Kuepusha stress za ndoa, do not marry a first born... Responsibility kibao!

Wabongo bhana,ukiongea reality una dharau! Ukikosa unasemwa,acheni hizo bhana,mnataka watu waish maisha y kupretend ili muone mko level moja au? Aaaarggggh mnabore
Mshukuru MUNGU kwa Haya na Usilete Ngebe wala Dharau Kwa Sisi Waafrika..

Umeniudhi Sana kwa Jinsi Unavyowatukuza Wazungu...WEWE NI MTUMWA..Mtu Usiyeweza Kuthamini vya kwenu..

Kwani Wazazi wako Kuwa na Masters ndo kitu gani?? Kwani Unaona Masters ni kitu cha Ajabu sana au??? Unachekesha Sana...Masters Hainitishi dada,Mi naona ni kitu cha kawaida tu...Naithamini Elimu na Ninaithamini pia hiyo Masters ila sio kuleta majivuno eti kwa sababu ya Masters!!!

Kuna Wenye wazazi waliosoma Kuliko wa Kwako na hawana Dharau Hizo!!! Ni Ulimbukeni tu Ulionao..Natalia Umeniudhi kwa Nyodo zako sio Siri..
BADILIKA,WAZUNGU NI WATU TU KAMA WEWE USIWATUKUZE HIVYO
 
Nina rafiki yangu hajakaa hata mwezi Kwenye ndoa mama mkwe kahamia na wajukuu wa Tatu .rafiki
Yangu kanipigia simu analia kwa uchungu baada ya kumuuliza mume wake kwa nini wanahamia akasema yeye ni first born .Wewe ungefanyaje ?
Ni jambo zuri kufanya due diligence kabla hujaoa au kuolewa! Hii itasaidia kupunguza stress za kuoa ama kuolewa na first born ambaye ni tegemeo kwao 'solo guitar'. Ni mtazamo tu
 
Kweli dunia hadaa,ukistaajabu ya mzee wa mabebs utayaona ya natalia,siku zinazidi kusonga naye ni mama wa watoto, watz lazima wakukome mwaka huu wallah.
 
inategemea na familia sio lazima awe first born hata last born wanaangalia uwezo wake, wengine hata awe na matatizo gani mkwe hawezi kuja kukaa kwako inategemea na mila na desturi
 
Inategemea. Kuna mwingne ameolewa mume wake wa mwisho. Cku ya kwanza wanaenda kutambulishana ma mkwe anamwambia bi dada ''nenden na mtoto mkamtafutie shule englsh midium asome!'' Huyo mtoto baba yk yupo hai na ni mfanyakaz ictoshe ma mkwe mwalim na mtoto anasoma hapo anapofundsha. Bidada na mwenzie ndo kwanza wako chuo kikuu wanasoma. Walivyooana ndo utacheka upasuke. Bidada anaambiwa ''inabid uje uish hapa kijijin na mumeo mi nastaf mwakan naenda dar kwa mume wangu'' (mumewe anafanya kaz huko). ''Af hi nyumba itabid mjenge ingine hi haifai!'' ( ndo kwanza wanasubiria ajira mishe za town za mmewe ndo znawaweka mjin) Mumewe kwao wanaume wapo wengi na waliotangulia wote wapo kazin. Bidada kachoka hana hamu lkn ndo kashayavulia nguo maji yabd aoge 2.

Heeh...jamani hii kweli au simulizi?
 
Kabla hawajaoana angemmwambia .sasa inabidi amuache huyo mume maana umaskini ndio
Unapoanza

Umaskini hauwezi kuanza kwa kuishi na Mama yako Mzazi. Pamoja na kwamba uzungu umetawala, lakini kumbuka huyo Mama kamtoa mbali huyo mume wa rafiki yako. Kwanza Mama Mzazi sio extended familly, labda kama ingekuwa wajomba, shangazi. Hakuna anachoweza kumlipa, bali kuhakikisha kuwa anaishi vizuri katika maisha yake yaliyobaki. Kwanza, tambua kuwa kama Mama anakaa na ninyi watoto wenu watalelewa vizuri wakati ninyi mkiwa kazini. Hatakubali HG alete kijana ndani na kumwonywesha maziwa ya mtoto.
 
Nina rafiki yangu hajakaa hata mwezi Kwenye ndoa mama mkwe kahamia na wajukuu wa Tatu .rafiki
Yangu kanipigia simu analia kwa uchungu baada ya kumuuliza mume wake kwa nini wanahamia akasema yeye ni first born .Wewe ungefanyaje ?
Acha kufuatillia maisha ya watu.
 
Wahenga walisema ukipenda boga penda na maua yake,maisha ni kujipanga hivyo mwanaume alipokuwa anataka kuona ilifaa ajue anaoa familia ya namna gani.
 
Nimemwambia atupe vitu vyao nje .mume mwenyewe mshahara million 2 shillings jamani .extended family Noma

wewe inaonekana ni tatizo,
kwanza kwa kumshauri mwenzako kudharau wazazi wa mumewe, wazazi ndio Mungu wetu duniani. vitabu vinasema amtukanaye baba au mama na afe, na tena tunashauriwa kuwaheshimu wazazi wetu ili kwamba tuishi maisha marefu duniani. inawezekana hukubaliani na hili ila ni muhimu na lazima

pili, unadharau kipato cha shillling millioni 2, kweli Tanzania tunatofautina, sh million 2 unaidharau. una uelewa finyu sana kuhusu nchi yako, wengi wa Watanzania wana kipato cha 80,000; laki moja na nusu na laki tatu hapa. hata wengi tunaosoma jf ndio vipato vyetu hivi. sasa mwenzetu sijui upo wapi utuvute na sisi tupate hizo milion 10 kwa mwezi na sisi. kwa jinsi unavyoongea, unapata zaidi ya milion 15 wewe.

tatu, unaonekana una nyodo, kwa vijisenti vyako ama vya urithi toka kwa baba ama vya ufisadi unaoufanya huko kazini kwako, jambo ambalo unalitaka hilo hilo mwenzio aishi hivyo hivyo kama wewe. muache aishi maisha yake na usithubutu kumu haribia ndoa yake. akiachika utamwoa?

nne, huna maadili pamoja na kuonekana una watoto. hata mme wako inaonekana anapata kazi kwelikweli-pengine yuppo tu kwa ajili ya visenti vyako lakini hufai hata kidogo.

tano, huna busara hata chembe, badala ya kumshauri atupe mizigo ya wageni, ungemshauri kwamba mama arudi kule alikokuwa anakaa pamoja na wajukuu, halafu wajipange kuwasaidia wakiwa huko huko. watoto wa digitali mna matatizo kweli. hamna utu hata kidogo
 
Mm ni first born na sijaona hiyo shida. Nyie ni wale maselule wanopenda kutelezea kila kitu. Kusaidia wengine ni lazima. Acha ubinafsi hutaendelea. After all wakikaa wanaleta kadhia gani kwenye kitanda chenu?
 
Umaskini hauwezi kuanza kwa kuishi na Mama yako Mzazi. Pamoja na kwamba uzungu umetawala, lakini kumbuka huyo Mama kamtoa mbali huyo mume wa rafiki yako. Kwanza Mama Mzazi sio extended familly, labda kama ingekuwa wajomba, shangazi. Hakuna anachoweza kumlipa, bali kuhakikisha kuwa anaishi vizuri katika maisha yake yaliyobaki. Kwanza, tambua kuwa kama Mama anakaa na ninyi watoto wenu watalelewa vizuri wakati ninyi mkiwa kazini. Hatakubali HG alete kijana ndani na kumwonywesha maziwa ya mtoto.

nakila mtu akileta mama (mke na mume) yake inakuwaje?
 
Back
Top Bottom