Kubenea: Lowassa ameonesha njia

Kubenea: Lowassa ameonesha njia

Tuliwahi shauri chadema kuwa siasa za harakati hazifai. Ilifikia hatua JK aliita chadema ni mkusanyiko wa wana harakati na si wanasiasa. Ona Leo Magufuli kabeba agenda zao zote za kiharakati kitu ambacho huko nyuma ilikua adimu kumsikia mtu wa hadhi ya Rais akitamka neno fisadi!! Leo Magufuli kabeba agenda ya ufisadi... kabeba agenda za "tunaibiwa madini" kabeba agenda ya tumbua tumbua ili kuzima ile hoja ya "udhaifu"

Shida ni kuwa Magufuli kabeba uanaharakati sasa wanashindwa tembea na bit!!
Mkuu umeelewa ulichoandika? unashangilia Porojo...na unataka Chadema waende na Bit magu umeelewa vzr ulichoandika kweli?
 
Tuliwahi shauri chadema kuwa siasa za harakati hazifai. Ilifikia hatua JK aliita chadema ni mkusanyiko wa wana harakati na si wanasiasa. Ona Leo Magufuli kabeba agenda zao zote za kiharakati kitu ambacho huko nyuma ilikua adimu kumsikia mtu wa hadhi ya Rais akitamka neno fisadi!! Leo Magufuli kabeba agenda ya ufisadi... kabeba agenda za "tunaibiwa madini" kabeba agenda ya tumbua tumbua ili kuzima ile hoja ya "udhaifu"

Shida ni kuwa Magufuli kabeba uanaharakati sasa wanashindwa tembea na bit!!
...so uanaharakati ukibebwa na Jamaa yako ni sawa ila wakifanya Chadema hapana now nimekuelewa ndugu
 
Tunarudi kule kule harakati ziachiwe akina Helen kijo bi Simba!! Siasa za harakati hazina manufaa!! CUF ilijaribu ikashindwa... NCCR ilishindwa na hata CDM ya Dr Slaa ilishindwa pia. Slaa amewahi endesha operesheni sangara lkn kwenye udiwani wakavuna kata tatu tu!!

Zile siasa za kuimba CCM inafumbia macho ufisadi hazina nguvu tena coz Magufuli keshamaliza agenda hiyo kwa sanaa zake!!

Zile agenda za tunaibiwa kwenye madini Magufuli kazibeba tayari!!

Zile agenda za uzembe wa kuchukua hatua Magufuli anacheza na mdundo!!

Unalotakiwa kujua Majira na mambo yamebadilika!! Majira hayafwati watu bali watu hufwata Majira!!! Sisa za harakati kwa karne hii hazina nafasi tena mkuu.
Kwahiyo unawashauri Chadema wamlambe miguu mtukufu
 
Mh.Lowasa si mtu wa kujibizana sana majukwaani na hata kwenye mitamdao.Mtakumbuka alipoitwa fisadi kwa miaka mingi hakujibu kitu. Baadae watu walikuja kuona ufisadi halisi ulikuwa wapi?

Hili la kukutana na Rais na kupongeza juhudi kama lilivyoripotiwa, je ni hilo tu? Mnajuaje kama ni hayo tu aliyozungumza. Je kama kuna aliyokosoa lakini hayakuripotiwa? Je, nani alikuwepo kubalance story?

Huenda kuna mengi yalijadiliwa na huenda kuna ukosoaji na kupongeza, lakini ikaripotiwa kupongeza. Kabla Mh. Lowasa hajatoa maelezo ya kilichojadiliwa, mmeanza maneno makali na vitisho.
Kama ilivyo kawaida yake kutojibizana, kaamua kunyamaza. Mtakuja gundua baadae mambo mengine makubwa yaliyojadiliwa.

Mbona makamanda mna maneno makali? Mbona mnaleta mpasuko wa chama bila sababu za msingi?

Kumbukeni CHADEMA ndicho chama cha kidemokrasia, kinapaswa kuwa mfano kwa vyama vingine. Kutofautiana mtazamo ni moja ya mambo ya kidemokrasia. Mh. Lowasa kaona kuna mambo ya kupongeza.
Sasa kama unaunga Mkono kutofautiana mawazo mbona hutaki Lowasa ajadiliwe
 
Nashauri huyu mzee atupishe.
Hizi ni siasa za ccm hakunaga fikra tofauti .CDM sio ccm lazima tukubaliane na fikra na mbinu tofauti kutoka kwa wanachama achilia mbali Lowasa au Kubenea .
 
Lowassa siyo mtu sahihi kuwa CDM? umerogwa? Nani mwenye chama? Nani alijiunga na chama siku ya kwanza, ya pili akawa mgombea urais na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama?

Sasa ngoja tumuambie mwenye chama hapa hadharani kama alinunua chama basi aliingizwa mjini, watoto wa marehemu wamekuwa wakubwa.
 
Lowassa katuangusha
Ujui mbinu za siasa au unajua moja tuu au mbili kukabiliana kwa hoja au maandamano ujui zaidi ya hapo .heri hukae kimya ,CDM hoyeee kwakuwa na watu wakuonyesha njia wakati wa mkwamo .Lowasa hoyeee
 
Kuna udhaifu mkubwa kwa kiongozi mkuu ndani ya Chedema. Yanayoendelea sasa yanaonyesha Mwenyekiti amekosa udhibiti wa nidhamu ndani ya chama. Haiwezekani kila mtu anaibuka na kuzungumza na tamko lake ikachukuliwa ni kauli ya Chama. Hakuna nidhamu ya chama kuwa na utaratibu wa kuheshimu tamko la kiongozi mkuu na wengine kusubiri maelekezo ya vikao.
 
Naanza ku doubt uwezo wa kufikiri wa Kubenea!
Ataa yeye pia kwa msg hii .lazima ataanza ku doubt uwezo wako wa kufikiri .kwani hujui kuwa fikra utolewa zikajadiliwa na kupatikana fikra ya kufanyia kazi .sio fikra kushutumiwa na kuonekana adui .
 
Lowassa siyo mtu sahihi kuwa CDM? umerogwa? Nani mwenye chama? Nani alijiunga na chama siku ya kwanza, ya pili akawa mgombea urais na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama?

Sasa ngoja tumuambie mwenye chama hapa hadharani kama alinunua chama basi aliingizwa mjini, watoto wa marehemu wamekuwa wakubwa.
 
Ataa yeye pia kwa msg hii .lazima ataanza ku doubt uwezo wako wa kufikiri .kwani hujui kuwa fikra utolewa zikajadiliwa na kupatikana fikra ya kufanyia kazi .sio fikra kushutumiwa na kuonekana adui .
Kuna level ya mtu expected of him or her to think. If you go outside that ambit, then regardless of the liberty one to air his or her views, those capable of philosophical thinking will doubt you.
 
Saed Kubenea

HATUA ya Edward Lowassa, waziri mkuu mstaafu na mgombea urais katika uchaguzi mkuu wa 2015 ya kukutana na Rais John Magufuli, imezusha taharuki ndani na nje ya chama chake.

Kinacholeta taharuki, ni kauli zake kuhusiana na utawala wa Magufuli. Binafsi, nimewasikiliza wote.

Hata hivyo, naomba niseme machache.
Kati ya mwaka 1995 hadi 2010, Zanzibar ilikumbwa na mkwamo mkubwa wa kisiasa.

Ndani ya visiwa hivyo, uhasama ulitalamaki. Fitina na maonevu mengine lukuki - yalikuwa yameshamiri.

Jemedari la kisiasa Visiwani, Maalim Seif Sharif Hamad, aliamua kukutana na hasimu wake mkuu kisiasa, Rais Amani Abeid Karume.

Mkutano kati ya Seif na Karume, ulifanyika wakati mamia ya wananchi wa Pemba wakiwa ukimbizini nje ya nchi.

Aidha, wakati Maalim anakutana na Karume, makumi ya akina mama walikuwa wamebakwa na kulawitiwa na watu wengine kadhaa walikuwa wamefunguliwa kesi za jinai mahakamani.

Si hivyo tu: Mamia ya wananchi, hasa wafuasi wa CUF walikuwa wamefutwa kazi serikalini.

Wengine kadhaa, wakiharibiwa mali zao, yakiwamo majumba, mashamba na baadhi wakiwa wameachwa wajane kutokana na mateso waliyopata wenza wao.

Maalim alikutana na Karume kimya kimya na bila kushirikisha wenzake kwenye chama.

Alikutana na kuzungumza na Karume na kukataa katakata kutaja kile walichojaliana.

Ilidaiwa kuwa Maalim alichukua hatua hiyo kwa kuwa alihofia kuwa kueleza mapema kile walichojadili; na au wanachokwenda kujadiliana, kungevuruga mikakati yake.

Hata Rais Karume naye hakueleza kuwapo mkutano na Maalim Seif. Hakueleza walichotaka kukizungumza na wala hakusema kile walichokijadili baada ya mkutano wao.

Mkutano kati ya viongozi hawa wawili ulifanyika wakati tayari vyama vya CUF na CCM, vikiwa vimefunga miafaka mitatu ya kisiasa bila mavuno kwa CUF.

Mwasisi wa mazungumzo kati ya Karume na Seif, ni mzee Nassoro Moyo, Eddy Lyami na Mansour Hamid.

Baada ya taarifa za kuwapo mkutano huo kuvuja, wafuasi wa CUF walikuja juu. Walimtukana Maalim Seif matusi ya nguoni.

Nakumbuka katika mkutano mmoja wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kibandamaiti, wafusi wa chama hicho, walimtupia mawe na maganda ya machungwa kiongozi wao huyo.

Kuna mengi ya kueleza juu ya tukio hilo. Lakini itoshe tu kusema, mkutano kati ya Maalim na Karume ndio uliozaa Katiba mpya ya Zanzibar na ndio msingi wa CUF kuingia serikalini katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Hivyo basi, naifananisha ziara ya Lowassa ya jana na tukio hilo la mwaka 2010 Visiwani.

Lowassa amekutana na Magufuli, kipindi ambacho chama chake kiko kwenye mkwamo. Hakiwezi kufanya mkutano wa hadhara.

Kimefika mbali zaidi; sasa hata uchaguzi mdogo hakiwezi kushiriki.

Baadhi ya viongozi wakuu chama badala ya kuwaongoza wanachama, nao wamegeuka kuwa walalamishi.

Ni kwa sababu, CHADEMA ya mwaka 2010 hadi 2014 ya maandamano na mikutano haipo tena.

Katika muktadha huo, njia pekee ya kutoka hapa tulipo ni kujadiliana adui yako. Lowassa amefungua njia hiyo. Ni vema ikatumiwa.

Mwisho
shida moja tuliyo nayo vijana na nakumbuka nimewahi kusema shida hii hata wakati hule wa uchaguzi, tunajibu mambo kwa hisia tu sio kwa kufikiri. Ndugu kubenea ametumia mifano akafanya comparison na kufanya hitimisho lake. Sasa kwanini hatujishughulishi na hoja yake?
 
Naomba na mimi nitoe maoni yangu kidogo...

katika mapambano yoyote inapojitokeza chance au fursa ya kujaribu mbinu mpya basi hutumika ila pia silaha huendelea kuwa mkononi wakati mbinu ya maongezi inatumika mpaka itakapoonyesha mafanikio ndipo silaha zinawekwa chini. Rejea mapambano ya waasi wa FARC dhidi ya serikali ya colombia....rejea wapigania uhuru wa south africa enzi hizo...vita na mazungumzo kwa wakati mmoja.

Wengi wanabeza Lowasa hawezi kibadili ugumu na kiburi cha magu...sio kweli..kwa hali ilipofikia kama taifa Magu na washauri wake wanajua nini kinakuja na wanalazimika kutumia fursa ya kukutana na kiongozi wa upinzani ili waweze kujinusuru na makubwa ambayo yangefuata ...rejea Tundu lissu alivyoanza kutema cheche na ameenda ulaya kwa wazungu ambao wanamsikiliza na kumwona na wanahoji vizuri sana kwa kila.detail.

MAGU ATABADILIKA MAANA HAWEZI KUKUBALI KUPITIA YALE YA MUGABE....na Lowasa ni mtu sahihi maana ni diplomatic na anaouwezo wa ku give and take katika negotiation agenda atazotumwa na vhama pindi muda wa maongezi halisi utapowadia...

SIASA ZA NGUVU MAANDAMANO NA VIRUNGU ZIMEPITWA NA WAKATI....

Inahitaji maji na moto ili chuma kuundwe na muhunzi upate zana ...... magu moto lowasa maji wananchi wahunzi taifa zana bora.

Hawa wakubwa wanapoongea huwa hawatoi details zote...main agenda huwa inafichwa kwanza na mwisho wa siku utasikia lowassa na mbowe wameenda ikulu kuongea na rais then tutaona uhuru wa siasa unaongezeka na mwishowe kesi za kijinga kufutwa na kelele za katiba mpya kusikilizwa na kutekelezwa kwa baadhi ya hatua za kukuza uchumi

NITOE ANGALIZO
...haya ni maoni yangu nayanatokana na uelewa wangu mdogo ila pia sio shuruti yaaminiwe na yachukuliwe kama maandiko matakatifu.
 
Kubenea yupo sahihi. Siasa za kiharakati za akina Lema kwa karne hii hazisaidii
Sio hazisaidii ila tatizo hazikwamui mkwamo uliopo .ukweli sasa hivi ccm imekwama kwa kukosa fikra mpya sasa inatumia nguvu za serikali na cha ajabu CDM nayo inataka kukwama kwa kukataa fikra mpya wakati aina serikali.Ushauri Lema,Mbowe,Lisu,tulizeni kichwa kubalini fikra mpya .CDM tujikwamue
 
Back
Top Bottom