Kubenea... Sali sala yako ya mwisho!

  • Thread starter Mzee Mwanakijiji
  • Start date

Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,872
Likes
8,022
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,872 8,022 280
Kama vile vitisho vya mwanzo havikutosha; na kama vile kupigwa na mijeba hakukunoga; na kama kumwagiwa tindikali hakukuonesha kilele cha umafia wa baadhi ya watu muda mfupi uliopita Mhariri Mtendaji wa MwanaHalisi Bw. Saed Kubenea amejikuta tena kwenye kona ya wale "watishao"!

Habari za uhakika na zilizothibitishwa zinasema kuwa Usiku huu (tanzania) Bw. Kubenea amejikuta amepigiwa tena ile "simu ya kifo" na mtu asiyejulikana ambaye namba yake ya simu inaonesha "private". Mtu huyo ambaye hakujitambulisha alitaka kujua kama ni Kubenea anayeandika habari za zisizo nzuri za mmoja wa wanasiasa maarufu ambao wameguswa na Kashfa ya Richmond hivi karibuni.

Bw. Kubenea alipokiri kuwa yeye ni mwandishi wa habari zinazodaiwa mpiga simu alimuambia "sali sala zako za mwisho".

Hadi dakika hii tunavyozungumza juhudi za kuviarifu vyombo vya usalama zinaendelea kwa kasi ili hatua zianze kufuatiliwa hasa baada ya kuzingatia kuwa kupuuzia vitisho kama hivi ni kukaribisha vitendo vya kihuni na vya kihalifu.

KLHN inasimama pamoja na Bw. Kubenea pamoja na waandishi wengine wote ambao wanajikuta kwenye matishio ya kuwafanya washindwe kufanya kazi zao za uhandishi kwa uhuru na kwa uwazi. Endapo jambo lolote litamtokea Bw. Kubenea wakati huu wa msuguano wa mawazo na mgongano wa kifikra na hasa kama ni kitendo cha kihalifu lawama za kwanza na kuwajibika kwa kwanza kutaendea vyombo vyetu vya usalama kwa kushindwa ku "trace" "private" calls kwani ni hatari hata kwa usalama wa nchi!!

Tunatoa wito kwa vyombo vya usalama kuhakikisha usalama wa watu wote hasa wale ambao wana sababu ya kuamini kuwa madhara yanapangwa dhidi yao.
 
M

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2007
Messages
5,194
Likes
17
Points
0
M

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2007
5,194 17 0

Mimi natoa wito binafsi kwa waziri mkuu Pinda kumlinda Kubenea na kumhakikishia usalama wake!
 
Saharavoice

Saharavoice

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2007
Messages
2,707
Likes
267
Points
180
Saharavoice

Saharavoice

JF-Expert Member
Joined Aug 30, 2007
2,707 267 180
Nampa pole Bw. Kubenea, Muhimu ni kwa vyombo vya usalama kutafuta namna ya kumlinda na kuweka mtego wa kuwakamata hawa jamaa. Ni wazi kwamba wanatumwa kufanya hivyo na Mafisadi.

Kwa TZ yetu kutrace namba ya simu ni ngumu sana, maana Laini za simu zinauzwa kama karanga. mtu ananunua laini anakutishia akimaliza anaitupa.
 
Liz Senior

Liz Senior

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2007
Messages
485
Likes
0
Points
33
Liz Senior

Liz Senior

JF-Expert Member
Joined Apr 19, 2007
485 0 33
Ni wakati wa bunge letu kuhakikisha linapigania haki za vyombo vya habari na wanahabari kwa ujumla. Wakati wa kuchangia hoja zilizohitimisha bunge hivi majuzi walimshukuru sana Kubenea na wenzie kwa kazi nzuri waliyoifanya...sasa tunataka vitendo vinavyoendana na shukrani hizo. Taifa lilisilo na wanaosema na kufichua ukweli ni sawa na chaka lenye giza nene
 
zomba

zomba

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2007
Messages
17,081
Likes
70
Points
0
zomba

zomba

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2007
17,081 70 0
Bwana Saidi kubenea, nakuombea kwa Mwenyeezi Mungu akuepushe na mabaya yeyote wanaokudhamiria wabaya wako. Mwenyeezi Mungu atakuvuwa kwenye hili na lingine na atakupa umri mrefu inshaAllah.

Na namuomba Mwenyeezi Mungu akubainishie wote waliokukalia kwa ubaya. Amin.
 
Dua

Dua

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2006
Messages
2,481
Likes
28
Points
135
Dua

Dua

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2006
2,481 28 135
Watawaua WTZ wote halafu wabaki peke yao ndio watakapokuwa na usingizi mnono kwenye nchi ya kusadikika ambako hawalipi kodi wala kufanya kazi.
 
M

Mafuchila

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2006
Messages
752
Likes
22
Points
35
M

Mafuchila

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2006
752 22 35
Serikali ina wajibu wa kumlinda Kubenea sio tu kwa kuwa ni mwandishi wa habari, lakini kwa kuwa ni raia wa Tanzania na anayefanya shughuri zake kihalali kabisa, hivyo kumtishia maisha yake ni uhalifu ambao serikali inapaswa kuujibu kikamilifu.
 
Madela Wa- Madilu

Madela Wa- Madilu

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2007
Messages
3,073
Likes
56
Points
135
Madela Wa- Madilu

Madela Wa- Madilu

JF-Expert Member
Joined Mar 24, 2007
3,073 56 135
Rafiki zake Lowassa wote macho mekundu kama ya kindi kwa kuvuta bangi ili kujipooza na kujisahaulisha uuaji wao.
Wanao mzunguka Lowassa wengi hawaoni taabu kuua mtu yeyote hata kama ni mama yao mzazi.
Hata maaskofu wanao mzunguka hawaoni taabu kuua ili mradi hawazikosi sadaka na zaka za Lowassa, nasikia siku zoteEL huangusha pochi nene ya kifisadi kwenye matoleo na michango.

Tatizo la kutishia wajenzi wa uwazi ni moja.
Mtishaji husaidia kusambaza taarifa aitoazo mjenzi wa uwazi.

Ni sawa na kufagia zizi la mbuzi na kutupa taka kwenye shamba la mahindi ukitegemea mahindi yatapa tetenasi, unakua umechemsha ile mbaya, mavuno mara dufu.

Pole sana Mkuu Kubenea
 
M

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2007
Messages
5,194
Likes
17
Points
0
M

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2007
5,194 17 0
Rafiki zake Lowassa wote macho mekundu kama ya kindi kwa kuvuta bangi ili kujipooza na kujisahaulisha uuaji wao.
Wanao mzunguka Lowassa wengi hawaoni taabu kuua mtu yeyote hata kama ni mama yao mzazi.
Hata maaskofu wanao mzunguka hawaoni taabu kuua ili hawazikosi mradi sadaka na zaka za Lowassa, nasikia siku zote huangusha pochi nene ya kifisadi kwenye michango.

Tatizo la kutishia wajenzi wa uwazi ni moja.
Mtishaji husaidia kusambaza taarifa aitoazo mjenzi wa uwazi.

Ni sawa na kufagia zizi la mbuzi na kutupa taka kwenye shamba la mahindi ukitegemea mahindi yatapa tetenasi, unakua umechemsha ile mbaya mavuno mara dufu.
Hii ya kutupa taka kwenye shamba la mahindi kutegemea kuwa mahindi yatapata is my quote of the day!
 
BabaH

BabaH

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2008
Messages
703
Likes
7
Points
35
BabaH

BabaH

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2008
703 7 35
Serikali ina wajibu wa kumlinda Kubenea sio tu kwa kuwa ni mwandishi wa habari, lakini kwa kuwa ni raia wa Tanzania na anayefanya shughuri zake kihalali kabisa, hivyo kumtishia maisha yake ni uhalifu ambao serikali inapaswa kuujibu kikamilifu.
Nakushukuru sana kwa kuyaona haya
Ila Ulinzi wetu chini ya Mwema ni kama ndoto, Mimi niliwambia kuwa sisi hatuna Polisi wala Jeshi, basi tu nasi tuonenekane tumo, watu wanaacha kufuatilia haya mambo wanaenda kuwashika wana JF na kutangazia uma mambo ya uongo, Saidi mwema na Mapolisi wake wote hawana maadili ya kazi na ndo tatizo, ila Mwenyezi Mungu atatulinda tu bila wasi wasi.

Pole sana mpiganaji wetu, tupo nawe kila mahali ndugu
 
Idimi

Idimi

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2007
Messages
11,356
Likes
3,081
Points
280
Idimi

Idimi

JF-Expert Member
Joined Mar 18, 2007
11,356 3,081 280
Watawaua WTZ wote halafu wabaki peke yao ndio watakapokuwa na usingizi mnono kwenye nchi ya kusadikika ambako hawalipi kodi wala kufanya kazi.
Na kwa taarifa yao hiyo nchi yenye mfumo huo haipo kabisa!
Ukisha 'tamper' na damu ya mtu ni vigumu sana kufuta damu hiyo mikononi mwako, huwezi kukaa kwa amani kamwe!
Mungu mlinde Kubenea
 
Nemesis

Nemesis

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2008
Messages
4,142
Likes
1,565
Points
280
Nemesis

Nemesis

JF-Expert Member
Joined Feb 13, 2008
4,142 1,565 280
Kwa TZ yetu kutrace namba ya simu ni ngumu sana, maana Laini za simu zinauzwa kama karanga. mtu ananunua laini anakutishia akimaliza anaitupa.
Ni kweli 'line' za simu zinauzwa kama karanga, lakini hata huduma ya kuficha namba? (private/hide number) kama huduma hii inatolewa kienyeji basi kazi tunayo.

hata hivyo tungekuwa na intelligency nzuri, mtu anakamatwa tu, lakini yale yale (refer thread ya usala wa taifa).

polisi wakiwa serious wahalifu hawa watakamatwa.
 
Moshe Dayan

Moshe Dayan

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2008
Messages
812
Likes
91
Points
45
Moshe Dayan

Moshe Dayan

JF-Expert Member
Joined Feb 10, 2008
812 91 45
pole mkuu kubenea, ni mapitio ya maisha.bongo sina uhakika network providers kama wana state of the art technology, wenzao nje kama vyombo vya usalama vinataka kumkamata mtu anayetisha watu kwa simu, wanamkamata kirahisi.

Kila mobile phone ina unique serial number just as chasis number ya gari.kinachofanyika, mtu hata aweke private number au hata abadilishe line, still inakua rahisi kum-trace a long as wanajua exact muda simu ilipopigwa.na kweye baadhi ya nchi ni must network provider afikie this standard ili ku-avoid mikosi kama hii inayomkumba kubenea na pia ni suala la security in general.sasa sjajua kama network providers tz wana vifaa vya ku-track hizo anon calls.

Na wakishajua ni simu gani ilipiga basi inakua rahisi kumfatilia huyo mtu hata akibadilisha line na hapo ndipo wataweza kusikiliza anaongea na kina nani, na wapi wanaweza kumkamata.
 
Icadon

Icadon

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2007
Messages
3,589
Likes
29
Points
0
Icadon

Icadon

JF-Expert Member
Joined Mar 21, 2007
3,589 29 0

Kula tano mzee,

(International Mobile Equipment Identifier)

A 15-digit number (composed of four parts) that uniquely identifies an individual wireless device. The IMEI is automatically transmitted by the phone when the network asks for it. A network operator might request the IMEI to determine if a device is in disrepair, stolen or to gather statistics on fraud or faults.

IMEI is most commonly used in GSM and WCDMA (UMTS) phones. CDMA phones use a similar type of number called an ESN.

Ila kwenye hili ni pagumu sana kumtrace huyo mtu kama akiwa anatumia mtandao fulani .......
 
Moshe Dayan

Moshe Dayan

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2008
Messages
812
Likes
91
Points
45
Moshe Dayan

Moshe Dayan

JF-Expert Member
Joined Feb 10, 2008
812 91 45
asante kwa tano, hapo mtandao wowote una namna yake ya ku-respond kuonyesha hiyo namba.any digital phone is traceable.
 
Moshe Dayan

Moshe Dayan

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2008
Messages
812
Likes
91
Points
45
Moshe Dayan

Moshe Dayan

JF-Expert Member
Joined Feb 10, 2008
812 91 45
tehe tehe tehe, mkuu wa kazi, nimekupata vilivyo, tehe tehe!! sorry, i overlooked!
 
Majita

Majita

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2008
Messages
606
Likes
94
Points
45
Majita

Majita

JF-Expert Member
Joined Jan 13, 2008
606 94 45
Ningekuwa mimi ni POLISI,ningeangalia hili jambo kwa jicho la pili.Yani Ninge-suspect maadui zaidi kuliko tunaowahisi.Kwa mtazamo wangu,mimi nahisi kuwa kubenea ana maadui wengi.Sasa kuna mmoja sasa anajifanya ni rafiki yake au ni adui wa chini chini.Baada ya kubenea kupatwa na dhahama ile ya mwanzo sasa yeye huyo adui wa siri anataka kutumia hiyo nafasi ili jamii iseme kuwa labda aliyepiga hiyo simu ya vitisho ni huyu adui tunae mfikiria.

Tutake tusitake,huyo mpiga simu lazima anapitia hapa JF kusoma news.Huyo wa mwanzo aliyemwagia tindikali nae nahisi anapitia hapa JF kusoma news na ktk hali ya Ujambazi wa kawaida LAZIMA anaogopa ama anahisi kuwa jamii tayari inamjua,so hawezi tena kuendelea kupiga simu za vitiso.

Ila kama ni jambazi aliyekubuhu basi huyo mmwaga tindikali ndo mpiga simu,kitu ambacho sitarajii sana kwa ujasiri wa waTZ.Namshauri kubenea kukaa chini na kuanza kuorodhesha ANAO WAHISI NI MAADUI ama wana TOFAUTI zozote.Namba moja awe ni yule anaemhisi kwa asilimia ndogo zaidi na wa mwisho Awe adui wake wa wazi ambae kila mtu anamjua na ambae obvious hawezi kumpigia simu ya vitisho.

Tatizo la Polisi wetu wa bongo ni blah blah nyingi.Yani utafikiri walinzi wa sungusungu vile.Wao kukurupuka tu.Ukitaka kuamini wewe fuatilia wanavyomhoji mtu kukiwa na tukio serious.
Yani wako shallow kweli.
© Ningesema siwapendi ilaisemi tena
 
F

FDR Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2007
Messages
249
Likes
4
Points
0
F

FDR Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2007
249 4 0
Ktk dunia hii mambo ya mtu kuamini kuwa yeye ana haki ya kuchukua uhai wa mwenziwe tena kwa simu haivumiliki lakini kibaya zaidi sasa wanachofanya ni kumpa ugonjwa usiotibika rohoni, huu ni ukimwi interms of kihoro.

Hawa ndio watesi wake,sasa jamii ibebe dhamana ya uhai wa Saed Kubenea,si masihara hawa watu si wajinga wanajua mipango yao.

Mungu akupe nguvu ktk harakati zako na maisha ya kila siku,kifo ni ahadi toka kwa maulana na ni yeye tu mjuaji wa hilo,pole sana kwa kuishi kwa kihoro ambalo kwakweli ni tatizo kubwa kuliko kifo chenyewe.
 
Forum statistics

Threads 1,235,258
Members 474,471
Posts 29,215,556