Uchaguzi 2020 Karata ya mwisho ya CCM ni kuahirisha uchaguzi na sio kuiba kura

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
CCM ilianza mapema kutafuta kura, ilianza na mbinu ya kuzuia vyama vingine na wagombea wao kujitangaza akabaki Magufuli peke yake, ikaja na mbinu ya kununua wapinzani waliyoshauriwa na Polepole na KM Bashiru, CCM ikautumia uchaguzi wa serikali za Mitaa kuwahujumu wapinzani.

CCM walijua wagombea threat kwao ni Lissu na Seif wala sio Membe, ndio maana waliposikia Lissu atarudi na atagombea wakaanza kumtisha kuwa akifika ataishia gerezani au atauawa na mahasimu wake, wakasema hata akiteuliwa na chama chake NEC itamuengua, mbinu zote hizo zimeshindwa.

Ili kuwapunguza nguvu wapinzani NEC/ZEC wakaja na mbinu ya kuwaengua baadhi ya wagombea sasa wameaanza kuwazuia wasifanye kampeni, najua hii nayo itashindwa kama ilivyoshindwa ya kuwazuia wapinzani kwa miaka 5.

Safari hii chochote wanachokianzisha kinaonekana kushindwa ikiwa ni pamoja na kutoa matamko mbalimbali kupitia vyombo vya serikali.

Mbinu ya mwisho ya CCM ya kizamani wanayoitegemea ni kuiba kura, lkn nawatahadharisha CCM na NEC, safari hii zoezi hilo litakuwa gumu sana, daftari liko wazi kwenye mitandao wanachoongeza kinaonekana wazi kwa wananchi.

Jumuiya za kimataifa zinafuatia kwa karibu sana uchaguzi huu, wasifanye kosa hilo linaweza kubadili kabisa historia ya Tanzania.

Nimeshiriki chaguzi zote tangu za kuchagua Nyumba na Trekita baadaye ule wa Picha na Kivuli, binafsi naona Mbinu ya mwisho kabisa ambayo angalau itakuwa salama kwa CCM ni kuahirisha uchaguzi na kujipanga upya.
 
Hawatoahirisha Uchaguzi. Wanachoweza kufanya ni kile alichofanya Kenyatta hapo Kenya: Inapigwa model na calibrated equation ambapo kila kura moja ya Lissu, kwa Magufuli inamultiply let say by 1.7

Ni bora kuomba ushauri wa Maalim Seif. Mwaka 2015 aliwakalia kooni na ilibidi uharamia wa ajabu sana ufanyike ili kuokoa jahazi lao
 
Hawatoahirisha Uchaguzi. Wanachoweza kufanya ni kile alichofanya Kenyatta hapo Kenya: Inapigwa model na calibrated equation ambapo kila kura moja ya Lissu, kwa Magu inamultiply let say by 1.7

Ni bora kuomba ushauri wa Maalim Seif. Mwaka 2015 aliwakalia kooni na ilibidi uharamia wa ajabu sana ufanyike ili kuokoa jahazi lao
Mwaka huu haitojitokeza tena, Wasahau
 
Ukweli ni kwamba haya usemayo ni maneno ya MFA MAJI. CCM inao mtaji wake kwa wananchama wake na wapenzi wake siyo "kwenye mbinu chafu".

Na haya mnayasema sasa hivi kwa sababu ya kuaminishwa vibaya na kwa UONGO na akina Amsterdam, mkidhani watawasaidi kwa njia yoyote ile kwenye kushindwa kwenu kwenye uchaguzi huu. Hao wanatumia mbinu ya mwaka 47 kutaka kuleta fujo katika nchi zetu. Tunawafahamu na tumewashtukia!
 
Ukweli ni kwamba haya usemayo ni maneno ya MFA MAJI. CCM inao mtaji wake kwa wananchama wake na wapenzi wake siyo "kwenye mbinu chafu". Na haya mnayasema sasa hivi kwa sababu ya kuaminishwa vibaya na kwa UONGO na akina Amsterdam, mkidhani watawasaidi kwa njia yoyote ile kwenye kushindwa kwenu kwenye uchaguzi huu. Hao wanatumia mbinu ya mwaka 47 kutaka kuleta fujo katika nchi zetu. Tunawafahamu na tumewashtukia!
Wewe ni tomaso hata yule aliyekimbia na sanduku la kura mchana kweupe hukuamini.
 
Hawatoahirisha Uchaguzi. Wanachoweza kufanya ni kile alichofanya Kenyatta hapo Kenya: Inapigwa model na calibrated equation ambapo kila kura moja ya Lissu, kwa Magu inamultiply let say by 1.7

Ni bora kuomba ushauri wa Maalim Seif. Mwaka 2015 aliwakalia kooni na ilibidi uharamia wa ajabu sana ufanyike ili kuokoa jahazi lao
Nafikiri safari hii hackers wako pande zote.
 
Ukweli ni kwamba haya usemayo ni maneno ya MFA MAJI. CCM inao mtaji wake kwa wananchama wake na wapenzi wake siyo "kwenye mbinu chafu". Na haya mnayasema sasa hivi kwa sababu ya kuaminishwa vibaya na kwa UONGO na akina Amsterdam, mkidhani watawasaidi kwa njia yoyote ile kwenye kushindwa kwenu kwenye uchaguzi huu. Hao wanatumia mbinu ya mwaka 47 kutaka kuleta fujo katika nchi zetu. Tunawafahamu na tumewashtukia!
Good lete HOJA Abuu!
 
Hivi mnaposema ccm ina mtaji wake wa wanachama huwa mnatumia akili kuongea au mnaimba tu kama kasuku? Huo mtaji ni maroboti wasio na utashi wa kuhama chama wanapoona dhuluma inafanyika. Au ukiwa ccm huwezi kuhama chama hata kama unadhulumiwa?
 
I can grasp the point.
Uko sahihi. Magufuli na CCM yake ulimi nje. Hoja za Toto Tundu zimewavuruga vibaya! Nimecheka sana nilipomsikia Magufuli akijibu hoja ya Lissu kuwa ATI VITAMBULISHO VYA MACHINGA SIYO LAZIMA!!!

Lissu akapigilia msumari wa 6 inches kuwa Kama siyo lazima basi Magufuli AIFUTE HIYO SHERIA na ARUDISHE ZILE 20 ELFU kwa MACHINGA wote nji nzima!!! Bado sijasikia response ya Mataga... yajayo yanafurahisha Sana.
 
Back
Top Bottom