Kubenea... Sali sala yako ya mwisho!

Hivi huyu mwandishi anachoogopa nini haswa ikiwa Tanzania hakuna mtu aliyeuawa na viongozi wa serikali... Sii ndio waandishi hawa wanavyokuwa wakisema!... leo imekuwa wao inakuwaje tuwaamini wao?
 
Haya mambo pia alijaribu kuyagusia Mkuchika pale alivyoongea na vyombo vya habari na kutishia kuwa serikali itarudi kule kwa Mkapa kwa kujaribu kudhibiti uhuru wa vyombo vya habari.

Kama wananchi hawajisikii huru katika nchi yao wenyewe basi serikali kuu inabidi iwajibishwe kwa hilo. Haiwezekani siku moja tu baada ya Kubenea kuleta story ya Deep Green ndio aanze kupata vitisho hivi.

Hii Deep Green mbona inalindwa hivi? Mbona Kikwete amekuwa kimya kabisa katika suala hili? lazima kuna kitu hapa na ndio maana namuuliza PM Pinda ahakikishe ulinzi wa maisha ya Kubenea maana kuna mambo yako karibu kutoka hapa na watanzania watajua tu ni nini serikali yao inafanya kwa niaba yao.

Lakini, si alipotembelewa pale hospitali Muhimbili na kupewa pole, si alipewa usia pia? Maneno kama...."Kuweni waangalifu mnapoandika habari za watu......", ama maneno yanayofanana na hayo. Hii ni kumbukumbu yangu kama nilivyosoma maandishi ya gazeti lililoandika habari hiyo.

Maneno hayo ni mazito yanapotolewa na mtu mzito kama huyo. Mimi nayachukulia kuwa ni maneno ya kutoa onyo zaidi kuliko tahadhari.
 
Serikali ya SISIEMU inasumbuka kujaribu kunyamazisha sauti za ukombozi.
Watu wamechoka kudanganywa kila siku.
Zaidi, watu wamechoka kuibiwa na kubebeshwa mzigo ya gharama za wizi wa viongozi wetu.
Sauti zao za kudai haki( Sheria) ni sauti za mapambano ya kupinga uovu na uonezi wa watawala kutoka kwa wanyonge.
Sauti zinazo dai haki hazitanyamaza hata siku moja kwa sababu kila dakika inayo pita kundi jipya la vijana wanaopata sababu za kudai haki Tanzania linaibuka.

Ili mradi mpambano huu umeanza sioni wa kuuzuia.

Serikali ya SISIEMU imetumia karibu silaha au mbinu zote kunyamazisha sauti za kudai haki, Silaha nyingi zimeshindwa na chache bado zinafanya kazi, ziko mbioni kushindwa.

SISIEMU kwanza ilitumia silaha yake ya kusema uongo silaha hiyo imefyekwa wimo wake na JF.JF kila kitu inaandikwa kwa uwazi upana na urefu wake.

SISIEMU wametumia silaha ya kukaa kimya, JF kwa mara nyingine ikatumia nafasi ya Technolojia ya habari kuwapaka upupu viongozi wa serikali ya SISIEMU mpaka wameanza kusema.

SISIEMU wametumia silaha ya vitisho hii pia imegonga ukuta wa Berlin kwa sababu huku kwenye Internet sisi waandishi tunaweza kuwa vile tunataka. Ukitaka kuwa Jabari unakua ukitaka kuwa kipepeo unakua. Silaha hiyo ya vitisho imeshindwa kufanya kazi pia.

SISIEMu wametumia silaha ya kuhujumu Uchumi wa wanamapambano, silaha hiyo inaelekea kuwa na nguvu bado lakini muda wake wa kudumu unaenda ukingoni silaha hiyo naye itakuwa historia hivi punde.

SISIEMU wametumia silaha ya kublackmail watu kadhaa wa chini walio iba vijifedha vya kujengea nyumba hapa na pale kwa kuwaambia kwamba au mnaunga mkono au mjiandae kujibu mahakamani "nyumba zenu mmezijengaje."
Wengi wa watu hawa wamesalimu amri na kubaki kimya. Na kati yao ndo wanatupa habari nyeti za ndani ya kambi kubwa kwa sababu wapo pale kujiponya nafsi zao tu vinginevyo ni wenzetu.
Silaha hii nayo inadumu kwa sasa lakini muda kidogo ujao watu hawa watabaini kwamba SISIEMU hawana ubavu wa kuwafanya chochote.

SISIEMU wametumia silaha ya kuhonga fedha kibao.
Sisiti kusema silaha hii ni kiboko kwani imeweza kuwachota wapiganaji wengi na kuwashawishi kubadiri kambi. Unajua tena fweza ni sabuni ya Roho. silaha hii ya fedha itatusumbua sana kwa sababu moja kubwa;

Kama wapambanaji bado tumeshindwa kuziba kisima au chanzo kikubwa cha fedha haramu iingiayo mifukoni mwa viongozi wa SISIEMU kila siku.
Kwa mfano kila siku iendayo Mafisadi wanajazwa $152,000 kutoka chanzo kimoja tu cha RDC.
Ukiwa na $152K inayoingia bure bure mfukoni mwako kila siku ni Rahisi kutoa $40K na kuwahonga Wahariri na magwiji kadhaa wa habari ili waache kukuandika vibaya au wabadiri kambi kabisa na kuandika mazuri juu yako.

Naamini kabisa kwa kutumia Ngawira SISIEMU wataweza kuyarudisha nyuma majeshi yetu ya wanamageuzi na hata kutudhoofisha.
Lakini pia kitendo hicho cha SISIEMU kununua wapiganaji wetu kitatusaidia kwa sababu tutapata wasaa wa kujua nani ni mpambanaji halisi pia tutapata ujanja wa kupanga upya mapambano kwani kila siku zoezi la kutoa Rushwa huleta mgawanyiko na mpasuko mkubwa.

System kubwa zote duniani zina weakness moja.

Mfumo ujengao uimara wake pia hutoa mwanya wa kujua udhaifu wake, hiki si kitu cha moja kwa moja ni kwa wale tu watumiao bongo zao vizuri tu ndiyo huwa na macho ya kuuona udhaifu wa mfumo kupitia uimara wa mfumo.

Kwa lugha nyingine nina maana ni lazima tujifunze kutumia udhaifu wa SISIEMU kupambana na SISIEMU.

Kitendo cha kununua wahariri na wana habari,na zaidi kitendo cha KUWABENEA wanahabari ni daliali moja ya udhifu wao.

Kuwapunguza kasi wana habari kuna maana moja,mambo yote tunayo andika yanawagusa pabaya kabisa wanahanagaika huku na kule kufunika aibu yao kwa manoti.

Kusema wazi juu ya wizi wa Viongzozi wa SISIEMU kunasaidia sana.
Moja ya udhaifu wao ni kwamba hawapendi kusemwa na yeyote hata kama heshima yake ni ndogo kamaya panya buku.

Hii ina maana tukifanikiwa kuongeza kundi la watu hata wa kutoa miguno tu mapambano yetu yatafanikiwa kwa sna.
Miguno ya maelfu ya watanzania itasaidi kumpa hofu nunda wetu ataanza kukosa kujiamini, miguu yake itaanza kutetema kwa woga na hasira ya kuzomewa na kuzodolewa, mitetemo hiyo itamfanya alegee na kushindwa kubeba Furushi la ufisadi na kudondoka nalo Pwaa!
Ameskwisha.

Ni ujinga na ni kujidanganya kudhani kwamba silaha itumiwaya na mafisadi wa SISIEMU ya kutoa maburungutu kama njugu haiwezi kufanya kazi. Lakini wenda wazimu wa karne kusalimu amri eti kwa sababu tu SISIEMU wana fedha ya kuhonga.

Fedha hiyo hiyo waitumiayo kama silaha ya kuhami Ufisadi wao ndiyo hiyo hiyo itatuelekeza kwa usahihi namna ya kuwamaliza.

Tutafuata Mkuya( Trail) huo wa fedha mpaka tunduni mwao. Fedha ianyowafanya watambe leo, kesho itawatoa tunduni mwao wakiwa uchi na kuwafanya wakimbilie ugahibuni huku wakionyesha aibu yao kwa kila mtu.
 
hapo ^ tatizo lako ni kwamba, unataka kuleta mambo ya partisan hapa ukidhani serikali ni ya chama kimoja (angalau ipo madarakani under chama kimoja tawala) lakini kumbuka maendeleo/hasara sio za hicho chama bali ni watz wote kwa ujumla, sasa sijui unataka kufaidika nini kwa kuponda chama haswa pale isipostahili, i simply dont understand what it is that you are trying to achieve, and fortunately naona unapoibua neno SISIEMU nadhani unapata wafuasi wengi kiasi kwamba unadhani una-achieve kitu fulani, lakini kumbuka kwamba, unapoandika uongo chembe moja hata kama zilikuwa kurasa 10 nzima za facts tupu, TRUST ME TUTAONA KURASA ZOTE 10 NI UOZO MTUPU !

get it !
 
nimecheka sana na baadhi ya wachangiaji wa hoja kwenye hii mada hadi wengine wakitaka **viongozi wa serikali** wamlinde **mwandishi wa habari** wakati hao viongozi wenyewe wanalindwa na **jeshi la polisi** sasa najua hapa JF wengine ni wenye uelewa mkubwa, inakuwaje kiongozi anayelindwa alinde mwandishi wa habari ? got damn it, jamani fikirieni saa nyingine na sio kutamka tu ili mradi mmeongea, mnaweza kuwa na idea nzuri na kushindwa kuipresent, sasa hao viongozi wakishindwa kumlinda, mtawalaumu hao viongozi ? ni sawa sawa mgonjwa wa ngoma unaenda kupata ushauri nasaha kwa dentist !

fikirieni tena kidogo kwa hapo !

hey, by the way huyu kubenea ni mzima hadi sasa hivi au ? maana naona kimyaaaaaaaaaaa !!

Mimi nami nimecheka kweli.. yaani inakuwaje mtu afikirie kuwa mtu akisema viongozi wamlinde mtu inaama waenda na vimulimuli vyao kupiga kambi nje ya nyumba ya mtu huyo! hili linachekesha.. but ndivyo tunavyotofautiana uelewa I guess..
 
hapana, sikumaanisha hivyo unavyofikiri.... lakini anyway lets be happy for the time being kabla hatujasikia kubenea hatunae tena - - ndipo mtakapokuja na mawazo ya kumcontact saidi mwema badala ya waziri mkuu kama ilivyoelezwa hapo awali !
 
Leta vitu vyako vya "Fridays" bana.. maana wengine saumu hii kali na wiki ijayo ina mambo yake mengi tu!
 
hapo ^ tatizo lako ni kwamba, unataka kuleta mambo ya partisan hapa ukidhani serikali ni ya chama kimoja (angalau ipo madarakani under chama kimoja tawala) lakini kumbuka maendeleo/hasara sio za hicho chama bali ni watz wote kwa ujumla, sasa sijui unataka kufaidika nini kwa kuponda chama haswa pale isipostahili, i simply dont understand what it is that you are trying to achieve, and fortunately naona unapoibua neno SISIEMU nadhani unapata wafuasi wengi kiasi kwamba unadhani una-achieve kitu fulani, lakini kumbuka kwamba, unapoandika uongo chembe moja hata kama zilikuwa kurasa 10 nzima za facts tupu, TRUST ME TUTAONA KURASA ZOTE 10 NI UOZO MTUPU !
get it !

Can you pinpoint one thing that is not true in my article?
 
Rafiki zake Lowassa wote macho mekundu kama ya kindi kwa kuvuta bangi ili kujipooza na kujisahaulisha uuaji wao.
Wanao mzunguka Lowassa wengi hawaoni taabu kuua mtu yeyote hata kama ni mama yao mzazi.
Hata maaskofu wanao mzunguka hawaoni taabu kuua ili mradi hawazikosi sadaka na zaka za Lowassa, nasikia siku zoteEL huangusha pochi nene ya kifisadi kwenye matoleo na michango.

Tatizo la kutishia wajenzi wa uwazi ni moja.
Mtishaji husaidia kusambaza taarifa aitoazo mjenzi wa uwazi.

Ni sawa na kufagia zizi la mbuzi na kutupa taka kwenye shamba la mahindi ukitegemea mahindi yatapa tetenasi, unakua umechemsha ile mbaya, mavuno mara dufu.

Pole sana Mkuu Kubenea

Sasa mpo nae ufipa.
 
Back
Top Bottom