The Businessman
JF-Expert Member
- Jan 9, 2014
- 7,396
- 9,264
Wasalaam,
Bila shaka wapo wanaoelewa au kusikia mtu amechanjiwa na anaweza kuona yale yasioonekana kwa macho ya kawaida.
Mwaka 1982 nilipokuwa na miaka 11 baba yake bibi ambaye mimi namuita bamkubwa alinipeleka porini ambapo aliweza kunionyesha mti ujulikanao kama Mlami kwa kilugha chetu kibena na kuniambia huu mti ukichanjiwa yaani uchanganye kwenye damu yako kisha kunuia unaweza ukawa unaona mambo yanayotendeka kishirikina na mchawi anakuogopa.
Nikamwambia mtani nichanje na mimi akanichanja chini ya nyao za miguu akapyatila magome yake akanipaka na kuanza kunuia kazi ikawa imeisha.
Toka hapo kweli nimekuwa nashuhudia mambo ya ajabu ajabu nilishawahi kukutana na watu ambao tulikwisha wazika siku nyingi ila chini wana kwato si binadamu wa kawaida. Migomba ikizikwa na kuzaniwa na watu hiyo ni kawaida.
Kuna matukio nimeyaona hivi karibuni, tukio la kwanza ijumaa nilienda kumuona bint yangu ambaye anasoma kidato cha pili shule moja iliyopo pale Idodi na bahati nzuri nilikuta ndio wanakula chakula cha mchana kilichonistaajabisha ni kumuona mwanangu anakula Majivu ambao ni Ugali na Nyasi ambao ndio mboga nikaangalia na wanafunzi wengine nao ni vile vile nikaenda mpaka jikoni kuangalia wanapakuliwa nini napo nikakuta ni Majivu na Nyasi kiukweli nilikosa nguvu nikamuaga mwanangu nikaondoka na mwingi wa mawazo.
Mpaka sasa shule ikifunga nina mpango kumuhamisha nikae naye mwenyewe asome day.
Tukio la pili ni la leo ambapo niliingia duka moja hapa miyomboni ili kupata mahitaji ya nyumbani, ghafla aliingia mama mmoja anataka Sukari, muuzaji akaanza kumpimia, nilichokiona ni Mchanga badala ya Sukari ndicho alichokuwa anapimiwa yule mama, nilitaka kumwambia ila nikasita nikaamua kuondoka.
Sina raha, Sina amani, ninajihisi sio binadamu wa kawaida kwa haya ninaoyaona. Nimejaribu kila hali niweze kuacha kuyaona haya mambo lakini imeshindikana.
Kisaikolojia siko sawa.