Kubenea: Lowassa ameonesha njia

Kubenea: Lowassa ameonesha njia

Kilichopo, kazi iliyobaki wanayoifanya ccm ni kutafuta namna ya kuua upinzani, hasa Chadema! Swala la maendeleo imekuwa sio kipaumbele tena....!

Ila wasichokijua kwa mazingira ya sasa, kuuwa upinzani ni near impossible job na sababu kubwa ni kuwa watu wengi, hasa vijana wamepigika ile mbaya na ni wazi serikali hii imekosa mbinu/mikakati ya kuwaondoa ktk hali hiyo..

Na serikali baada ya kuukosa ufumbuzi wa tatizo wamekuwa desperate na matokeo yake kuanza hii biashara ya nunua nunua hali ambayo imefanya izidi kuchukiwa zaidi na wananchi.

Hata kama wataendelea kutawala lkn watatawala katikati ya chuki kubwa na hawatakuwa tofauti na iliyokuwa serikali ya Mugabe kule Zimbabwe. Na hatimaye mwisho wao utakuwa mbaya ni hakuna mfano.
 
Kubenea, sawa lkn hoja zako nyingi zinaukakasi. Kama alikuwa na nia njema na chama chake angeweka akiba ya maneno kama Seif, ngelikaa kimya bila kusema chochote!!!!!!!!!!!!!!!
 
Lowassa àende tu anatuharibia chama sisi tumeshazoea kuandamana tangu aje anajifanya kuinyenyekea ccm
 
Mvua ndio imekolea
Mashamba maji yameingia
sasa nikupanda mpunga tu
hii siasa ya Wabongo ngumu kumeza
 
Kosa kubwa lililowahi kufanywa na CDM tangu kuasisiwa kwake ni kumpokea ENL
 
Mbona unaanza kuweweseka?
Mm siweweseki . Wakuweweseka utakuwa wewe unaodhani mawazo ya kakikundi kamoja kalikofilisi nchi miaka yote leo kanaweza kakaleta maendeleo? Kale kakikundi kaliko uza nyumba za uma, kaliko nunua vivuko vibovu na kalikoua azimio la arusha ambalo kimsingi ndio philosophy ya taamifa leo kana kuja kwa frastrations at hako kakikundi kanajengwa upya? Poor u. Mnajenga viwanda kwa phylosophy ipi? Unafikiri kujenga viwanda ni sawa na kufokafoka bila sababu kama mwehu? Mbomoe nchi wenyewe kisha mjenge wenyewe ? Huko co kuweweseka kweli? Mm siweweseki kwakuwa najua yanyotamkwa hayawezekani na hayatawezekana. Labda kumnunua mtulia na kufungia magazeti hayo yanawezekana
 
Mm siweweseki . Wakuweweseka utakuwa wewe unaodhani mawazo ya kakikundi kamoja kalikofilisi nchi miaka yote leo kanaweza kakaleta maendeleo? Kale kakikundi kaliko uza nyumba za uma, kaliko nunua vivuko vibovu na kalikoua azimio la arusha ambalo kimsingi ndio philosophy ya taamifa leo kana kuja kwa frastrations at hako kakikundi kanajengwa upya? Poor u. Mnajenga viwanda kwa phylosophy ipi? Unafikiri kujenga viwanda ni sawa na kufokafoka bila sababu kama mwehu? Mbomoe nchi wenyewe kisha mjenge wenyewe ? Huko co kuweweseka kweli? Mm siweweseki kwakuwa najua yanyotamkwa hayawezekani na hayatawezekana. Labda kumnunua mtulia na kufungia magazeti hayo yanawezekana
Insha yoote hii ya nini sasa?
 
Kweli tupu umesema mkuu. EL hajielewi yupo kwa maslahi yake..
Ujafikisha ataa mwezi JF wewe ndio huwe kiongozi wakushauri wana Cdm hapa JF maccm umna akili za kuazima .awamu hii humnalipwa sh ngapi lumumba au bado ni bk 7
 
Si mlisema Mwanachadema anaweza kumuunga mkono Rais Magufuli akiwa ndani ya Chadema siyo lazima ahamie CCM. Pia mlimwambia Lowassa 'ULIPO TUPO' ,mbona mnabadilika?
 
Kuna level ya mtu expected of him or her to think. If you go outside that ambit, then regardless of the liberty one to air his or her views, those capable of philosophical thinking will doubt you.
Uwezi pata fikra mpya kwa kuwaza ukifuata mstari au kufuata sheria na kanuni mlizo kwama nazo mlipo ndani ya boksi .ni sharti uwaze nje ya boksi .thats its
 
Saed Kubenea

HATUA ya Edward Lowassa, waziri mkuu mstaafu na mgombea urais katika uchaguzi mkuu wa 2015 ya kukutana na Rais John Magufuli, imezusha taharuki ndani na nje ya chama chake.

Kinacholeta taharuki, ni kauli zake kuhusiana na utawala wa Magufuli. Binafsi, nimewasikiliza wote.

Hata hivyo, naomba niseme machache.
Kati ya mwaka 1995 hadi 2010, Zanzibar ilikumbwa na mkwamo mkubwa wa kisiasa.

Ndani ya visiwa hivyo, uhasama ulitalamaki. Fitina na maonevu mengine lukuki - yalikuwa yameshamiri.

Jemedari la kisiasa Visiwani, Maalim Seif Sharif Hamad, aliamua kukutana na hasimu wake mkuu kisiasa, Rais Amani Abeid Karume.

Mkutano kati ya Seif na Karume, ulifanyika wakati mamia ya wananchi wa Pemba wakiwa ukimbizini nje ya nchi.

Aidha, wakati Maalim anakutana na Karume, makumi ya akina mama walikuwa wamebakwa na kulawitiwa na watu wengine kadhaa walikuwa wamefunguliwa kesi za jinai mahakamani.

Si hivyo tu: Mamia ya wananchi, hasa wafuasi wa CUF walikuwa wamefutwa kazi serikalini.

Wengine kadhaa, wakiharibiwa mali zao, yakiwamo majumba, mashamba na baadhi wakiwa wameachwa wajane kutokana na mateso waliyopata wenza wao.

Maalim alikutana na Karume kimya kimya na bila kushirikisha wenzake kwenye chama.

Alikutana na kuzungumza na Karume na kukataa katakata kutaja kile walichojaliana.

Ilidaiwa kuwa Maalim alichukua hatua hiyo kwa kuwa alihofia kuwa kueleza mapema kile walichojadili; na au wanachokwenda kujadiliana, kungevuruga mikakati yake.

Hata Rais Karume naye hakueleza kuwapo mkutano na Maalim Seif. Hakueleza walichotaka kukizungumza na wala hakusema kile walichokijadili baada ya mkutano wao.

Mkutano kati ya viongozi hawa wawili ulifanyika wakati tayari vyama vya CUF na CCM, vikiwa vimefunga miafaka mitatu ya kisiasa bila mavuno kwa CUF.

Mwasisi wa mazungumzo kati ya Karume na Seif, ni mzee Nassoro Moyo, Eddy Lyami na Mansour Hamid.

Baada ya taarifa za kuwapo mkutano huo kuvuja, wafuasi wa CUF walikuja juu. Walimtukana Maalim Seif matusi ya nguoni.

Nakumbuka katika mkutano mmoja wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kibandamaiti, wafusi wa chama hicho, walimtupia mawe na maganda ya machungwa kiongozi wao huyo.

Kuna mengi ya kueleza juu ya tukio hilo. Lakini itoshe tu kusema, mkutano kati ya Maalim na Karume ndio uliozaa Katiba mpya ya Zanzibar na ndio msingi wa CUF kuingia serikalini katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Hivyo basi, naifananisha ziara ya Lowassa ya jana na tukio hilo la mwaka 2010 Visiwani.

Lowassa amekutana na Magufuli, kipindi ambacho chama chake kiko kwenye mkwamo. Hakiwezi kufanya mkutano wa hadhara.

Kimefika mbali zaidi; sasa hata uchaguzi mdogo hakiwezi kushiriki.

Baadhi ya viongozi wakuu chama badala ya kuwaongoza wanachama, nao wamegeuka kuwa walalamishi.

Ni kwa sababu, CHADEMA ya mwaka 2010 hadi 2014 ya maandamano na mikutano haipo tena.

Katika muktadha huo, njia pekee ya kutoka hapa tulipo ni kujadiliana adui yako. Lowassa amefungua njia hiyo. Ni vema ikatumiwa.

Mwisho
Kumbe njia ya upinzani kupata ahueni ni kwenda kulamba miguu ya chama kubwa! Kweli mwenye nguvu mpishe.
 
Chadema wanapaswa kumwelewa Lowassa. Huyu hawezi kuwa 'mpinzani' wanayemfahamu kwa matendo na kauli zake. Ni tofauti. Pia Lowassa 'ameshindwa' kufahamu tabia za siasa za upinzani duniani na hasa za huku kwetu Afrika. Kuna njia ya kuongea kama mpinzani hata ukisifia kuna njia yake kama ilvyo kwa chama tawala 'kinavyosifia' upinzani.
 
Hongera Kubenea kwa kuwapa hawa Bavicha siasa sio uadui.
Kama Nelson Mandela aliweza kukaa meza moja na Fredrick De Clerk. Lowassa kukutana na Rais Magufuli ni ukomavu wa Demokrasia nchini
 
Back
Top Bottom