Kufuatia kifo cha Rais Magufuli, Bendera ya UN itapepea Nusu Mlingoti siku ya Mazishi

Hata kama ni utaratibu wa kawaida nafikiri ingepasa bendera hiyo isipepee kabisa nusu mlingoti maana Nchi mwanachama Rais wake miaka 6 hakuhudhuria hata Mkutano mmoja wa UN eti kwa ya kutojua Kingereza, Kisukuma nacho je?

Rais mpya anajua faida ya kuwa na Makamu anayejua lugha za Kimataifa maana yeye akiwa Makamu alimuwakilisha Rais mara kadhaa kwa hiyo asikubali CCM wamletee Rais ajaye mbumbumbu aaibishe Nchi yetu. Miaka 6 imeaibishwa vya kutosha!
Mkuu unajidhalilisha sana either haujui au unafanya makusudi. Nani kakwambia Magufuli hajui English. Mbona unakuwa mtumwa? Siku ya SADC ulimsomea wewe hotuba? Akina Gadafi walikuwa hawatamki hata neno moja la English na bado walihutubia. Magufuli hakuona umuhimu sana kwake, aliona ilitosha kutuma mwakilishi. Nakumbuka Hayati Mugabe alisema mengi sana kuhusu Mikutano ya UN, kwamba wao kama viongozi wanaenda wanatumia hela nyingi sana lakini wanatoa Hollow speaches ambazo hazisikilizwi na akatamani kuitisha Mgomo wa Nchi za Africa zisishiriki. Nakumbuka Tanzania tulisifiwa kwa kutumia hela kidogo kwenye mikutano ya UN. Tukumbuke kama Nchi bado safari ni ndefu, kujibana na kutumia kodi tunazokusanya vizuri ni muhimu sana. Matumizi bora ya pesa za kodi tunazokusanya yasiwe na mipaka ya Chama. Mambo yakienda sivyo vyama vyote vipaze sauti kupambana na hilo. Lazima tuwe na nchi yenye nidhamu. Katiba Mpya ni Muhimu. Tufumue iliyopitishwa na Bunge kipindi cha warioba, tutengeneze iliyo bora. Mambo yaende. Uzalendo kwa nchi yetu kwanza mengine baadaye.
 
Back
Top Bottom