Kuchanjiwa kumeniharibu kisaikolojia

Kuchanjiwa kumeniharibu kisaikolojia

malizia tu bhanaaa BABANUSA....................
Ha ha ha ha ha ................

siku hizi naskia kuna duka la mkongwe kwa sasa ndo linavuma kweli nalo linaitwa kwa KAUNDAMA

Mnatuogopesha sana..nimepita sana ukanda wa iringa lkn nikiwa Mpore muda wrote hata vimwana sikuwahi kutamani.
 
Maajabu sana haya,pole. Vipi ukilog in JF?Unaikuta jf kawaida au inabadilikaga na kuwa fb?

Shauri yako ww chokoza tu asije akakuambia anakuona upo uchi?
 
Mkuu hukuwahi kuvuta bangi au madawa ya kulevya? maana naona inafanana sana na madhara
ya uvutaji wa madawa ya kulevya.

Nasema hivyo kwa sababu.
kuna jirani yangu mtoto wake wa kiume
alianza story za ajabu,anasema kuna
watu wanakuja wanataka kumuua,anasema anaona watu lkn cc hatuwaoni.
akasema ni majirani,wanataka asiwe mrithi.

Baada ya kumpeleka kwenye maombi,tuliamua
kumpeleka amana kitengo cha waliochanganyikiwa.
wale jamaa walipomhoji na kumpa dawa
akawa fresh lkn walimsihi asiendelee na vilevi
hivyo kwani ni hatari.

Na wewe umeshauriwa uende kwenye maombi
lkn kama unatumia bangi au madawa yaache kwanza
unaweza ukawa mzima.

Angalia hata AVATAR yako imejaa kipenda roho chako.
hapo hakuna uchawi wala kuchanjiwa.
 
Duuh hilo limeshakuw ni tatzo kwako broo.....

Kikubwa ww umwombe Mungu tu akuondolee hayo macho..!
 
Je afya za wanafunzi hapo zikoje? Usije ukawa wewe ni mwalimu uliyefukuzwa sasa unaichafua shule.
 
Wasalaam,

Bila shaka wapo wanaoelewa au kusikia mtu amechanjiwa na anaweza kuona yale yasioonekana kwa macho ya kawaida.

Mwaka 1982 nilipokuwa na miaka 11 baba yake bibi ambaye mimi namuita bamkubwa alinipeleka porini ambapo aliweza kunionyesha mti ujulikanao kama Mlami kwa kilugha chetu kibena na kuniambia huu mti ukichanjiwa yaani uchanganye kwenye damu yako kisha kunuia unaweza ukawa unaona mambo yanayotendeka kishirikina na mchawi anakuogopa.

Nikamwambia mtani nichanje na mimi akanichanja chini ya nyao za miguu akapyatila magome yake akanipaka na kuanza kunuia kazi ikawa imeisha.

Toka hapo kweli nimekuwa nashuhudia mambo ya ajabu ajabu nilishawahi kukutana na watu ambao tulikwisha wazika siku nyingi ila chini wana kwato si binadamu wa kawaida. Migomba ikizikwa na kuzaniwa na watu hiyo ni kawaida.

Kuna matukio nimeyaona hivi karibuni, tukio la kwanza ijumaa nilienda kumuona bint yangu ambaye anasoma kidato cha pili shule moja iliyopo pale Idodi na bahati nzuri nilikuta ndio wanakula chakula cha mchana kilichonistaajabisha ni kumuona mwanangu anakula Majivu ambao ni Ugali na Nyasi ambao ndio mboga nikaangalia na wanafunzi wengine nao ni vile vile nikaenda mpaka jikoni kuangalia wanapakuliwa nini napo nikakuta ni Majivu na Nyasi kiukweli nilikosa nguvu nikamuaga mwanangu nikaondoka na mwingi wa mawazo.

Mpaka sasa shule ikifunga nina mpango kumuhamisha nikae naye mwenyewe asome day.

Tukio la pili ni la leo ambapo niliingia duka moja hapa miyomboni ili kupata mahitaji ya nyumbani, ghafla aliingia mama mmoja anataka Sukari, muuzaji akaanza kumpimia, nilichokiona ni Mchanga badala ya Sukari ndicho alichokuwa anapimiwa yule mama, nilitaka kumwambia ila nikasita nikaamua kuondoka.

Sina raha, Sina amani, ninajihisi sio binadamu wa kawaida kwa haya ninaoyaona. Nimejaribu kila hali niweze kuacha kuyaona haya mambo lakini imeshindikana.

Kisaikolojia siko sawa.

Uliikubali hiyo hali ipokee, bora tu ufanye yaliyo sawa na usimchukize Mungu, unachokiona ibakie siri yako, hizo nguvu ulizotunukiwa zitabakia kuwa nguvu zako, zitumie vizuri, fanya yaliyo mema, kwani katika hii dunia kuna watu wengi sana wamejaliwa vipawa na uwezo tofauti na Mungu, si wa kuchanjiwa, Wazungu wenyewe wanaamini hivi vitu vipo, mfano mdogo ni movie ya Merlin, wengine wanazaliwa navyo, wengine ndio kama hivyo ni vya kuchanjia.

Wanasema mtoto anapokuwa mchanga au mdogo anaona mambo mengi sana ambayo ni ngumu kwa watu wazima kuyaona, na kuna mambo mengi sana ya ajabu ambayo yanendelea katika hii dunia, lakini kutokana na matendo mengi ya hovyo yaliyokithiri ni ngumu sana sana kuyaona, yahitaji mtu mwema haswa na anayemcha Mungu, unapoona vitu vya hovyo usiwazalilishe watu wewe achana nao na ikiwezekana walinde na kuwakinga familia yako na watu wako wa karibu.
 
duh!, mimi kuna mzee alikuwa mwendapanandi alinichanjia dawa sijui ya kitu ila tangu hapo mpaka sasa hakuna demu ninayemtaka akakataa mpaka wake za watu
Ikitokea ukanitokea ukanipata jiandae kuwa kilema au kufa kabisa
 
Kweli kazi unayo , kuondokana na hilo tatizo unahitaji maombi,ni kumrudia mungu ili uwe kiumbe chake tena , kwa sasa uko kwenye milki nyingine tofauti kabisa
 
Wala sio tatizo ukijieka sawa na wala hauko mbal na Mungu ni wew kufanya vitu ambavyo vyampendeza mungu hua mara nyingi mtu unachanjiwa kwa usalama wake peke ake nakuambia from experience coz ata mi nilichanjiwa but nikiwa mdogo sana sikua najitambua its a gift use it........
 
Mbena,mhehe,mkinga,msafwa makabila ya kusini kwa ushirikina sitaki kabisa mwanaume wa huko....
 
Kwa kweli hyo ni bahati sana maana huwezi lishwa vitu vya ajabu ajabu na huwezi chunguliwa ovyo ovyo.kikubwa usiwe na www ni sehemu ya ushirikina
 
Wasalaam,

Bila shaka wapo wanaoelewa au kusikia mtu amechanjiwa na anaweza kuona yale yasioonekana kwa macho ya kawaida.

Mwaka 1982 nilipokuwa na miaka 11 baba yake bibi ambaye mimi namuita bamkubwa alinipeleka porini ambapo aliweza kunionyesha mti ujulikanao kama Mlami kwa kilugha chetu kibena na kuniambia huu mti ukichanjiwa yaani uchanganye kwenye damu yako kisha kunuia unaweza ukawa unaona mambo yanayotendeka kishirikina na mchawi anakuogopa.

Nikamwambia mtani nichanje na mimi akanichanja chini ya nyao za miguu akapyatila magome yake akanipaka na kuanza kunuia kazi ikawa imeisha.

Toka hapo kweli nimekuwa nashuhudia mambo ya ajabu ajabu nilishawahi kukutana na watu ambao tulikwisha wazika siku nyingi ila chini wana kwato si binadamu wa kawaida. Migomba ikizikwa na kuzaniwa na watu hiyo ni kawaida.

Kuna matukio nimeyaona hivi karibuni, tukio la kwanza ijumaa nilienda kumuona bint yangu ambaye anasoma kidato cha pili shule moja iliyopo pale Idodi na bahati nzuri nilikuta ndio wanakula chakula cha mchana kilichonistaajabisha ni kumuona mwanangu anakula Majivu ambao ni Ugali na Nyasi ambao ndio mboga nikaangalia na wanafunzi wengine nao ni vile vile nikaenda mpaka jikoni kuangalia wanapakuliwa nini napo nikakuta ni Majivu na Nyasi kiukweli nilikosa nguvu nikamuaga mwanangu nikaondoka na mwingi wa mawazo.

Mpaka sasa shule ikifunga nina mpango kumuhamisha nikae naye mwenyewe asome day.

Tukio la pili ni la leo ambapo niliingia duka moja hapa miyomboni ili kupata mahitaji ya nyumbani, ghafla aliingia mama mmoja anataka Sukari, muuzaji akaanza kumpimia, nilichokiona ni Mchanga badala ya Sukari ndicho alichokuwa anapimiwa yule mama, nilitaka kumwambia ila nikasita nikaamua kuondoka.

Sina raha, Sina amani, ninajihisi sio binadamu wa kawaida kwa haya ninaoyaona. Nimejaribu kila hali niweze kuacha kuyaona haya mambo lakini imeshindikana.

Kisaikolojia siko sawa.
Bila shaka upo Iringa ntakutafuta ukanioneshe uo mti "!au nitumie contact zako we ujuz wako n muhim
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom