyo rais JMT ndio kila kitu.
  2. Ibara ya 37 ya Katiba inaelekeza katika jambo fulani, Rais wa JMT anaweza kushauriwa na yeyote lakini katika kufikia maamuzi, rais anafikia maamuzi yeye mwenyewe kama rais, bila kulazimika kufuata ushauri wa yoyote "in the performance of his duties and functions, the President shall be free and shall not be obliged to take advice given to him by any person, save where he is required by this Constitution or any other law to act in accordance with the advice given to him by any person or authority.
    Act "
    hivyo rais Magufuli alipotamka kuwa hapangiwi, he was right rais wa JMT hapangiwi kitu na mtu.
  3. Ila hili la rais kutopangiwa kitu na mtu yoyote linamfanya rais wa JMT kuwa ndiye mtu mwenye mamlaka kuu kuliko mtu yoyote mtu yoyote ndani ya JMT ila pia mamlaka hizo sio juu ya Katiba bali ni ndani ya katiba. Hivyo tunapozungumzia ukuu wa Katiba, Katiba ya JMT ndio mamlaka kuu kuliko mamlaka nyingine zote, na rais yuko chini ya Katiba, ndia maana hata rais wa JMT anaapishwa kwa mujibu wa Katiba na kuapa kuilinda, kuitetea na kuitekeleza katiba ya JMT, na jambo lolote linalokwenda kinyume cha Katiba ya JMT, jambo hilo ni batili, ndio maana nikasema Bunge haliwezi kutoa Azimio linalikwenda kinyume cha Katiba ya JMT, azimio hilo ni batili ab-initio, hivyo na ufafanuzi wa Spika pia ni batili.
  4. Japo rais wetu haamrishwi na yoyote, lakini kuna vipengele vya katiba, rais wa JMT anaamrishwa tena sio amri kavu kavu tuu, bali amri zenye ultimatum, na hiyo ultimatum ikipita, katiba inaelekeza rais apuuzwe, hilo jambo lifanyike.
  5. Moja ya mambo ambayo katiba inatoa amri kwa rais, ni uwasilishaji wa Ripoti ya CAG Bungeni. Kutokana na umuhimu wa ripoti hiyo, rais wa JMT, anapangiwa cha kufanya, anaamrishwa, anapewa na ultimatum, asipotekeleza, anapuuzwa na kuwa bypassed, ripoti inatua mezani kwa Spika.
  6. Kwanza tumjue mtu anayeitwa CAG, anazungumzwa katika ibara ya 143.-(1), huyu jamaa ana powers za ajabu. Miongoni mwa powers zake katika kutimiza majukumu yake, baada ya bajeti ya serikali kupitishwa na Bunge, ni mtu huyu ndiye pekee anayeidhinisha fedha kutoka mfuku mkuu wa hazina kutumika, zikiwemo fedha za Ikulu, fedha za Bunge, na vote nyingine zote, akigoma kuidhinisha, fedha haitoki na hapa ndipo ugomvi mkubwa wa CAG na serikali unapoanzia, serikali unajichotea tuu fedha kutoka mfuko mkuu wa hazina na kufanya matumizi ambayo hayajaidhinishwa na Bunge na CAG.
  7. Baada ya kuidhisha matumizi, CAG anatakiwa kufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha hizo na kutoa hiyo Ripoti ya CAG ambayo sasa ndio mzizi wa fitna hii yote inayoendelea. Kwenye Ripoti ya CAG, CAG anatoa mapendekezo kwa Bunge, kuisimamia serikali, Bunge limekuwa likionyesha udhaifu katika utekelezaji wa mapendekezo ya CAG, CAG kaulizwa swali kajibu ukweli wa mambo na hali halisi, limekuwa kosa!.
  8. Naomba kukiri bandiko hili, linetokana na hoja ya mwana jf huyu
  9. Mkuu Tiba, Kwanza nakubaliana na wewe, you cant rule out possibility ya serikali kujua Azimio la batili la Bunge, prior, ndio maana Ripoti ya CAG ilipokelewa kimya kimya, kwa Bunge linalomuuliza rais tumteue nani kuongoza kamati teule, then anything is possible.
  10. Ripoti ya CAG ndio ripoti muhimu kuliko ripoti yoyote ndio maana inaandamana na maamrisho, Kwanza CAG anaamrishwa na Katiba kukabidhi ripoti kwa mujibu wa Ibara ya 143 (4) The Controller and Auditor-General shall submit to the President every report he makes. hilo neno shall ni amri.
  11. Rais akiisha kabidhiwa, Ripoti ya CAG, kinachofuatia ni rais naye anaamrishwa kwa amri zenye ultimatum, hakuna pengine popote rais wa JMT anapewa Ultimatum ya siku 7, aikabidhi ripoti hiyo Bungeni 143 (4)."Upon receipt of such report the President shall direct the persons concerned to submit that report before the first sitting of the National Assembly which shall be held after the President has received the report and it shall have to be submitted to such sitting before the expiration of seven days from the day the sitting of the National Assembly began"
  12. Ripoti hiyo inakabidhiwa kwanza kwa rais ili kupata mamlaka ya kiraisi, yaani presidential status, hivyo ripoti hiyo ikiisha kabidhiwa inakuwa ni president report of CAG, inaingia Bungeni as presidential document with presidential powers, ndio maana Bunge halina uwezo wala mamlaka kuikataa na likiikataa linapaswa kuvunjwa.
  13. Rais akiisha ipokea Ripoti ya CAG, hana mamlaka kubadili chochote kwenye ripoti hiyo,bali ana haki ya kupewa tuu ufafanuzi wowote.Rais anaamrishwa na Katiba kuiwasilisha Bungeni ndani ya siku 7 bila option ya kuchagua kama aiwasilishe ama laa.
  14. Kufuatia umuhimu wa ripoti hiyo, mfano inaweza kuwa na qualified option kuhusu matumizi ya Ikulu, hivyo rais akaamua asiiwasilishe Bungeni, katiba kwa kulijua hilo, inatoa maelekezo rais apuuzwe kwa kumuelekeza CAG, kuwa siku 7 zikipita bila rais kuiwasilisha Bungeni Ripoti ya CAG, then CAG ampuuze rais na badala yake aichukue ripoti yake na kuiwasilisha yeye Bungeni, 143 (4) If the President does not take steps of submitting such report to the National Assembly, then the Controller and Auditor-General shall submit the report to the Speaker of the National Assembly"
  15. Amri kuhusu Ripoti ya CAG hazikuishia kwa Rasi tuu wa JMT, bali hadi Spika ameamrishwa kuwa akipokea Ripoti ya CAG ni lazima aiwasilishe Bungeni 143 (4) the Controller and Auditor-General shall submit the report to the Speaker of the National Assembly who shall submit the report to the National Assembly. Spika hakupewa option ya kuchagua kuipokea ripoti hiyo au asipokee, hii amri ya Katiba, kama hata rais asipoipeleka, rais anapuuzwa, who is Spika kuweza kuchagua kuipokea au laa, tena kuchagua usisainiwe na nani ndipo ipokelewe?. Hivyo as far as Ripoti ya CAG is concerned, CAG ni zaidi ya rais katika uwasilishaji wa ripoti hiyo endapo rais wa JMT atapata kigugumizi cha kutoiwasilisha na Spika ameelekezwa lazima aiwasilishe mezani.
  16. Ripoti hiyo ikiisha wasilishwa rasmi mezani kwa Spika, hapo hapo, inageuka kuwa a public document na kufuatia maendeleo ya technology, ripoti hiyo ikisainiwa inapanda online kwenye mtandao wa NAO, pale Bungeni copies zikawekwa kwenye pigeon holes za Wabunge, sisi waandishi tunapewa copies hard na soft.
Hivyo lile Azimio la Bunge kutofanya kazi na CAG ni batili kwa sababu huwezi kumtenganisha CAG na office ya CAG. Hata ufafanuzi wa Spika pia ni batili, Ripoti ya CAG haiwezi kusainiwa na mtu mwingine isipokuwa CAG kama presidential decree, warrant or accent haiwezi kusainiwa na mtu mwingine yoyote isipokuwa rais, na noti za fedha haiwezi kusainiwa na mtu mwingine isipokuwa Gavana.

Hivyo wajameni, with three days to go, lets rest assured Katiba itafuatwa, na Ripoti ya CAG yenye sahihi ya CAG Prof. Mussa Assad, itawasilishwa mezani kwa Spika kwa mujibu wa katiba.
Nawatakia Jumatatu Njema.

Paskali
KaShivjiKadogo.
Hayo Ndiyo madhara ya kuongoza Taasisi kwa mihemko na matamko swali fikirishi nani anajua mrejesho wa kuhojiwa kwa CAG na Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge
 
Niliposoma tu kuwa "...Raisi yupo chini ya katiba..." nikaishia hapo, sikuona sababu ya kuendelea kwa sababu umeshindwa kuelewa pointi kubwa na ambayo ndiyo ya muhimu zaidi. Raisi wa Tz yuko juu ya sheria, sheria ikiwemo katiba, hiyo katiba ndiyo iliyompa ukuu pale iliposema kuwa hatashtakiwa kwa chochote atakachofanya kwenye madaraka yake, akiwa raisi au baada ya uraisi.

Hiyo hapo juu ndio mzizi wa fitina, kwa maana anaweza kufanya lolote ikiwemo kutoifuata, kuivunja na kuisigina kabisa hiyo katiba, hakuna mtu, bunge wala mahakama inaweza kumfanya lolote!
Simply tu mkuu,soma tena,haujamwelewa bro paschal.

Sent using Brain
 
Back
Top Bottom