MBINU Zinazotumika Kuiba Kura Tanzania

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Na declare Interest Mimi sina chama na ni Mtanzania nimeishi Rwanda miaka 10,Ni mtaalamu wa Fedha na Pia nimeshiriki kutoa mbinu za Uchaguzi na Ushindi kwa vipindi tofauti Tanzania kwa ufupi Nimesomea pia mambo ya Political impact Analysis (PIA)

Mbinu namba moja :
Tunatumia akina Mama wajawazito wengine kweli wajawazito wengine sio wajawazito wanabeba kura tumboni kwa kuzifunga vizuri na nguo zao, Hawa tunawapa kazi ya kuwa wasimamizi wa kituo cha uchaguzi

Mbinu namba mbili :
Tunatumia zile kofia zinaitwa cap wengi huzivaa kichwani hata tume ya uchaguzi hutoa cap nyeupe mule ndani hujaza kura kwa kushindilia na kuzibana na gundi maalum mara nyingi hizi kofia tunawapatia mawakala wetu mapema kwa kushirikiana na watendaji kata na mitaa

Mbinu namba Tatu :
Tunawatumia wazee hasa vikongwe kama mabibi na mababu Hawa kitaalamu tunawaita ( Duplication au Back up), nitaeleza maana ya hili neno asili na kwanini linatumika Hivi, kwa watu wa IT engineers wanajua system ikifeli lazima kuwe na backup, Hawa wazee tunawabebesha kura kwenye zile koti zao na mara nyingi hawa wazee huja na wasindikizaji ambao hujifanya kumsaidia Mzee hivyo nao tunawabebesha kura, akishapiga kura Mzee hujifanya kuchoka hivyo mkuu wa kituo husisitiza kachukueni wheelchair kwenye gari hapo ndipo kura zingine huletwa zilifungwa vizuri na wheelchair

Hii mbinu ya kutumia wazee Ndio mbinu kuu kwani kila mtu huona wazee ni wastaarabu hivyo hata msimamizi akisema wazee kwanza waingie mara nyingi hapa wazee huenda kushusha kura walizobeba

Mbinu mamba nne
Tunatumia Yale magari ya kubeba kura kupeleka wilayani au sehemu ya majumuisho, Chini ya kiti cha dereva na siti zingine tunajaza kura zinawekwa kiustadi mkubwa sana Sana na hapa madereva wanafahamu akicheza kidogo kazi hana, Tupo radhi kumwambia dereva aseme sanduku limepasuka wakati wa kusafirisha kama ikibainika

Mbinu namba Tano

Kuwatumia mawakala kinzani hii inaitwa (Separation) hapa tunawagawa mawakala pinzani kwa level zao au priority Scale, Tunawatafuta na kuongea nao kabla ya uchaguzi hapa tupo radhi hata kuwasumbua na kuwachelewesha vituoni ili wapate sababu wakibanwa na vyama vyao kuwa wamenunuliwa

Hii mbinu ni gharama it's much cost hivyo hutumika kwenye chaguzi ndogo ndogo au maeneo ya kimkakati ambapo mambo huwa magumu

Mbinu namba Sita
Hii inaitwa The Response sijui kwa kiswahili ni mbinu katili sana hapa kama mbwai na iwe mbwai,
Hii mbinu wataalamu wengi wa psychological risk wanaonya isitumike lakini ndio mbinu kuu ya sasa Tanzania hapa kuna mambo mengi

Kufuta matokeo
Kukubali matokeo
Kugawana ushindi mwembamba
Kutokubali kushindwa, hapa sasa Ndio watawala tunawashauri watumie polisi, wakuu wa wilaya na zana yeyote hata vitsho lazima kushinda

Katika hii mbinu za Response au muitikio Ndio mbinu hatari ingawa lazima tupime madhara kwanza yatakuwaje

Mbinu nyingine zitabaki Siri nitaeleza taratibu, Hili la kukimbia na sanduku lipo kwenye The Response tumewahi kuitumia hii Mbinu huko Ruvuma pia mwaka 2010 watu wa Dsm ndio wageni wa haya mambo
 
Uko sahihi..shida ni kwamba huwezi kuhoji kwani tayari wanalindwa hao wanaofanya hivyo.
 
Uko sahihi..shida ni kwamba huwezi kuhoji kwani tayari wanalindwa hao wanaofanya hivyo.
Mkuu hakuna asiyependa starehe, Kumbuka hizi mbinu hata ukizifahamu kuna haki za binadamu huwezi anza msearch Mzee kabeba nini au kumshika tumbo mjamzito utaitwa udhalilishaji
Haya mambo yanasomewa sana lakini hata yule anayejiita "Yericko Nyerere humu Jf anachambua tu mbinu za kijasusi tofauti Wengine wanazitumia kwenye ushindani
 
MLETA mada na wewe wote wazushi tu.Sanduku la kura unatumbukiza openly kila mtu akiwa anaona.Hizo za tumboni au kwenye kofia unazitoa wapi kuzitumbukiza sandukuni bila kuonekana?
 
MLETA mada na wewe wote wazushi tu.Sanduku la kura unatumbukiza openly kila mtu akiwa anaona.Hizo za tumboni au kwenye kofia unazitoa wapi kuzitumbukiza sandukuni bila kuonekana?
Unajua kagame zile 98 percent anatoa wapi za ushindi? Unaongelea masanduku gani yale unayoyakuta pale mbele yako au kituoni ndio unajua kura zenyewe eeh,
 
Kuna moja niliona miaka ya nyuma, Lori lililobeba masanduku ya kura, linaanguka, jingine linakuja fasta kufaulisha mzigo,na kutokomea.
 
Uko sahihi..shida ni kwamba huwezi kuhoji kwani tayari wanalindwa hao wanaofanya hivyo.
muongo mkubwa mleta mada.KURA zinajumlishwa vituoni na matokea yanabandikwa vituoni.Wakimaliza masanduku na karatasi za matokeo husafirishwa sio kwenda kuhesabiwa tena bali kujumlisha kwa ku base kwenye fomu za matokeo ya vituoni zilizosainiwa na mawakala wa vyama vyote.Hizo kura alizosema gari ya kubeba inakuwa nazo ni uongo labda aliona huko rwanda alikokaa miaka 10
 
Unajua kagame zile 98 percent anatoa wapi za ushindi? Unaongelea masanduku gani yale unayoyakuta pale mbele yako au kituoni ndio unajua kura zenyewe eeh,
basi angsema yeye mtaalamu koko wa wizi wa kura rwanda sio tanzania.Hizo mbinu haziko applicable kwa Tanzania
 
basi angsema yeye mtaalamu koko wa wizi wa kura rwanda sio tanzania.Hizo mbinu haziko applicable kwa Tanzania
Mkuu mbona Povu limeanza kukutoka nani kasema wewe Mwana CCM au Chadema mnafanya

Kaa kimya hata kura zikibebwa Mimi ni mshauri wa hayo mambo kuhusu analysis na assessment za uchaguzi, Nayafahamu na yanafanyika wewe unaumia unaogopa wataanza kuwakagua wazee vituoni au? Mbinu tunazo nyingi usihofu
 
Kuna moja niliona miaka ya nyuma, Lori lililobeba masanduku ya kura, linaanguka, jingine linakuja fasta kufaulisha mzigo,na kutokomea.
Bora wewe umeona haya ni mambo ya kawaida Sana, Tena kwenye kufaurisha hapo ndipo kilio huanza gari ya kufaurisha hubeba kura tena yale ya kubeba mchanga hutumika sana au Fuso
 
Mkuu mbona Povu limeanza kukutoka nani kasema wewe Mwana CCM au Chadema mnafanya

Kaa kimya hata kura zikibebwa Mimi ni mshauri wa hayo mambo kuhusu analysis na assessment za uchaguzi, Nayafahamu na yanafanyika wewe unaumia unaogopa wataanza kuwakagua wazee vituoni au? Mbinu tunazo nyingi usihofu
waweza kuwa umesoma lakini una elimu useless na outdated tanzania kura zinapigwa wazi unapotumbukiza kura kila mtu anakuona.Hizo kura za makoti sijui tumbo la mimba sijui kofia mmmmmm kawadanganye wengine sio watanzania na elimu yako koko kawashauri wasomi koko wenzio
 
Tutaendelea tu kupiga kura mpaka mwisho. Miaka yote Kabila alifanya hivyo leo hata huo uchaguzi anauogopa. Uzuri yana mwisho.
 
Naona hizi mbinu zimeanza kuwa msumari wa moto kwa baadhi ya Members humu, Kwa ufupi nilishadeclare interest hata chadema wakihitaji Counter attack ya Mbinu naweza toa ila kwa maslahi ya kazi na tumbo zitazitoa sasa,

Yehodaya ameshindwa kuelewa anaumia, Hizi mbinu zinasomewa muda mrefu na zipo nyingi sijazitaja nini Suluhisho kuna njia pia ya kufanya
 
Back
Top Bottom