Rooney
JF-Expert Member
- Jan 16, 2015
- 3,782
- 3,910
Ah ah ah brother ,you are a GENIUS.Mkuu Kaka Wakudadavua, mimi sijengi hofu yoyote bali nafafanua kile mtunga katiba alichodhamiria, wakati Bunge lilipopitisha Azimio batili kuwa halitafanya kazi na CAG Prof. Assad, na Spika kufafanua kuwa Prof. Assad tuu as person lakini sio ofisi yake, na kutaka ripoti hiyo isainiwe na mtu mwingine ndipo ipokelewe, naamini kabisa Bunge letu na wabunge wetu, hawakujua Ripoti ya CAG ina hadhi gani, huwezi kumtenganisha CAG na Prof. Assad, Ripoti ya CAG bila saini ya CAG sio ripoti ya CAG.
Amini usiamini, mabandiko kama haya yanasaidia sana taifa letu, Bunge letu na serikali yetu, maana kuna vitu tunavisema humu, hata wenyewe walikuwa hawavijui, mfano mzuri ni angalia tarehe ya bandiko hili,
https://www.jamiiforums.com/threads...ccm-2015-could-be-john-pombe-magufuli.707165/
wakati huo hata Magufuli mwenyewe alikuwa hajui lakini watu humu tulijua.
Hivyo usikute hata Bunge wakati linatoa azimio hilo batili, hawakujua kuwa Bunge kufanyakazi na CAG sio a matter of choice ni utekelezaji wa amri za katiba. Spika aliposema hawapokei Ripoti ya CAG kama ina saini ya CAG Prof. Assad, ila ikisainiwa na mtu mwingine itapokelewa, hakujua kuwa Ripoti ya CAG bila saini ya CAG sio Ripoti ya CAG, na aliposema hawaipokea, alidhani Bunge lina optiion ya kuchagua kuipokea au kuikataa Ripoti ya CAG, katiba imeamrisha ripoti hiyo ipokelewe bila options, kama rais tuu anapuuzwa, ripoti inakuja Bungeni, who is Speaker asiipokee?.
Najua hofu kubwa kwa wengi ni kutojua kuwa Bunge likiikataa Ripoti ya CAG yenye sahihi ya CAG Prof. Assad, Katiba inamuelekeza rais kulivunja Bunge kwa mujibu wa Ibara ya 90 (c).
Nakuomba sana Kaka yangu Wakudadavua, hapa ninafafanua tuu matakwa ya kikatiba, hivyo usiwe na hofu, hata Bunge likivunjwa, likiundwa tena, viti maalum vitaendelea kuwepo, hivyo wale wabunge wa viti maalum, waliohudumu vizuri kwenye nafasi zao za viti maalum na kutoa huduma maalum za viti hivyo maalum, watateuliwa tena kuendelea kuhudumu vitu maalum na kutoa huduma maalum za viti maalum kwa Bunge letu na Watanzania kwa ujumla.
P.
Thank you kwa ufafanuzi mzuri.
Countdown is on.
Sent using Brain