Kufilisika kisiasa kwingine kunatisha!

Kufilisika kisiasa kwingine kunatisha!

Kumbe we jamaaa hamnazo? Story yako haieleweki. Naanza kushangaa unavyoongoza kama hata kunukuu huwezi.

Ile elimu ya kufupisha insha inabidi uisome upya.
 
mwenye makosa ni huyo aliyempa kinana cheo kwenye chama
hivi kweli kuona huona hata kupapasa pia, au lao ni moja.
 
Hebu litizame hapo lilivyosimama kwenye hiyo picha,kijana mdgo tumbo kubwa shauri ya pesa zetu za kodi na mgao wa pesa zetu za pembe za ndovu,likizeeka litakuwaje??
Aibu kubwa sana hii...
 
Mheshimiwa sana Nape, Katibu mwenezi wetu.

Kwa kuwa kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake, Kwa heshima na taadhima naomba utoe kauli hapa:

  1. Kwanini kila mara Unaliita jina la Dr. Slaa kwa ku-prefix "Babu"? (kwa sababu imekuwa ni kawaida yako na huwezi kukana hili) Ni babu kivipi?
  2. Unatoa maoni gani kwa wale wote ambao pia wameamua ku-prefix jina la Dr.Slaa kwa kama "Padre" Yaani kila wakitaka kutaja jina hili husema "Padre Slaa"> Hii ilianza rasmi wakati alipogombea urais wa JMT 2010. Je unavyoona wewe kauli hii ya kumwita "Padre" wakati yeye mwenyewe hakutaka aitwe hivyo (rejea majina rasmi aliyotumia wakati wa kujiandikisha kama mgombea na mpigakura) ililenga nini? (reflect your answers on the context of what is going on now in our lovely country)
  3. Kwa usawa huohuo basi, ni sahihi pia (hata wewe unaweza) kumwita mtu mwingine kama Dr. Jakaya Mrisho kikwete, Hon Peter Pinda au Wassira kwa Prefixes kama hizo hata kama wenyewe hawajiiti hivyo? Hint: Wassira alizaliwa 1945, anamzidi Slaa kwa miaka mitatu, Slaa anamzidi J.K miaka miwili tu, (ages:Wassira 68, Dr. Slaa ana 65 and JK ana 62) Hon. Pinda alizaliwa August 12, 1948, Dr. Slaa alizaliwa October 29, 1948. (source: Bunge website and other sources) Hivyo Wassira na pinda wamemzidi siku za umri Slaa. Kama kumwita mtu babu ni heshima, na Umri wa miaka >65 ndio base year yako kuita mtu kwa heshima ya "Babu", Je unataka tuelewe kuwa huna heshima kwa Wassira na Pinda kama unavyomheshimu Dr. Slaa?

Majibu tafadhali...

Watadakia wengine (LUMUMBA BK7) kumtolea majibu kwa mtindo wa kebehi na matusi lakini kamwe Nape hatajaribu kutoa majibu kwa hayo uliyomuuliza
 
Nape huoni kuwa wewe ndie unathibitisha kufilisika kisiasa. Hata kama mtu ana kasoro katika ubongo wake hawezi kushindwa kuona ukweli kuwa kama walialikwa watu wawili wenye vyeo vinavyoshabihiana katika vyama vyao mmoja akaitikia mwaliko akafika kwenye tukio na mwingine hakufika, huyo ambae hakufika kauogopa mwaliko. Unaamini kuwa watu wote wana mtazamo kama wa kwako. Panua upeo wa kutazama na ku-address issues for you to grow politically otherwise you will end up being mpiga kelele zisizo na mantiki
 
Ukitaka kujua kuwa Nape uwezo wake wa kufikiri ni mdogo linganisha alichoandika kwenye verified ID na kwenye fake ID hii. Kule amesema TandaleOne alikuwa anafanya propaganda lakini hapa aliyeshutumiwa kufanya propaganda eti na yeye anacomment kwa kuiponda CHADEMA utadhani ndo wameanzisha uzi huu.
 
Kwa mazoea yako ya kumwita BABU DR Slaa ndio maana alisepa, naamini alifikiri ungeenda zaidi ya hapo. Bora Kinana huwa anaongea kwa staha na kwa heshima.

na ndo maana babu alisepa, huwezi kufanya mdahalo na mjukuu wako hata siku moja unless ukae nae umpigie hadithi za sungura mjanja, halafu cheki asivyo na aibu leo kamkana mtu aliyemtuma jana alete propaganda hapa, ha ha ha haaaaaah, kweli kila boya ana boya wake
 
Jamani mbona habari inajieleza. Udaku wa tz daima uko wapi? Ni kweli kinana hakufika na mazingira yanaonesha alikwepa kufika na sababu alizotoa nape ni utetezi tu.
 
Khaa!! Huyu Nape ndiyo anamuita Dr Slaa Babu kwenye media bila hata aibu. Dogo siasa zisitufanye tukose adabu. Kwa jinsi ulivyotyumia neno la Babu kwenye thread yako ni kama tusi binafsi kwa Dr Slaa. Wewe na Dr Slaa wote ni wanasiasa. Siasa ndiyo zinawafanya jamii zenu ziishi. Leo ukihamia CDM an Dr akihamia CCM mtatizamanaje?? Pinganeni kwa mawazo na sera lakini si kwa muonekano binafsi. Tumia akili wewe :mvutaji:
 
Kama JK alimkimbia Dr Slaa katika mdahalo mwaka 2010 sasa Kinana atamweza?
 
Hata mimi jana niliandika baada ya kuona hizi propaganda za huyo mtu wa propaganda wa CCM.

Sijui ni kwa nini Katibu mkuu wa CCM na Mwenyekiti wake Jakaya kikwete wanaogopa mdahalo na Dr.Slaa kiasi hiki.Leo Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana amemkimbia Dr.Slaa kama alivyofanya Mwenyekiti wa CCM ndugu Jakaya Kikwete wakati akiwa mgombea Urais Mwaka 2010 alipokimbia mdahalo kwa kumhofia Dr.Slaa.Taarifa za awali ni kwamba Kinana amehofia kuumbuliwa zaidi hadharani na Dr.Slaa kuhusu tuhuma zinazomkabili kuhusiana na nyara za Taifa ambazo ameshindwa kuzitolea majibu.Leo ITV waliwaalika makatibu wakuu wa vyama vya siasa kujadili hali ya kisiasa nchini.Dokta Slaa alikubali na kuitikia wito ila alipofika kwenye ofisi za ITV Kinana hakutokea na baadae akatokea Nape Nnauye-mpiga gitaa na mnenguaji kwenye mikutano yao ya hadhara (literally mistaken kama kATIBU WA ITIKADI NA UENEZI)bila kuzingatia itifaki.Dr.Slaa akataka itifaki izingatiwe akaamua kuondoka.Walialikwa makatibu wakuu na itifaki ilistahili kuwa hivyo

Wananchi wanajiuliza sasa ni chama gani hiki ambacho mwenyekiti na katibu mkuu wanaogopa mijadala kiasi hiki?.Rais kikwete (kwa kuhofia uwezo wake mdogo kama inavyojulikana sana)alikimbia mdahalo mwaka 2010 kwa kumuogopa Dr.Slaa,leo imekua zamu ya katibu mkuu Kinana.

Tujifunze kuzoea mijadala/midahalo(debate).This is the age in which you must be yourself na uwe tayari kwa public condemnation or appraisal and not otherwise.

Th

KINANA NA JK NI WEUPE SANA KWA Dr. SLAA HAWAMWEZI.
 
Hamocha😛amoja na sintofahamu ya historia yako,bado mm naamini wewe ni "mnyampaa".Viti yule mla fisi(mnyiramba,mtani) yupo au kapeleka ushahidi mbinguni? msalimie
Yuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu! Ngwi munyampaaaaaaaaa yule, sikujua bwana. Nilidhani niko peke yangu Nkhomango,
 
Toka jana nimekuwa nikisoma kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu hoja ya " NAPE, KINANA NA DR. SLAA" juu ya kipindi kilichodaiwa kuandaliwa na ITV. Leo kwa uzito mkubwa stori hiyo imebebwa na gazeti la CHADEMA la Tanzania Daima. Kwa gazeti hili ni stori inayouza gazeti lao leo.

Niseme toka jana niliposoma propaganda ya Tandaleone nilishangaa lakini nikajipa muda kujua msingi wa propaganda ile. Baada ya muda nikaona majibu ya Babu Dr. Slaa nikayashangaa pia japo si sana, bado niajipa muda. Jioni nikapigiwa simu na mwandishi wa TanzaniaDaima kuulizwa juu ya hiyo stori, nikasema wameanza sasa kuja hadharani na makusudi yao naanza kuyafahamu.

Pamoja na kujitahidi kueleza kilichotokea bado matokeo ni Lead Stori ya Tanzania Daima leo inayodai eti Kinana kamkimbia kiaina Babu Dr.Slaa!!!! Raafiki yangu mmoja asub alipoona gazeti la CHADEMA limeandika vile akanitania akasema nilitegemea UHURU waandike "KINANA AMPUUZA BABU DR. SLAA" nikamwambia UHURU linafanya kazi ya nchi si ya Chama pekeake ndo maana limekuwepo hata kabla ya CCM kuwepo!!

Lakini ninachotaka kusema hapa ni propaganda kama za Gazeti la CHADEMA leo ni dalili za kufilisika sana kisiasa kiasi kwamba hhata jambo dogo sana linageuzwa kuwa jambo kubwa na linalodhaniwa linaweza kutumika kipropaganda.

WASWAHILI WALISEMA kwa sisimizi hata kifuu cha nazi kwake ni sawa na bahari!Pengine tungemsaidia sana mwajiri kwa kumfanyia utafiti kwanini ofisi za wilayani na mikoani za taasisi anayoiongoza zinafungwa kwa kasi ya ajabu.

================================
Habari kamili toka Tanzania Daima
================================

Una marafiki mataaira, sasa alizani gazeti la uhuru liandike, 'kinana ampuuza Dr. Slaa', au aipuuza ITV.Kwasababu alieandaa mahojiano si Dr. Slaa bali ni ITV.
 
hivi kuna mtu anasomaga Tanzania Daima kweli??

kama hayasomwi yanayozalishwa kila siku unayapeleka wapi.Watu wanapiga mahela kwa kuuza zaidi ya copy 2,000,000 daily wewe unauliza kama baharini kuna maji?...UTACHEKWA.

HIZI AKILI NYINGINE BWANA..Subiri upandishwe mtini kwa sababu dalili zote za kuwa kobe unazo!!!!
 
Toka jana nimekuwa nikisoma kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu hoja ya " NAPE, KINANA NA DR. SLAA" juu ya kipindi kilichodaiwa kuandaliwa na ITV. Leo kwa uzito mkubwa stori hiyo imebebwa na gazeti la CHADEMA la Tanzania Daima. Kwa gazeti hili ni stori inayouza gazeti lao leo.

Niseme toka jana niliposoma propaganda ya Tandaleone nilishangaa lakini nikajipa muda kujua msingi wa propaganda ile. Baada ya muda nikaona majibu ya Babu Dr. Slaa nikayashangaa pia japo si sana, bado niajipa muda. Jioni nikapigiwa simu na mwandishi wa TanzaniaDaima kuulizwa juu ya hiyo stori, nikasema wameanza sasa kuja hadharani na makusudi yao naanza kuyafahamu.

Pamoja na kujitahidi kueleza kilichotokea bado matokeo ni Lead Stori ya Tanzania Daima leo inayodai eti Kinana kamkimbia kiaina Babu Dr.Slaa!!!! Raafiki yangu mmoja asub alipoona gazeti la CHADEMA limeandika vile akanitania akasema nilitegemea UHURU waandike "KINANA AMPUUZA BABU DR. SLAA" nikamwambia UHURU linafanya kazi ya nchi si ya Chama pekeake ndo maana limekuwepo hata kabla ya CCM kuwepo!!

Lakini ninachotaka kusema hapa ni propaganda kama za Gazeti la CHADEMA leo ni dalili za kufilisika sana kisiasa kiasi kwamba hhata jambo dogo sana linageuzwa kuwa jambo kubwa na linalodhaniwa linaweza kutumika kipropaganda.

WASWAHILI WALISEMA kwa sisimizi hata kifuu cha nazi kwake ni sawa na bahari!Pengine tungemsaidia sana mwajiri kwa kumfanyia utafiti kwanini ofisi za wilayani na mikoani za taasisi anayoiongoza zinafungwa kwa kasi ya ajabu.

================================
Habari kamili toka Tanzania Daima
================================

wewe siyo size ya Dr. Slaa. hauna ubavu huo.
 
Back
Top Bottom