Elections 2015 Kuelekea 2015: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

hii inamaanisha ili chadema ishinde kwa kishindo kinachotakiwa, lazima ikubali kubadilika and start doing things right besides doing the right thing!.
jambo zito hilo
 
Nimegundua humu jamvini chadema mipewa ushauri mnakuja juu, hata kama una manufaa na chama chenu kwanini? nashindwa kuelewa! ni mtu gani asotaka kushauri? hii ni ishara ya chama kibaya, mnataka kujifanya nyie kama nyerere alokataa ushauri na kujifanya kutawala kwa akili zake yeye tu ! hivi mtafika kweli?

mtoa mada hajaweka waz CDM ibadilikke kwalip, we unaweza ukaambiw badilika na hujawekwa waz na ukabadilika sijui utabadilika kwa lip? achen kukurupuka.
 
Hivi chadema itashinda kwa kura za kina nani? wachagga? wako wangapi nchi hii?

kama wachaga waliweza kuwachagulia wabunge iringa,mwanza,dar,arusha,mbeya,singida ninini kitawazuia kuwapa nchi yote?
hizi propaganda hazijawahi kuisaidia ccm bado wewe na ukilaza wako unaendelea kuziamini?
 
Mkuu Pasco

Uwa unaleta hoja nyingi sana hapa JF kuhusu kuchokwa kwa CCM na kupanda kwa umaarufu wa CHADEMA. Tatizo lako ni hili; Hoja zako nyingi ni za kinafiki, umekaa katikati, unasubiria uone shilingi itaangukia wapi. Kwa hoja kama hii ya leo, inaonyesha kuwa unaamini kuwa CCM imechokwa, ila unaamini kuwa wananchi wanaipenda CHADEMA bila sababu yoyote isipokuwa ni kwasababu wameichoka CCM. Hii sababu yako sio toshelevu kabisa, na hapa ndipo unadhihrisha unafiki wako au ufinyu wa kufikiri na kujenga hoja. Sasa kwa mawazo haya inaonyesha kuwa wewe ni mnafiki, unasubiria uone wapi shilingi itaangukia ili na wewe ujiweke kwenye hiyo nafasi yaani upande wa CCM au CHADEMA. Nakupunga wakati wa uchaguzi wa Arumeru Mashariki, ulikuja na hoja kuonyesha kuwa CHADEMA haitashinda, baada ya kushinda ukaja na hoja hapa kuwa "wewe unafahamu kuwa CCM imechokwa isipokuwa CHADEMA haijajipanga" na nakumbuka hasira za wana-CHADEMA zilikushukia kwa kupewa vidonge vyako.
 
SISI SOTE NI NDUGU TATIZO NI CCM
Mkuu wangu shukran na umegusia haswa pale panapotuweka sote pamoja nyuma ya Chadema.. Je hii inatosha kweli kutegemea kuchoka kwa CCM ndio uwe mtaji wetu kisiasa?. Kwa mwenye kutazama ndani vizuri sana atafahamu support kubwa ya Chadema ni kuipiga mande CCM waondoke, mtaji huu hautoshi kisiasa maana wananchi hawa hawana tumaini la sisi kufanya nini baada ya ushindi.

Hii ni tahadhari tu kwa wapenzi wa Chama. Ikiwa watu wengi sana wameingia Chadema kwa sababu ya Uzalendo wao, UTU wao ili kumfukuza adui yao mkubwa CCM ina maana watu hawa hawategemei lolote kutoka kwetu wala hawana mapenzi ya dhati kwa chama isipokuwa hasira zao kwa CCM kama vile Simba mla watu kaingia kijijini wanakijiji wamepiga parapanda kumfanyia. Je, tukisha muondoa Simba huyu what next? hapo ndipo tunapogwaya maana salama tu haitoshi na malengo ya chama sio tu kumuondoa CCM isipokuwa kuingia Ikulu na kuongoza.

Ebu tujiulize tukiweza kuindoa CCM mwaka 2015 hawa watu waliokuja kutoa pande na harambee kumfukuza mnyama huyu wanategemea nini kutoka Chadema?
 
Mkuu Pasco inaelekea hufahamu maana ya neno ridhaa. Maamuzi yoyote yanayofanywa na mwanadamu baada ya kupokea "consideration" ya aina yoyote ile kamwe hayawezi kuitwa ni ya ridhaa na ndio maana baadhi y a matokeo hubatilishwa kwa kuwa si matokeo halali

Mkuu BAK, determinant factor ya ushindi wowote kupitia ballot box ni idadi ya kura halali!. Matokeo yakishatoka, "the end justify the means", kama mshindi alihonga ili apigiwe kura au alichakachua, kura batili zika its way into ballot box, mshindi ni aliyeshinda no matter what!. Hao wanahongwa pilau, t-shirt na kofia na kupiga kura zao in favour ya CCM, kura zao ni halali kwa sababu hiyo ndiyo ridhaa yao!.
 
Last edited by a moderator:
Lisemwalo lipo,kama halipo linakuja. Karibu sana mwaka 2015.Tunakukaribisha kwa mikono miwili hata kama ni kwa udi na uvumba tutakusubiri. Inasikitisha wengine wametangulia au kutangulizwa kwa lazima kwa kuuawa(Daudi Mwangosi na wengine) mbele ya haki bila kukuona mgeni usiyejulikana mwaka 2015.

Wanasiasa na wasio na siasa wanakusema sana pengine kuliko ndugu zako wengine waliopita. Ajabu haijulikani utakuja kwa shari au mema. Je,hao wanaokusema sana na kusubiri ujio wako kwa hamu na wengine kukosa usingizi, watakuwepo kweli utakapowasili siku hiyo saa sita kamili usiku toka safari ya mbali?

Kesheni mukiomba, kwa maana hamjui saa wala siku.
 
Ukweli husemwa:


Pasco,
umeuma na kupuliza. Ni kama vile umetembea kilometa mia moja halafu ukarudi tena pale ulipoanzia. Umewapa matumaini wapenzi na wanachama wa hivi vyama halafu ukahitimisha kwa bad news.

Hivi unaposema CDM watashinda kama watabadilika na kusikiliza, kwani CCM wao hawabadiliki. Tusikae hapa na kuanza kubweteka wakati katika siasa, masaa 24 ni sawa na mwaka.

Kuna factor nyingi tu ambazo huko mbeleni zitachangia kwa kiasi kikubwa kibadilisha upepo wa kisiasa.


Ningependa nikuulize swali la kuchombeza, Je, matokeo yatakuwaje kama CDM wakisikiliza na kubadilika halafu nao CCM ikamsimamisha ENL kuwa mgombea wao?

Mimi ninafikili, mwenye kuiondoa madarakani CCM ni CCM yenyewe. Uchovu wa CCM ndiyo kifo cha CCM. Mabadiliko ndani ya CDM hayatakuwa na impact kubwa ya kufanya watu kwa mamillioni wawape kura.
 
Pasco,

Umenena vema,ni rahisi sana kukosoa na kurekebisha makosa.au niseme ni rahisi sana kutazama boriti lililo ndani ya jicho la mwenzako,LAKINI nivigumu sana kuwa sehemu ya hayo mazuri unayoyafikiria.

Jamani serikali ya CCM haiwachoshi tu bibi,shangazi,na watoto wa wanachama wa chadema.Sote tumepigika,sote Tunaumia,sote tunateseka.NI lini!!!!!!!! kauli hizi za kunyooshea vidole wengine kwamba wafanye hivi wafanye vile zitakomeshwa.

Huu ni mda wa kufanya maamuzi na kusimama upande mmoja.kama uko CCM zungumza kama mwanaCCM na kama ni mpambanaji simama ujibainishe na kuwa sehemu ya mabadiliko.

Tuachane na uvuguvugu ndio unaochelewesha safari yetu ya ukombozi,nchi hii bwana,

walimu vuguvugu
madaktari vuguvugu
waandishi vuguvugu
wanasiasa vuguvugu

Tatizo liko hapo.!!!!!!!!

EVERYBODY HAS TO CHANGE .

Mama Junior,
Usilazimishe watanzania wote wawe wafuasi wa vyama vya siasa kuna watanzania wengine hawana vyama vya siasa ndiyo maana kwenye katiba mpya wanaitaji mgombea binafsi.
 
Dah, ama kweli nchi hii watu wamepagawa na katu hawataki tena kusikia kitu CCM, Kikwete wala wakala wake!!!!!!!!! Mkuu ungetulia kidogo ukasoma hadi mwisho maoni ya Pasco humu pengine marejesho yako yangekua bora zaidi ya hapo chini.

pumba na mchele zikichanganywa pamoja.

badilika kwanza wewe na mafumbo yako. watanzania tushachoka na mafumbo na misemo(ya jk).
 
yataje hayo mapungufu kama kweli we unanianjema na chadema
Mkuu mwananchi wa kawaida kijijini hahitaj kujua ufisd wa ccm anahtaj umwambie ni jins gan utatatua changamoto zake za miundo mbinu afya na elimu ni lazima CHADEMA 2WE NA SULUHISHO MBADALA KWA CCM ILIYOCHOKWA
 
Wakuu mimi nina swali moja....

Hivi KANU ya Kenya na ile CCM ya Zambia iliyoondolewa na Michael Satta hawakuwa na propaganda kama hizi?
Na kama walikuwa nazo' je kwanini vyama hivyo vilin'golewa madarakani? Naombeni jibu wakuu!
 
Mkuu BAK, determinant factor ya ushindi wowote kupitia ballot box ni idadi ya kura halali!. Matokeo yakishatoka, "the end justify the means", kama mshindi alihonga ili apigiwe kura au alichakachua, kura batili zika its way into ballot box, mshindi ni aliyeshinda no matter what!. Hao wanahongwa pilau, t-shirt na kofia na kupiga kura zao in favour ya CCM, kura zao ni halali kwa sababu hiyo ndiyo ridhaa yao!.

Pasco Naomba unifumbue macho zaidi.
Umesema kwa sauti kubwa sana, VIONGOZI WA CHADEMA WANATAKIWA KUBADIRIKA" nimekusikia pia vizuri sana kwamba wanatakiwa "KUFANYA MAMBO YAO KWA USAHIHI" Naomba mifano tafadhali.
 
Mkuu mwananchi wa kawaida kijijini hahitaj kujua ufisd wa ccm anahtaj umwambie ni jins gan utatatua changamoto zake za miundo mbinu afya na elimu ni lazima CHADEMA 2WE NA SULUHISHO MBADALA KWA CCM ILIYOCHOKWA
We ni mvivu wa kuhudhuria mikutano ya CDM ungefaham na usingeleta huo umbea wenu hapa jf.hiz ndizo ajira alizo ahid jk kuwa atatoa ahsante tunaziona
 

Attachments

  • 304352_112377832246501_1200285824_a.jpg
    304352_112377832246501_1200285824_a.jpg
    5.6 KB · Views: 176
Mkuu mwananchi wa kawaida kijijini hahitaj kujua ufisd wa ccm anahtaj umwambie ni jins gan utatatua changamoto zake za miundo mbinu afya na elimu ni lazima CHADEMA 2WE NA SULUHISHO MBADALA KWA CCM ILIYOCHOKWA

Kwa hiyo unachotaka ni kwamba CHADEMA waanze kutoa ahadi za kujenga madaja? barabara? masoko n.k? or else toa sample la suluhisho ambalo unategemea CHADEMA walifanye sasa japo kidogo tu.
 
Chadema sio rahisi kushinda, kwa sababu imeonesha dhahiri kuwa ni chama cha kanisa, sisi waislamu hatuwapi kura zetu , hilo lazima walijue, sasa watashinda kwa kura za kina nani?

Mimi niliwashauri zamani na niliwauliza wana kipi cha kuwaahidi Waislaam? Nyuzi ikaishia kufutwa mbio mbio na moderator mwenye mapenzi na chadema, badala ya kujadili, mwenyewe akidhani anaitengenezea chadema kumbe anaiharibia.

Huo ndio ufinyu mkubwa wa hawa watu. "Hawasikii la muadhini wala mteka maji msikitini".
 
Back
Top Bottom