Kuchapisha mitihani UK ni kukubali kushindwa?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Mitihani ya kidato cha nne ya taifa inayoendelea imechapwa huko UK. Watahiniwa binafsi wakifanya mitihani tofauti na ile ya mashule. Yote haya ni katika jaribio linaloonekana kufanikiwa la kuzuia uvujaji wa mitihani. Je tumekiri kushindwa kuchapa mitihani yetu wenyewe kwa usalama? Ni kipi tunachoweza kukifanya vizuri sisi wenyewe na tukaona fahari?
 
Mkuu ni aibu kwa kweli, lakini pia imepunguza aibu kubwa zaidi ya mitihani kuibiwa na kuvuja kabla ya watahiniwa hawajaifanya!
Na kwa kuwa mpaka sasa haijavuja imeonesha uadilifu wa watanzania bado ni mdogo mno.
 
AIBU AIBU AIBU... Unajua MJJ, mambo mengine ni aibu sana, yaani hata kuyaongelea hadharani kama hivi!!
 
mitihani ya UK inasahihishwa marekani, kupunguza upendeleaji sioni baya kama aim ni kuwafanya wanafunzi wasome.

Yeah ni inavujaga sana hii mitihani ya bongo duh kumbe mpaka leo!!!!!!!!
 
Hili bado sio suluhisho la kudumu. Muda si mrefu wakati wa distribution itaibiwa tena tu. Labda tuwaite waingereza watusambazie na kusimamia katika mashule. KInachohitajika ni hatua ya haraka ya kubaini nini hasa chanzo cha kuibiwa mitihani hiyo na kuwachukulia hatua kali waliohusika. Hilo likitushinda basi tumekwisha.

Ndio kusema, tangu mitihani ianze kuvuja miaka kadhaa iliyopita, hakuna yeyote aliyenaswa kuhusika? Na hapa nazungumzia kiongozi. Mtiririko mzima wa utungaji, uchapishaji, usambazaji na usimamiaji una viongozi. Hawa wote lazima wawajibike maana wanatakiwa kujua nini kinachoendelea kwenye section zao. Sio kwa maneno bali kwa vitendo. Kama kiongozi mkuu wao hawezi kusema na akatenda, watu wa chini yake watacheka cheka na wataendeleza mambo yao maana wanajua hakuna jipya la kuwatisha.

Kuna kitu wanaita root cause analysis (msingi wa tatizo). Je ni njaa? wanaiba mitihani wauze wapate hela ya kula? Je ni kwa sababu ya msemo kila mtu hula kazini kwake kwa hiyo kama hawana nafasi kwenye madini au TRL, TANESCO, EPA au TICTS basi nafasi yao ni kwenye mitihani? Je hii ndio nafasi yao ya kujipatia kama ambavyo traffic hujipatia rushwa yake kwa madereva? Au ni kwamba tatizo linaanzia kwa wanafunzi kwamba hawaelewi au hawazingatii masomo ilhali wanataka kufaulu?

Chanzo cha tatizo kikishafahamika, basi viongozi wawe strict kutoa adhabu stahili kwa wakati na bila upendeleo. Na wananchi wajulishwe ili yeyote mwingine aliyekuwa anafikiria mkakati kama huo ajue kitakachomkuta. Tofauti na hapo ni yaleyale. Je huyo kiongozi yupo?
 
Mkuu ni aibu kwa kweli, lakini pia imepunguza aibu kubwa zaidi ya mitihani kuibiwa na kuvuja kabla ya watahiniwa hawajaifanya!
Na kwa kuwa mpaka sasa haijavuja imeonesha uadilifu wa watanzania bado ni mdogo mno.

Kweni za Rada siwaliibia huko huko nje? sasa subiri uone watanzania walivyo,
 
Du, sasa nitakufa njaa maana nimejenga kwa ajili ya mitihani.......
 
Its abot time tusdiscuss huu ujinga. yani tumeshakubali kwamba sisi ni wajinga hata mitihani hatuwezi kuisimamia.
lakini mbona bado invuja?
 
Mkuu wa kijiji...

Huko ndio kushindwa... period!!! Ni kama yale ya tarime, DC anataka kuzuia ng'ombe simply because ameshindwa kuboresha ulinzi wa watu na mali zao!!

ANOTHER INDICATOR OF OUR WEAKNESS AS A SOVEREIGN STATE
 
Halafu mimi nikisema yale ninayosemaga mnaniona niko chizi na sijipendi....

Na kwani mmeshasahau siku ile raisi alipokuwa anajibu maswali ya wananchi kuhusu ujenzi wa barabara mbalimbali....kila barabara aloitaja ujenzi wake ulikuwa ni msaada. Sasa kwenye hili la mitihani kuchapishwa UK nini cha kushangaza. Mbona wameanza zamani tu kuchapisha hii mitihani huko UK...

Haya ngoja ninyamaze maana hamkawii kuanza kuniita mzungu mweusi (whatever that is)
 
Mmesahau mbona na suit wananunua zilizo shonwa UK na USA mmesahau Spika 6 alikuwa anajinadi na Joho lile eti limeshonwa UK sisi hapa sijui tunaweza kipi? Inabidi jamaa wabadilike wakikumbuka kuwa kila kitu kinawezekana nyumbani basi tutapiga hatua tuanze na vitu vidogo vidogo hivi kwanza.
 
Kuna vitu viwili hapa:
1. Kuchapisha mitihani
2. Kuchapisha shahada za kupigia kura

Kwa tathmini ya haraka haraka niliyoifanya kwa wachangiaji humu JF, wengi walipinga kuchapisha shahada za kupigia kura hapa nchini katika hoja iliyowekwa HAPA . Mimi ninahoji, sababu zipi za msingi zinazotofautisha shahada na mitihani? Sababu zipi za msingi zinazofanana kuhalalisha mitihani/shahada kuchapishwa ndani/nje ya nchi? Tuweke hoja zetu humu, labda tutapata uelekeo wa kuunga mkono au kupinga.
 
Mzee mwanakijiji,
Mkuu sio kukubali kushindwa ila Ndivyo Tulivyo - Ulimbukeni, ili nasi tuonekane tuna uzungu fulani..
 
Sisi tumebaki kupiga majungu tu na kuongea ni nani amesema vile mara vile eti Leo mwanakijiji amesema hivi oh mara hivi.. It is really sucks man kama hata mamlaka zetu bado ni dhaifu kiasi kama hivi leo hiii kila kitu tunaiga mithili ya watu ambao akili zetu zimedumaa.
 
Naipenda sana ile kauli ya ndugu yangu/Poti Julius ya 'Miafrika Ndivyo Tulivyo(MNT)'..Juzi hapa serikali ya Tanzania imetangaza kwamba inakusudia kuchapisha shahada za uchaguzi mkuu wa mwakani yenyewe(zitachapishwa Tanzania) watu kibao wamepinga kwa madai kwamba kuna wizi/ujanja utafanyika so zichapishwe nje ya nchi..Hii inaonesha ni jinsi gani sisi waTanznia tusivyojiamini.Tunataka kila kitu tufanyiwe na wazungu tuuu.Nina uhakika hata mitihani ikiachapishwa Tanzania na ukatokea wizi wa hiyo mitihani lawama zote zitaiendea serikali..Nakumbuka mwaka 1998 baada ya mitihani ya kidato cha nne kuvuja ilibidi mitihani ya marudio ikachapishwe nje ya nchi(Uingereza kama sikosei)...Binafsi naona hapa kuna mambo mawili(02),kwanza waTanzania hatujiamini,pili baadhi ya watanzania wanaopewa dhamana ya kushughulikia uchapishaji na uhifadhi wa mitihani wanakosa uaminifu(hasa wa kutunza nyaraka za serikali) hali inayopelekea kuvuja kwa mara kwa mara kwa mitihani..Cha msingi ni kutafuta dawa ya ugonjwa wa UTEGEMEZI kwa wazungu ambao umesambaa na kukomaa ndani ya Bongo za Watanzania,tujiamini watanzania la sivyo tutakuwa wategemezi daima
 
Back
Top Bottom