Elections 2015 Kuelekea 2015: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

Wachagga wapo wengi sana zomba ngoja ni kumwagie list.

[1] Anthony G Mbassa huyu ni mchagga wa Biharamulo magharibi

[2] Prof Kulikoyela Kahigi huyu ni mchagga wa Bukombe Shinyanga

[3] Simon Peter Msigwa huyu ni mchagga wa Iringa Mjini

[4] Yohana Natse huyu ni mchagga wa Karatu

[5] Halima Mdee huyu ni mchagga wa Kawe Dar

[6] Zitto Z kabwe huyu ni mchagga wa Kigoma kaskazini

[7] John Shibuda huyu ni mchagga wa Maswa mashariki

[8] Joseph Mbilinyi huyu ni mchagga wa Mbeya mjini

[9] David Silinde huyu ni mchagga wa Mbozi magharibi Mbeya

[10] Mustafa Akonnay huyu ni mchagga wa Mbulu

[11] Meshack Opulukwa huyu ni mchagga wa Meatu Shinyanga

[12] Said Arf Amour huyu ni mchagga wa Mpanda Rukwa

[13] Vicent Kiboko Nyerere huyu ni mchagga wa Musoma mjini

[14] Ezekia Wenje huyu ni mchagga wa Nyamagana Mwanza

[15] Tundu Lissu huyu ni mchagga wa Singida Mashariki

[16] John Mnyika huyu ni mchagga wa Ubungo Dar

[17] Salvatory Machemuli huyu ni mchagga wa Ukerewe........

Mkuu zomba kama wachagga wameenea kila pembe ya Tanganyika ni kwanini wasishike dola haa ha ha ha wanchekesha!!!!!!.




Hivi chadema itashinda kwa kura za kina nani? wachagga? wako wangapi nchi hii?
 
mimi huwa nafurahi sana nikiona ushauri wa watu kwa chadema hivi unasema kibadilike Je uliwapa ushauri wakati hawajakubalika ili wakubalike? kama sio waunge mkono kwa kuhamasisha jirani na ndugu zako ili tusaidie kuondoa mfumo mbovu uliopo, tuacheni kuwapanikisha viongozi wa chadema kilchopangwa na mungu kamwe binadamu hawezi kukitengua atachelewesha tu na kwa maono yangu ilicheleweshwa toka 1995 na sasa 2015 ndi mwisho.

hakuna mabadiliko hakuna maendeleo na watanzania naombwa wahamasishwe kuichoka CCM sababu nyingine baadae. ukimchoka mume au mke si unachukua hatua na sababu zitatolewa mbele ya vikao vya wanafamilia?
 
Hivi chadema itashinda kwa kura za kina nani? wachagga? wako wangapi nchi hii?

akili za magamba.....hivi bado unaamini kuwa cdm ni chama cha wachaga! ajabu.kama ni hivyo, ukichanganya wachaga wote walio ndani ya ccm na vyama vingine vyote, kisha ongeza wakristo wote, kisha watz wote, cdm itakuwa bado haijaingia madarakani? ........kumbuka..cdm ni chama kisicho na dini wala kabila.
 
Wanabodi,
Preamble: "Kwa opinion yangu, Uchaguzi wa 2015, Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!"!

Preamble: "Kwa opinion yangu, Uchaguzi wa 2015, Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!"!

Trend za Upepo wa Kisiasa kuelekea 2015, zinavuma kwa Kasi ya Ajabu kuelekea Direction ya Mabadiliko (The Wind of Change, is Sweeping Across Tanzania) na kila dalili inaonyesha na kuelekeza Chadema is gaining momentum and there is "nothing" to stop it kuchukua nchi mwaka 2015 iwapo...

1. Preamble yako ni fedheha kwa kila mtu si CDM itayochukua nchi bali ni kwa wapiga kura watakaokabidhi nchi kwa chama cha mabadiliko

2. Neno "______ kwa kishindo" ni kauli mufilisi inatokana na nguvu ya ziada inayotumika kwenye kuhalalisha matokeo ya kura knyume cha wapiga kura na wala si hiari ya wapiga kura.

Kwenye mazingira, upepo unazuiliwa na upandaji miti. Kipindi tulicho nacho chama tawala kinaweza kupanda miti kuzuia upepo. Kinachotakiwa ni dhamira ambayo HAWANA kwa hiyo upo sahihi.

Ila "!... Only If...!"!; iwapo..." haya maneno haya "uswi". Kumbuka unapopanda mahindi mbegu inaoza halafu inachipua hakuna suala la "iwapo". Na mabadiriko haya yapo uje upepo, mvua, jua; SUALA kama ulivyoliweka ni kuchokwa chama tawala na dhamira zake mufilisi. Sitegemei chama kitakachochukua nchi kifanye miujiza. Nategemea kitakuwa na changamoo nyingi ila kitakuwa na mikakati shirikidhi, ya ukweli na yenye dhamira safi.
 
Wanabodi,
Preamble: "Kwa opinion yangu, Uchaguzi wa 2015, Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!"!

Trend za Upepo wa Kisiasa kuelekea 2015, zinavuma kwa Kasi ya Ajabu kuelekea Direction ya Mabadiliko (The Wind of Change, is Sweeping Across Tanzania) na kila dalili inaonyesha na kuelekeza Chadema is gaining momentum and there is to stop it kuchukua nchi mwaka 2015 iwapo...

  • Hakuna ubishi kuwa siku zote, CCM imekuwa ikishinda chaguzi mbalimbali "kihalali" na mtaji wao mkubwa wa ushindi ni "watu".
  • Hakuna ubishi kuwa CCM kama chama, kimechoka, dalili zote za chama kichovu kinachosubiri kifo, tayari, zimeisha jitokeza kwa CCM, kinachosubiriwa sasa its only a matter of time ni lini kitaangwa rasmi, hiyo 2015 naiona kama ni mbali sana!.
  • Hakuna ubishi kuwa wengi wa hao "watu", wamekuwa wakuichagua CCM sio kwa sababu wanaipenda sana!, (waipende kwa lipi?), la hasha!, "watu" wamekuwa wakiichagua CCM kwa mazoea tuu!.
  • Hakuna ubishi, kuwa wengi wa hao "watu" waliokuwa kuwa wakiichagua CCM kwa mazoea, sasa wameichoka, hivyo 2015, hawatachagua tena chama kwa mazoea, bali watachagua chama kwa "sababu"!.
  • Hakuna ubishi kuwa Chadema, ndicho chama kinachokubalika zaidi kwa sasa kuliko CCM, hivyo ule mtaji mkubwa wa CCM iliyoutegemea kwa miaka nenda miaka rudi, sasa umehamia Chadema!.
  • Kama ambavyo CCM imekuwa ikichaguliwa kwa mazoea tuu, na sasa CCM imechokwa, vivyo hivyo kwa sasa Chadema haina lolote la kukifanya kipendwe, bali kinapendwa kwa sababu "watu" wameichoka CCM!.
  • Kama utaguzi utaitishwa leo, Chadema itashinda kwa kishindo kikubwa cha ajabu, lakini ukiwauliza hao watakaokipa Chadema ushindi, ni sababu zipi za kuichagua Chadema, hawatakupa sababu yoyote zaidi ya kuichagua Chadema kwa sababu wameichoka CCM!.
  • ili Chadema iweze kupata ushindi wa Tsunami kwa uchaguzi wa 2015, lazima Chadema ikubali kubadilika, isiendelee kuutegemea huu umaarufu wa muda kwa kushangiliwa na umati wa watu walioichoka CCM, bali Chadema sasa lazima iwape Watanzania sababu za kuichagua Chadema.
  • So far so good, Chadema is doing a good job kwa sababu M4C is doing the right thing!. Doing the right thing alone, doesn't guarantee sweet clear victory for Chadema, it got to do things right!. Hii inamaanisha ili Chadema ishinde kwa kishindo kinachotakiwa, lazima ikubali kubadilika and start doing things right besides doing the right thing!.
  • Hivyo ndugu zangu viongozi wa Chadema najua 2015 mmedhamiria kwa dhati kuchukua nchi kwa ushindi wa kishindo!, lakini ili lengo hili litimie, ni lazima kwanza mkubali kusikiliza, pili mkubali kubadilika kwa kuzikiliza hoja zinazotolewa kuhusu Chadema na kuzifanyia kazi!.

Naomba kumalizia kwa nukuu kutoka kwa mmoja wa wanachama wetu humu jf.



Kwa wale wapenzi wa Chadema, ni vema kuwa great expectations on Chadema kuchukua nchi 2015, only if Chadema itabadilika, vinginevyo keep hopping for the best and get prepared for the worst kama Chadema haitabadilika na 2015 itakuwa ni CCM Tena!.

NB. Msiniulize Chadema wabadilike nini, wahusika wameshaambiwa imebaki kusikiliza na kutekeleza!.

Naomba kuwasilisha.

Pasco.




Namba 9 nakukumbusha Mkuu uendelee kuichangia M4C ili iweze kutekeleza malengo yaliyopangwa.. Vinginevyo; Message Sent!.
 
haya mawazo ni mazuri sana, hata mm ni mpenzi wa CDM tusipojirekebisha katu Ikulu hatuioni!!! tusiwe wepesi wa kuwaambia wezetu wameongea pumba ili hali mawazo ni mazuri na ya kutujenga.... ni hayo tu kwa leo!!!

hembu wekeni mambo ya wao kujirekebisha mbona hamueleweki. huwa napenda kusema watanzania wa leo sio wa jana na hawadanganyiki wala hawachaganywi tena. na kama unaipenda CDM si uende makao makuu ukatoe hayo mapungufu ili warekebishe na uingie kwenye kumbukumbu za mchango waku katika kukisaidia.
 
Wanabodi,
Preamble: "Kwa opinion yangu, Uchaguzi wa 2015, Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!"!

Kwa wale wapenzi wa Chadema, ni vema kuwa great expectations on Chadema kuchukua nchi 2015, only if Chadema itabadilika, vinginevyo keep hopping for the best and get prepared for the worst kama Chadema haitabadilika na 2015 itakuwa ni CCM Tena!.

NB.
Msiniulize Chadema wabadilike nini, wahusika wameshaambiwa imebaki kusikiliza na kutekeleza!.

Naomba kuwasilisha.

Pasco.




Ume amua kumtosa mzee wa watu siyo? M4C si mchezo haya we karibu.....Lakini CDM is peoples power haiendeshwi kwa matakwa ya individuals bali ya public!
 
Napata tatizo moja, TANU na baadae CCM wametawala tangu 1961 kufikia mwaka 1995 alipong'atuka Nyerere. Wakati huo hawakuwepo mafisadi, wala rushwa,sijui wauwaji, mikataba mibovu and so and so....na nchi haikuendelea na tumeendelea kuwa masikini. CDM wanachoongelea ni matatizo hayo hapo juu kama kwamba yakiondolewa na umaskini utakwisha. Kwa vile siamini hilo, naomba nifahamishwe CDM itafanya nini cha ajabu hapo 2015 kama wataingia madarakani? Naona sasa haziongelewi sera bali kuondoa mambo yanayotokana na matukio yanayojitokeza...! Nipeni ushawishi niichague CDM hapo 2015. (ila sasa hivi siandamani ng'o niko kwenye kujitafutia riziki)!!
 
kuna wanyakyusa, wahehe, waha, wanyamwezi, wasukuma, wakurya, na wengine kibao, sema jingine...Zombi

kama CDM ni ya wachaga na kwasababu wachaga wameweza kufanya mambo yao vizuri na kupata maendeleo naona si vibaya tukawakabidhi na nchi sio mbaya?
 
haya mawazo ni mazuri sana, hata mm ni mpenzi wa CDM tusipojirekebisha katu Ikulu hatuioni!!! tusiwe wepesi wa kuwaambia wezetu wameongea pumba ili hali mawazo ni mazuri na ya kutujenga.... ni hayo tu kwa leo!!!
Nimekubalina na wewe dada, lakini Avatar yako yaweza kuwachanga watu wakafikiri wako Jukwaa la MMU.
 
Chadema sio rahisi kushinda, kwa sababu imeonesha dhahiri kuwa ni chama cha kanisa, sisi waislamu hatuwapi kura zetu , hilo lazima walijue, sasa watashinda kwa kura za kina nani?

Vipi kama nature itasababisha watu wa dini moja (mf. wote waisilamu) tu wakawa ndiyo wagombea mta imba koras ipi tena?
 
umekunywa nini leo pasco?
Sikubaliani na namba 6: si kweli kuwa CDM inapendwa sababu tu CCM imechokwa,,!
Nguvu kubwa ya CDM ni vijana “TAIFA LA LEO” Ambao 1977 wakati ccm inaanzishwa ama hawakuwepo au walikuwa watoto wa miaka 1-8 . Hivyo Hoja ingekuwa CCM IMECHOKWA basi wazee ambao relatively ni wengi ccm kuliko CDM ,wote wangekuwa CDM maana walikuwa nayo tangu 1977 ilipo anzishwa.

My opinion: CDM Inapendwa kwa sababu sera zake zinajibu maswali ,mahitaji na matarajio ya vijana wa taifa hili,
1: Ukosefu wa ajira kwa vijana.
2: kupiga vita ufisadi kwa vitendo.
3:uwajibikaji .
4: sera mbadala ya mikopo ya elimu ya juu
5:bei nzuri ya mazao ya kulima na uhuru wa masoko
6:pembejeo kwa urahisi bila ukilitimba kama ilivyo sasa.
Hayo na mengine mengi ndio yanatuvuta wananchi na vijana CDM, Si kuchoka ccm pekee ingekuwa kuchokwa basi republican na democrat vya marekani visingekuwepo hadi leo kutokana na ukongwe wa zaidi ya karne kadhaa
 
hadi leohujajua sababu za watz kukichagua chadema? sababu ni hiz hapa
1.wananchi waliahidiwa maisha bora lakin imekuwa kinyume chake
Mkuu Ibra, ni kweli kabisa CCM ilichaguliwa kwa ahadi ya kuleta "Maisha bora kwa kila Mtanzania" na kiukweli haikutekeleza, hivyo 2015 hautaichagua kwa sababu hii!. Hii ndizo kura za "kuchokwa kwa CCM" ambazo Chadema itazivuma kama imeokota!. Lakini Jee, Chadema wamekuahidi nini kuhusu hayo maisha bora?, Jee tukishaipiga chini CCM kwa sababu ya hasira za kukosa maisha bora, wako watakao ichagua Chadema ili tuu kuiadhibu CCM, lakini watu makini zaidi, na hawawezi kuichagua Chadema kwa sababu tuu ya kuichoka CCM, bali wataichagua Chadema kwa sababu Chadema imesema itafanya A,B,C, D kuwapatia Watanzania maisha bora ambayo CCM wameshindwa!. Ndio maana nimewaambia viongozi wa Chadema, kusema tuu kuwa CCM ni mbaya, hakutoshi, wasema wao watafanya nini and how?, lazima sasa wabadilike, watupe sababu za kuichagua Chadema!.
4.kwa miaka 50 tangutupate uhuru chama kukaa madarakan kimeshindwa kutatua kero mbalimbali za wananchi kama vile ujenzi wa shule,nyumba za watumishi,zahanati,upatiakanaji wa dawa na watumishi. Sababu hizo zinatosha kukipigia kura
Na hapa pia nakuunga mkono, ni kweli CCM kimeshindwa kutatua kero ya umasikini, ujinga, maradhi, rushwa na ufisadi kwa Tanzania ndani ya miaka 50 iliyopita. Chadema kupitia M4C, is doing the right thing, kuzunguka nchi nzima kuwafungua macho Watanzania jinsi CCM ilivyoshindwa kutatua kero mbalimbali za Watanzania, kueleza tuu kuhusu kero ni one thing, sasa Chadema inatakiwa ibadilike, "not only doing the right thing, but also doing the things right" kwa kuwaeleza Watanzania yenyewe itafanya nini kinyume cha ilichofanya CCM ili kuwapa Watanzania sababu ya kuichagua Chadema!.

Ili Chadema wayaweze yote hayo, kwanza lazima ikubali kusikiliza kuhusu mapungufu yake, iyafanyie kazi na kuyatekeleza!. (Naombeni msiniulize mapungufu ya Chadema), viongozi wa Chadema wameisha ambiwa sana, imebaki kwanza kusikia, pili kutekeleza, 2015, ikulu ni yao!,

Kinyume cha hapo, CCM itaendelea, na Chadema waki miss hii golden opportunity ya 2015!, then Chadema kitakuwa ni chama cha kudumu cha upinzani, just imaginethe scanerio ya uchaguzi wa 2015, kama yule kamanda wangu wa CCM ndie ataongoza mapambano, Chadema bila kuja na credible reasons kwa nini kichaguliwe, CCM itapeta tena kwa kishindo, na nawaombeni sana tafadhali msirudi humu kulia lia na kususa as if hamkuambiwa!.

Pasco.
 
akili za magamba.....hivi bado unaamini kuwa cdm ni chama cha wachaga! ajabu.kama ni hivyo, ukichanganya wachaga wote walio ndani ya ccm na vyama vingine vyote, kisha ongeza wakristo wote, kisha watz wote, cdm itakuwa bado haijaingia madarakani? ........kumbuka..cdm ni chama kisicho na dini wala kabila.

Hapo ndio pazuri.
 
Wachagga wapo wengi sana zomba ngoja ni kumwagie list.

[1] Anthony G Mbassa huyu ni mchagga wa Biharamulo magharibi

[2] Prof Kulikoyela Kahigi huyu ni mchagga wa Bukombe Shinyanga

[3] Simon Peter Msigwa huyu ni mchagga wa Iringa Mjini

[4] Yohana Natse huyu ni mchagga wa Karatu

[5] Halima Mdee huyu ni mchagga wa Kawe Dar

[6] Zitto Z kabwe huyu ni mchagga wa Kigoma kaskazini

[7] John Shibuda huyu ni mchagga wa Maswa mashariki

[8] Joseph Mbilinyi huyu ni mchagga wa Mbeya mjini

[9] David Silinde huyu ni mchagga wa Mbozi magharibi Mbeya

[10] Mustafa Akonnay huyu ni mchagga wa Mbulu

[11] Meshack Opulukwa huyu ni mchagga wa Meatu Shinyanga

[12] Said Arf Amour huyu ni mchagga wa Mpanda Rukwa

[13] Vicent Kiboko Nyerere huyu ni mchagga wa Musoma mjini

[14] Ezekia Wenje huyu ni mchagga wa Nyamagana Mwanza

[15] Tundu Lissu huyu ni mchagga wa Singida Mashariki

[16] John Mnyika huyu ni mchagga wa Ubungo Dar

[17] Salvatory Machemuli huyu ni mchagga wa Ukerewe........

Mkuu zomba kama wachagga wameenea kila pembe ya Tanganyika ni kwanini wasishike dola haa ha ha ha wanchekesha!!!!!!.

Kwani hao walikuwa wapi mwaka 2005 na 2010? mbona Mbowe aligaragazwa vibaya sana, uchaguzi uliofatia akaona huyu Jakaya Mrisho Kikwete si size yake akamuomba Slaa amsaidie, nae akagaragazwa vibaya sana na hao vibaraka wenu si walikuwepo au umesahau?
 
34 Reactions
Reply
Back
Top Bottom