Kubenea: Lowassa ameonesha njia

Kubenea: Lowassa ameonesha njia

Unapoint mtoa mada, its good to look this in a +ve way/ side. Shida ni kwamba tofauti na wengi wetu katika siasa tukishaitwa upinzani -ve kwa kila jambo. Na pia mamvi angetumia busara zake kujua uongozi wa chama chake unauelewa wa kiwango gani ili a "forecast " kitakachojiri kabla ya kwenda kumsifia mkulu.
All in all ameki damege chama chake big time
 
Kilichobaki ni makamanda kuanza kulumbana wenyewe kwa wenyewe, kukosoana na baadhi kupeana faraja juu ya tukio lile wakati Ngoyayi kakaa kimya. Kosa lilifanyika mwaka 2015 walipompokea jamaa, yanayotokea sasa hivi ni matokea tu na wengi tuliyategemea kasoro wale fuata upepo uvumishwao na mkalia kiti.
 
Hata mkileta maelezo marefu vipi, Lowassa bado sio mtu sahihi kuwepo cdm. Anaweza kurudi tu ccm na kutoa huo ushauri wake mzuri akiwa huko. Ama anaweza kwenda hata TLP na kuongeza nguvu huko na hizo siasa zake. Watavuna watu wengi tu tunaombiwa walimpa kura mpaka cdm ikapata wabunge wengi.
Lowassa siyo mtu sahihi kuwa CDM? umerogwa? Nani mwenye chama? Nani alijiunga na chama siku ya kwanza, ya pili akawa mgombea urais na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama?
 
Kwa wasiofahamu tu ni kwamba Lowasa na Kubenea wana ukaribu wa miaka mingi hivyo inawezekana kabisa anachoongea kina baraka zake
Mbona bado mjajua kilichopo Chadema ....subiri kitifuke ....
 
Mh.Lowasa si mtu wa kujibizana sana majukwaani na hata kwenye mitamdao.Mtakumbuka alipoitwa fisadi kwa miaka mingi hakujibu kitu. Baadae watu walikuja kuona ufisadi halisi ulikuwa wapi?

Hili la kukutana na Rais na kupongeza juhudi kama lilivyoripotiwa, je ni hilo tu? Mnajuaje kama ni hayo tu aliyozungumza. Je kama kuna aliyokosoa lakini hayakuripotiwa? Je, nani alikuwepo kubalance story?

Huenda kuna mengi yalijadiliwa na huenda kuna ukosoaji na kupongeza, lakini ikaripotiwa kupongeza. Kabla Mh. Lowasa hajatoa maelezo ya kilichojadiliwa, mmeanza maneno makali na vitisho.
Kama ilivyo kawaida yake kutojibizana, kaamua kunyamaza. Mtakuja gundua baadae mambo mengine makubwa yaliyojadiliwa.

Mbona makamanda mna maneno makali? Mbona mnaleta mpasuko wa chama bila sababu za msingi?

Kumbukeni CHADEMA ndicho chama cha kidemokrasia, kinapaswa kuwa mfano kwa vyama vingine. Kutofautiana mtazamo ni moja ya mambo ya kidemokrasia. Mh. Lowasa kaona kuna mambo ya kupongeza.
 
Uzuri Kubenea alishaliona burungutu la kununua wapinzani.
 
Saed Kubenea

HATUA ya Edward Lowassa, waziri mkuu mstaafu na mgombea urais katika uchaguzi mkuu wa 2015 ya kukutana na Rais John Magufuli, imezusha taharuki ndani na nje ya chama chake.

Kinacholeta taharuki, ni kauli zake kuhusiana na utawala wa Magufuli. Binafsi, nimewasikiliza wote.

Hata hivyo, naomba niseme machache.
Kati ya mwaka 1995 hadi 2010, Zanzibar ilikumbwa na mkwamo mkubwa wa kisiasa.

Ndani ya visiwa hivyo, uhasama ulitalamaki. Fitina na maonevu mengine lukuki - yalikuwa yameshamiri.

Jemedari la kisiasa Visiwani, Maalim Seif Sharif Hamad, aliamua kukutana na hasimu wake mkuu kisiasa, Rais Amani Abeid Karume.

Mkutano kati ya Seif na Karume, ulifanyika wakati mamia ya wananchi wa Pemba wakiwa ukimbizini nje ya nchi.

Aidha, wakati Maalim anakutana na Karume, makumi ya akina mama walikuwa wamebakwa na kulawitiwa na watu wengine kadhaa walikuwa wamefunguliwa kesi za jinai mahakamani.

Si hivyo tu: Mamia ya wananchi, hasa wafuasi wa CUF walikuwa wamefutwa kazi serikalini.

Wengine kadhaa, wakiharibiwa mali zao, yakiwamo majumba, mashamba na baadhi wakiwa wameachwa wajane kutokana na mateso waliyopata wenza wao.

Maalim alikutana na Karume kimya kimya na bila kushirikisha wenzake kwenye chama.

Alikutana na kuzungumza na Karume na kukataa katakata kutaja kile walichojaliana.

Ilidaiwa kuwa Maalim alichukua hatua hiyo kwa kuwa alihofia kuwa kueleza mapema kile walichojadili; na au wanachokwenda kujadiliana, kungevuruga mikakati yake.

Hata Rais Karume naye hakueleza kuwapo mkutano na Maalim Seif. Hakueleza walichotaka kukizungumza na wala hakusema kile walichokijadili baada ya mkutano wao.

Mkutano kati ya viongozi hawa wawili ulifanyika wakati tayari vyama vya CUF na CCM, vikiwa vimefunga miafaka mitatu ya kisiasa bila mavuno kwa CUF.

Mwasisi wa mazungumzo kati ya Karume na Seif, ni mzee Nassoro Moyo, Eddy Lyami na Mansour Hamid.

Baada ya taarifa za kuwapo mkutano huo kuvuja, wafuasi wa CUF walikuja juu. Walimtukana Maalim Seif matusi ya nguoni.

Nakumbuka katika mkutano mmoja wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kibandamaiti, wafusi wa chama hicho, walimtupia mawe na maganda ya machungwa kiongozi wao huyo.

Kuna mengi ya kueleza juu ya tukio hilo. Lakini itoshe tu kusema, mkutano kati ya Maalim na Karume ndio uliozaa Katiba mpya ya Zanzibar na ndio msingi wa CUF kuingia serikalini katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Hivyo basi, naifananisha ziara ya Lowassa ya jana na tukio hilo la mwaka 2010 Visiwani.

Lowassa amekutana na Magufuli, kipindi ambacho chama chake kiko kwenye mkwamo. Hakiwezi kufanya mkutano wa hadhara.

Kimefika mbali zaidi; sasa hata uchaguzi mdogo hakiwezi kushiriki.

Baadhi ya viongozi wakuu chama badala ya kuwaongoza wanachama, nao wamegeuka kuwa walalamishi.

Ni kwa sababu, CHADEMA ya mwaka 2010 hadi 2014 ya maandamano na mikutano haipo tena.

Katika muktadha huo, njia pekee ya kutoka hapa tulipo ni kujadiliana adui yako. Lowassa amefungua njia hiyo. Ni vema ikatumiwa.

Mwisho
 
seif alipokutana na shein hakujitokeza hadharani kumsifu shein hata sikunmoja,walifanya mazungumzo kimya kiimya hadi walipotangaza muafaka,huyunwenu kaongea siku moja tu na kumpa sifa jpm kibao
 
Lowassa inawezekana hakwenda Ikulu Kama Mwana Chadema au Mwanasiasa kaenda kuzungumza ya Mkwewe Sioi maana Pamela Kawa Kama Mjane Mwaka wa pili huu anakumbatia Mto usiku peke yake
Hoja iko hapa anayosema Kubenea anahisi hana HAKIKA Maana kama ameenda kwa issue ya Muafaka kwa Vyoyote Viongozi wa Chadema wangejua na hata change kuongea kwenye Press wangekijua Lkn kusema eti alienda kama Maalim Seif
Kubenea anataka kuamini watz wote ni maBWEGE
 
Kwahiyo unadhani Lowasa kaenda kuongea na Magufuli kuhusu Serikali ya Kitaifa au Magufuli aruhusu siasa shindani za kukosoana?

Hahaha.... Poor you.
Usisahau demokrasia ni kukubali katika kutofautiana fikra .kumpinga Mbowe,Kubenea au Lowasa ni uditecta uchwara
 
Anataka afukuzwe ili agome
Kufukuzika moto uwake Kama NCCR ya Miaka ile
Ulipo tupo vs Bavicha
Wanamtandao wanataka kuteka Chadema baada ya kushindwa huko CCM
Nyie ndio umtaiua CDM chama gani hakitaki fikra au mbinu mpya .mwanachama akachangia wazo likajadiliwa .CDM imekuwa kama ccm sasa au !!???
 
Hahahahahaa Kubenea hapo Raha yake eti Ben Saa Nane anakunywa kahawa mtaani na marafiki zake makarai Bhana
 
The remaining part of the story sina interest nayo, mi naangazia hayo maneno yenye rangi nyekundu

Sitaki kuamini kuwa CCM, Usalama wa taifa hadi Jakaya walikuwa hawajui

Kama ni kweli basi hiyo ni hatari kubwa sana
Mbona kuna kauli ya Kikwete akikiri kujui kukutana huko baada ya kukutana huko kwa Karume na Seifu .usiongee kitu bila utafiti kwanza
 
Back
Top Bottom