Kuchaguliwa kwa Rais mteule WIliam Ruto kuna Umuhimu au mchango gani kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki?

Mar 15, 2018
26
36
Tume ya uchaguzi nchini Kenya 16-08-2022 ilitangaza matokeo ya Urais ambapo Wiliam Ruto aliteuliwa kuwa Rais mteule wa awamu ya Tano wa taifa la Kenya , kutokana na kuteuliwa kwake kuwa Rais, nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki tunamategemeo mengi juu

Kenya ni nchi muhimu panapohusika biashara ya kanda, kwa sababu ya kutumiwa kwa bandari yake ya Mombasa na wengi wa majirani zake. Kwa mfano Uganda isiyo na bahari inategemea kwa kiwango kikubwa bandari ya Mombasa kwa usafirishaji wa bidhaa inazosafirisha kwenda nje na zile inazoagiza kutoka ng'ambo. Kenya ni mshirika mkubwa wa biashara wa Uganda na Wagombea wote wawili wakuu; Raila ana Ruto walikwenda Kampala kwa nyakati tafauti kuonana na Rais Museveni, tukio linaloashiria kila mmoja anatafuta kuungwa mkono na kiongozi huyo jirani na mkongwe.

Rwanda ni nchi nyingine ambayo inategemea kwa upana mkubwa uagizaji bidhaa kutoka Kenya. Kwa mujibu wa takwimu za 2019, Rwanda iliagiza bidhaa za thamani za dola milioni 278.45 za Marekani kutoka Kenya.

Burundi mwanachama mwengine wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ilisaini mkataba wa kuimarisha ushirikiano wa biashara na maendeleo Kenyatta. Tangu ilipojiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki Aprili 2022, Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo (DRC) imeonesha ishara ya kufungua zaidi milango ya kiuchumi kwa wawekezaji.

Lakini kuna changamoto ambazo zilitokea kwa serikali ya Kenya 2021 ambapo Kenya ilipiga marufuku mara moja ununuzi wa mahindi kutoka mataifa jirani ya Tanzania na Uganda. Mamlaka ya ushuru nchini Kenya KRA, walisitisha baada ya uchunguzi kubaini kwamba mahindi kutoka mataifa hayo mawili sio salama kwa matumizi ya chakula cha binadamu.

Pia ikumbukwe Mataifa ya Kenya na Uganda yamewahi kuzozania kisiwa kidogo katika Ziwa Victoria kwa jina Migingo. Raia wengi wa Kenya walikuwa wamelalama kuhusu kunyanyaswa na maafisa wa polisi na jeshi wa Uganda na baadaye ikaibuka kwamba Uganda ilikuwa ikidai kukimiliki kisiwa hicho.

Katika miitandao ya kijamii wadau wengi wamkekuwa wakionesha kuunga mkono matokeo ya uchaguzi lakini kusema kweli wengi wetu hatujui sera ambazo atakuja nazo Rais huyu mpya kuhusu jumuiya Kutokana na uwepo wa migogoro mingi katika jumuiya ya Afrika mashairi ikiwemo migogoro ya mipaka , biashara , ajira, janga la njaa pia kuwepo kwa sarafu moja ya Afrika Mashariki.

Mategemeo ya jumuiya ya Afrika mashariki kuhusu matokeo ya Urais nchini Kenya ni kuundwa kwa sarafu moja ya Afrika mashariki, kutatuliwa kwa mgogoro wa Kongo DRC, kufunguliwa kwa biashara ya pamoja kwa wnachama wa jumuiya, kusuluwisha migogoro ya mipaka na vita vya wenyewe kwa wenyewe, kufunguliwa kwa soko la ajira kubwa kutokana Kenya kuwa Taifa kubwa lenye uchumi mkubwa Afrika Mashariki.
 
Kikubwa tuna wasiwasj na biashara ya nafaka kama Ruto ataruhusu tuendelee kufanya biashara au la Hilo tu mengineni ya kawaida.
 
Their country comes first, no matter what. Jumuiya? Jumuiya my foot😂. Hivi na hii nayo ni jumuiya?
 
Kikubwa tuna wasiwasj na biashara ya nafaka kama Ruto ataruhusu tuendelee kufanya biashara au la Hilo tuu mengineni ya kawaida
Kwakweli, nikikumbuka hata zile figisu za nafaka/mahindi kutoingia Kenya wakati ule inasemekana ilikuwa na mkono wake.

Tuombe Mungu, Watu Hubadilika.
 
Back
Top Bottom