Wapinzani waja na mbinu mpya ya kuiba kura uchaguzi wa serikali za mitaa

luchili

Senior Member
Nov 30, 2018
131
225
Wapinzani wameona jinsi gani Rais MAGUFULI akipambana kuleta maendeleo ya kweli katika Nchi yetu ya Tanzania,Hata baadhi ya wapinzani wanamkubali sana Magufuli lakini kwa kuwa wao wameshaapa kuwa wapinzani hawana jinsi bali ni kuendelea kumwaga sumu kwa wananchi ili ionekane wao ndio watu sahihi katika kuwapatia maendeleo.

Wamekuwa wakimwaga sumu kwa kuzisambaza picha za wagombea wa Serikali za mitaa wakijaza fomu zao na kuwaambia wananchi kwamba kuna watendaji wamekuwa wakiwasaidia wagombea wa CCM kujaza fomu huku wamefunga ofisi ili wapinzani wakose fomu.

Ukifuatilia kwa umakini kabisa mitandaoni utagundua kuna vikundi fulani ambavyo vimeandaliwa na wapinzani kwa ajili ya kumwaga sumu mbalimbali ili kuwachanganya watu na hata waonekane wao wanaonewa na hata sasa wamejipanga kuuchafua uchaguzi wa serikali za mitaa ili ionekane wanaccm wameiba kura.

Ila watanzania mkae mjue Rais Magufuli hana muda wa kukaa na watendaji wake kwa ajili ya kupanga mambo ya kijinga kama wapinzani wanavyodai kwamba watendaji wa kata wametumwa baada ya kukaa na Rais lakini swali la kujiuliza kama kweli wametumwa mbona kata zingine wanachukua fomu bila ya tatizo lolote kwanini hao wachache kama kweli amewapa maagizo basi kata zote zingekuwa na taarifa moja tu.

Aidha,kama ww ni mfuatiliaji mzuri wa habari mitandaoni utaona ni jinsi gani wapinzani wanavyojipanga kumwaga sumu kama wataona kitu hawakipendi mfano lile sakata la vodacom walilihamasisha sana watu waache kutumia mtandao wa vodacom eti kwa sababu ya kuingilia uhuru wa kusikilizisha sauti za wateja wao,sasa hivi wanaanzisha kuwa watendaji wa kata hawakai kwenye ofisi zao kwa makusudi na hata kunyimwa fomu zao, lakini inawezekana kuna masharti ambayo wanaweza wakawa hawajayafuati, na sio kila wakati upo ofisini inawezekana wao wanakuja mida ya mapumziko kwa makusudi kabisa ili ionekane wamenyimwa hizo fomu.

Binafsi naona hiyo ni mbinu yao mpya ya jinsi ya kuiba kura kwamba ionekane wao ndio wameshinda wakati hawajashinda kwa kuwa waliweza kumwaga sumu kabla ya uchaguzi. Ila wapinzani wakae wajue wananchi wana akili zao wao ndio watakaoamua hakuna mtu anayependa kuoongozwa na mtapatapa bali mtendaji tu.
 

Mromboo

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
2,635
2,000
Hata Kama Mama zenu hawakua na maziwa ya kutosha kutokana na lishe duni,hivi hata hakukua na jirani aliyekua mfugaji japo mpate maziwa ya ng'ombe?mnatia mashaka akili zenu.
Hii ni mpya ndugu yangu? Yaani jamabazi anatuhumu kuwa anataka kuibiwa na mchungaji? Hii ndo awamu ya tano. Awamu ya namba tasa ya kiukweli. Yaani CCM huwa hawaishiwi vituko. Nataka niwaone mpaka Nov. 24 watakuwa wamafanya yapi.
 

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
2,347
2,000
Mkuu sitambui imani yako, lkn kwa vyovyote vile unahitaji maombi maalumu ili upate hali ya uelewa wa mambo ktk uhalisia wake wote. Kwa sababu naona hata vitu vilivyopo bayana unashindwa kuvielewa.
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,878
2,000
hakika kuitetea CCM inabidi uwe na akili ya maiti.
Halafu CCM wamekuwa wachovu kweli! Yaani CCM wanisimamishie mgombea uenyekiti mtaa tunamjua ni mlevi, mpenda rushwa na kipindi kilichopita ametukwamisha mambo mengi hapa mtaani?
Kigezo wanachotumia Magufuli kanunua ndege! Jee zinahusianaje na huyu mgombea? Hakuna. Magufuli anajenga reli! Huyu mlevi na mla rushwa reli inahusianaje naye na mtaa wetu?
Hakuna mwenyekiti yeyote ambaye uwepo wa Magufuli una mahusiano na yeye mtaani kwake.
 

magu2016

JF-Expert Member
Oct 8, 2017
6,492
2,000
Rudi shule ukajifunze propaganda, wananchi wameshaamka wanajua kila uchafu unaoendelea ndani ya utawala huu.
Ni kweli wameamka wanajua pumba ya upinzani hawasumbuki nao. Mara hakuna kujiandikisha mara tena eti wananyimwa fomu sasa watapigiwa kura na nani wakati wanasaccos wenzenu hawakujiandikisha??
 

monde arabe

JF-Expert Member
Oct 22, 2017
9,437
2,000
hakika kuitetea CCM inabidi uwe na akili ya maiti.
Nilihusika kwenye zoezi la uandikishaji wa wapiga kura,tulipewa agizo na wakubwa kuandka majina hewa na haya majina hewa yatakuja na kura hewa
Iko hivi;kwenye zile kata au vitongoji ambavyo ccm wanauhakika wa kushinda basi wanatoa form kwa wagombea bila kipingamizi lkn,kwenye vitongoji ambavyo wanajua kuwa watashindwa wanawatoroka wagombea wa upinzani!
 

magu2016

JF-Expert Member
Oct 8, 2017
6,492
2,000
Nilihusika kwenye zoezi la uandikishaji wa wapiga kura,tulipewa agizo na wakubwa kuandka majina hewa na haya majina hewa yatakuja na kura hewa
Iko hivi;kwenye zile kata au vitongoji ambavyo ccm wanauhakika wa kushinda basi wanatoa form kwa wagombea bila kipingamizi lkn,kwenye vitongoji ambavyo wanajua kuwa watashindwa wanawatoroka wagombea wa upinzani!
Watapikiwa kura na nani wakati hawakujiandikisha mliwakataza!!
 

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,950
2,000
Ni kweli wameamka wanajua pumba ya upinzani hawasumbuki nao. Mara hakuna kujiandikisha mara tena eti wananyimwa fomu sasa watapigiwa kura na nani wakati wanasaccos wenzenu hawakujiandikisha??

Suala la kupigiwa kura halina mahusiano na kunyimwa fomu, huenda hujui unaloongea. Tunataka wachukue fomu kisha siku ya kupiga kura tuonyeshe ni jinsi gani ccm haikubaliki. Mnataka mgombea wa ccm apite bila kupingwa ili mfiche aibu ya watu kususia huo uhanithi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom