Kweli kabisaLowasa ondoka tu tuendeleze mashambulizi dhidi yako maana tulisimama
Kweli kabisaLowasa ondoka tu tuendeleze mashambulizi dhidi yako maana tulisimama
Well said mkuu hawa timu ulipo tupo wasituzingue, lowasa hawezi kuwa juu ya chama kwa kuwa ameona ameridhishwa na uongozi wa kipara ni heri aondoke na timu yake warudi kwao ccm watuachie chadema yetu.Kwa hiyo baada ya katiba mpya Zanzibar CUF wamepata nn na wana nini sasa.
Kweli Mwanahabari Huru umeamua kuleta upuuzi huu ktk jukwaa hili.
Nimesoma naona kilichopo ktk habari hii ya kubenea ni kujaribu kutongoza watu ambao wana fikra na wameshaelewa ukweli.
Lowassa alienda kutetea maslahi yake full stop.
EL sio mpinzani na hamjawahi kuwa mpinzani.
Si akapande daladala za gongo la mboto ili aendelee kupata wafuasi kama wkt ule wa kampeni.
Maigizo ni kitu cha ajabu sana ktk uhalisia.
Tuna bahati magazeti ya kubenea yamefungiwa angeanza story zake za kutunga uongo uongo tu..
Kubenea maslahi..
Mkuu huwezi niumiza kwa chochote. Nimetoa tu mtazamo wangu. Siasa za sitaki nataka za CCM zisiwatoe kwenye reli.
Juzi mlitishwa na Kauli zao kuwa mmechukua mafisadi nanyi mkaanza sutana Leo hao hao wanaanza nyimbo za Lowassa mzuri mara nimefarijika sijui nini.
Again chadema haiwezi ishi kwa siasa za personal attack!! Chadema haiwezi vuka kwa siasa za majungu na matusi chadema itavuka kwa nguvu ya hoja.
Mkuu umechelewa huyu jamaa ni hewa siku nyingi tuu. Ungekuwa unamfatilia sana ungeshamuelewa. Siko ktk vyama lakini mimi napenda mtu nwenye msimamo na strong feelings juu yakile anacho kiamini. Mfano sikubaliani ni siasa za Dr slaa lakini napenda anavyosimamia misimamo wake no matter yuko wrong au right.Naanza ku doubt uwezo wa kufikiri wa Kubenea!
Mkuu matusi sijamaanisha wewe binafsi namaanisha taasisi ya chadema!! Ok tujadili hivi, Lowassa kwa sasa anawazuia nini chadema kusonga mbele ikiwa si mwenyekiti au katibu mkuu?Mkuu nashukuru kwa kunielewa, ila kwa bahati mbaya sana unadhani mimi sijui ipi ni propaganda toka ccm na upi ni ukweli na upi ni udhaifu wa cdm. Nina uwezo mkubwa wa kutenganisha hayo mambo. Pitia hata hoja zangu nimeshikilia kwamba Lowassa sio chaguo kwa cdm kwenye nafasi ya urais kwani sio wa aina ya siasa za cdm. Hicho alichokifanya au kukisema Magufuli jana baada ya Lowassa kumtembelea ni kwamba alimgeuza Lowassa mtaji wa kisiasa na sehemu ya kuwapata wakosoaji wake akidhani wakosoaji wake wanamuwakilisha Lowassa.
Nikiwa hapa hapa ninakanusha kwa wale wanaopotosha kwamba Lowassa ndio aliyesababisha cdm leo ina wabunge wengi, hilo si kweli. Nikasema kwamba ili tuamini Lowassa kweli alikuwa kuinyanyua cdm na sio hiyo nafasi ya urais ndio ilimleta, wanionyeshe mchango wake hata mdogo ambao cdm wamenufaika nao. Wote tuliona miaka mitatu kabla ya uchaguzi jinsi EL alivyokuwa anapita kwenye taasisi hasa za dini akifanya harambee za kuwezezesha ujenzi. Je toka ameingia cdm na kuukosa urais amejenga ofisi ngapi kwa cdm? Nina mashaka na unaposema personal attack unataka kumaanisha au kuficha nini, ni ukweli bila kujali ccm wanasema nini kwamba Lowassa hana msaada unaonekana kwa cdm kama alivyofanya kabla ya uchaguzi kwenye taasisi mbalimbali. Mimi sijamtukana Lowassa labda kama ukweli wangu dhidi yake utautafsiri kama matusi. Unapojadili na mimi uwe makini maana kuna makamanda wenye maslahi naye wanakwazika sana pindi ukweli tunapousema. Demokrasia ni pamoja na kuvumilia ukweli kamanda mwenzangu.
Mkuu matusi sijamaanisha wewe binafsi namaanisha taasisi ya chadema!! Ok tujadili hivi, Lowassa kwa sasa anawazuia nini chadema kusonga mbele ikiwa si mwenyekiti au katibu mkuu?
Mkuu hujanijibu swali langu.... CDM ina wazee wengi tu waliochoka mikiki mikiki...Lowassa hajatukanwa bali anapewa vijembe vya kisiasa kitu ambacho hakikwepeki. Usiichafue cdm kwa kumtetea Lowassa tafadhali, ni kweli Lowassa hajazuia chochote, lakini kama unataka aondoke sio vibaya, na atakapoondoka utaona mageuzi yatakayotokea. Ujio wake ilikuwa ni kama nyumba iliyojengwa kwa matofali ya barafu. Kumbuka huku kwenye siasa ni mbio ndefu (marathon) na yeye ni mtu wa mbio fupi. Akae pembeni kwani umri wake umeshasonga na ni ukweli ulio dhahiri hata afya yake haimudu mikikimikiki ya cdm, na hana uwezo wa siasa za upinzani husasani cdm ambayo iko kiharakati zaidi.
Umeandika point failures hublame wengi kwa chuki hata hapo siwanaweza Ku move on tu kwani wamenyimwa?Mkuu matusi sijamaanisha wewe binafsi namaanisha taasisi ya chadema!! Ok tujadili hivi, Lowassa kwa sasa anawazuia nini chadema kusonga mbele ikiwa si mwenyekiti au katibu mkuu?
Unayakubali maneno ya Dr. Slaa kwamba Lowassa ni liability na si asset?Nashauri huyu mzee atupishe.
Mkuu hujanijibu swali langu.... CDM ina wazee wengi tu waliochoka mikiki mikiki...
Nimeuliza tu, Lowassa anaizuia nini chadema kusonga mbele? Au ni nini kikwazo cha Lowassa kwa CDM?
Tuliwahi shauri chadema kuwa siasa za harakati hazifai. Ilifikia hatua JK aliita chadema ni mkusanyiko wa wana harakati na si wanasiasa. Ona Leo Magufuli kabeba agenda zao zote za kiharakati kitu ambacho huko nyuma ilikua adimu kumsikia mtu wa hadhi ya Rais akitamka neno fisadi!! Leo Magufuli kabeba agenda ya ufisadi... kabeba agenda za "tunaibiwa madini" kabeba agenda ya tumbua tumbua ili kuzima ile hoja ya "udhaifu"Kumbe Kubenea siku hizi akili zake zimemrudia. Kaandika vizuri sana na kwa kiwango cha a full qualified journolist. Napendekeza hata hilo gazeti lake lifunguliwe.
Ukweli kabisa ni kwamba sonono, kelele na malalamiko ya kila siku ya chadema ndani na nje ya nchi yanatokana na kupigwa marufuku kwa mikutano na maandamano yao ya kila kukicha nchi nzima yenye malengo kama yale yaliyokuwemo kwenye operesheni yao ya UKUTA waliyopanga kuanza kuifanya Septemba 2016. Mikutano na maandamano ya aina hiyo walikuwa wamezoea kuifanya katika kipindi cha utawala wa JK hadi chadema ikajulikana kama chama cha maandamano na vurugu. Maduka na shughuli mbali mbali za kimaendeleo ilibidi zifungwe wakati wa mikutano na maandamano hayo. Kuna watu walijehuriwa au kuporwa mali zao katika maandamano hayo.
Malengo na mikakati wa operesheni UKUTA ambayo ilikuwa iwe endelevu na ya kila siku nchi nzima hadi pale JPM atakapoachia madaraka yake ya urais, ndiyo iliyomkasirisha kila mtu mwenye mapenzi na nchi hii. JPM aliwajibu yeye huwa hajaribiwi na kama wanabishi wajaribu waone kitakachowapata. Na hivyo mikutano na maandamano ya hadhara ya kibabe za kisiasa ya aina hiyo yakapigwa maarufuku. Haya waliyasababisha wao wenyewe na sasa serikali iko mbioni kuwakilisha musuada wa kisheria wa namna bora yenye ustaarabu ya kuendesha shughuli za siasa kwa vyama hivi.
Hivyo Lowassa kwenda kujadiliana na JPM kuhusu utatuzi wa jambo hili lililokwamisha vyama vya upinzani kufanya mikutano na maandamano yake ya hadhara lilipaswa kuungwa mkono. Lakini badala yake limechukuliwa kihasi na hivyo kumfanya Lowasa kuahirisha mkutano wake aliokuwa kapanga na vyombo vya habari kuelezea yale mazuri kwa chadema aliyovuna kutokana na majadiliano aliyoyafanya na rais wa JMT. Mbowe, Lema na Lissu hawayataki hata kuyasikia sababu tu kwamba Lowasa wamesikika akimpongeza rais kwa kuzalisha ajira kutokana na mpango wake wa kujenga SGR na Stieglers electric power plant! Tunampongeza Kubenea kwa kutounga msimamo huo wa akina Mbowe Lema na Lissu (MLL) wakisingizia kuwa ni msimamo wa chama. Tunajua kuwa kwa msimamo wako huu yanaweza yakakupata yale yaliyompata Zitto Kabwe alipokuwa kwenye chama hicho. Keep it up Mr Kubenea!
Lowasa anazuia CHADEMA kupambana na sera ya ufisadi kwa sababu ni fisadi nambari moja tanzaniaMkuu hujanijibu swali langu.... CDM ina wazee wengi tu waliochoka mikiki mikiki...
Nimeuliza tu, Lowassa anaizuia nini chadema kusonga mbele? Au ni nini kikwazo cha Lowassa kwa CDM?
DhamanaMwanahabari Huru Lowasa muoga,,,ameenda kumuomba Ngosha amsaidie mkwewe haweze kupata nusura na kesi yake ya uhujumu uchumi ambayo haina zamana inawasotesha keko,,
Tunarudi kule kule harakati ziachiwe akina Helen kijo bi Simba!! Siasa za harakati hazina manufaa!! CUF ilijaribu ikashindwa... NCCR ilishindwa na hata CDM ya Dr Slaa ilishindwa pia. Slaa amewahi endesha operesheni sangara lkn kwenye udiwani wakavuna kata tatu tu!!Hao wazee walioko cdm wamezeekea kwenye upinzani. Lowassa kaja upinzani kwa ajili ya kupata nafasi ya kugombea urais aliyoikosa ccm, huo ndio ukweli. Suala la kukua kwa cdm kwake sio issue na hapo alipo wala hajui cdm ina wanachama wangapi hai.
Jibu la swali lako, cdm ni chama kinachofanya siasa za kiana harakati, Lowassa hakubaliani na siasa hizo. Hivyo kwa kuwa anapewa nafasi ya kusikilizwa na viongozi, wengi wanafanyia kazi mawazo yake. Iwapo ataondoka ni dhahiri cdm itarudi kwenye siasa zake ambazo Lowassa aliwakuta nazo. Simply Lowassa ni kama kocha aliyekuja na kubadili formation, lazima timu iyumbe. Huenda kwa mfano huu nitakuwa nimekata kiu yako. Kwa hiyo kiroho safi ni bora arudi kule kwenye siasa zake za kistaarabu atuachie cdm yenye siasa zisizo za kistaarabu.
Kama wewe ni mpenzi wa mpira hasa wa miguu, kuna timu inaitwa Barcelona, aina ya mchezo wao ni pasi fupi fupi na kufunga kwa ustadi mkubwa. Sasa ukimpa kocha aliyezoea mipira mirefu na mashambulizi ya kustukiza hiyo timu haiwezi kucheza soka lake maridadi. Na hata ukiwa kocha wa timu hiyo, hata ulete makombe kwa mtindo huo mashabiki wa timu hiyo hawatakutaka. Kwa hiyo Lowassa yuko sehemu isiyomfaa.
Kuhusu ufisadi Magufuli katufungia mjadala juzi.Lowasa anazuia CHADEMA kupambana na sera ya ufisadi kwa sababu ni fisadi nambari moja tanzania