Kubenea: Lowassa ameonesha njia

Kubenea: Lowassa ameonesha njia

Mnatuvuruga sana wewe Kubenea. kaeni ktk chama toeni tamko acheni upuuzi wa kuchanganya wanachama kwa matamko ya kila mtu! ujinga mtupu!
 
Na aende tu.
Watanzania daini katiba mpya na tume huru vinginevyo mtapata tabu sana.
Taifa limegawanyika kabisa
 
Tunarudi kule kule harakati ziachiwe akina Helen kijo bi Simba!! Siasa za harakati hazina manufaa!! CUF ilijaribu ikashindwa... NCCR ilishindwa na hata CDM ya Dr Slaa ilishindwa pia. Slaa amewahi endesha operesheni sangara lkn kwenye udiwani wakavuna kata tatu tu!!

Zile siasa za kuimba CCM inafumbia macho ufisadi hazina nguvu tena coz Magufuli keshamaliza agenda hiyo kwa sanaa zake!!

Zile agenda za tunaibiwa kwenye madini Magufuli kazibeba tayari!!

Zile agenda za uzembe wa kuchukua hatua Magufuli anacheza na mdundo!!

Unalotakiwa kujua Majira na mambo yamebadilika!! Majira hayafwati watu bali watu hufwata Majira!!! Sisa za harakati kwa karne hii hazina nafasi tena mkuu.

Lusungo uko sahihi sana kwenye andishi lako. Lowassa ni mtu mwenye siasa za kistaarabu kwa mujibu wa mtazamo wako na hata mimi hilo sipingi. Ila cdm kinaendesha siasa ngumu ambazo sio mtindo wa Lowassa. Ili tusimkwaze ndio tunataka aondoke aanzishe chama chake cha kistaarabu, ama ajiunge na TLP au UDP nk kwani hivyo vinamuunga mkono rais wazi wazi. Na kwakuwa tunaaminishwa ana wapiga kura 6m watamfuata huko aliko, aiche cdm na siasa zake za hovyo.

Hayo unayoamini kwamba Magufuli anayafanyia kazi na anakubalika yalipaswa kuonekana kwenye uchaguzi juzi. Lakini unyama uliofanyika ni bora hata enzi za JK ambaye hakuwa na sifa za huyu. Kuwa na siasa za kistaarabu haimaanishi uwe mjinga. Hizo kata 3 unazosema Slaa alipata ni katika mazingira yaliyochangia magari mengi ya polisi kuletwa wakati wa uchaguzi wa 2015. Aliyekudanganya CUF walishindwa kwa siasa zao muambie aendelee kukupa hadithi hiyo hiyo. Kilichotokea uchaguzi wa 2015 ni kituko kingine huko ZNZ. Narudia, simtukani Lowassa, lakini cdm sio sehemu sahihi kwake.
 
Kwa wasiofahamu tu ni kwamba Lowasa na Kubenea wana ukaribu wa miaka mingi hivyo inawezekana kabisa anachoongea kina baraka zake
Mshana.Embu tuliza kichwa tafakari kwa kinaa .weka picha ya ccm iliyokwama kisiasa aina fikra mpya tena .na mbinu pekee iliyobaki ni kuzuia chama chochote kisiwapite walipo kwamia kwa kutumia marufuku ya siasa,Polisi,bunge,mahakama,kukosolewa kuanzia vyombo vya habari mpaka mwananchi wa kawaidi .achilia mbali marisasi na kutekana .embu tafakari alafu linganisha na uamuzi wa Maalimu Seifu wakati ule na Ccm na Cdm wakati huu tulio nao
 
Ni vyema Saed Kubenea akajikita kwenye taaluma yake iliyopelekea akamwagiwa tindikali, mbali na hilo binafsi natambua bila shaka Kubenea ni mojawapo wa wanufaikaji wa pesa alizozitoa Edo.
 
Tuliwahi shauri chadema kuwa siasa za harakati hazifai. Ilifikia hatua JK aliita chadema ni mkusanyiko wa wana harakati na si wanasiasa. Ona Leo Magufuli kabeba agenda zao zote za kiharakati kitu ambacho huko nyuma ilikua adimu kumsikia mtu wa hadhi ya Rais akitamka neno fisadi!! Leo Magufuli kabeba agenda ya ufisadi... kabeba agenda za "tunaibiwa madini" kabeba agenda ya tumbua tumbua ili kuzima ile hoja ya "udhaifu"

Shida ni kuwa Magufuli kabeba uanaharakati sasa wanashindwa tembea na bit!!
Utapataje tume huru, katiba mpya, tra, tiss na polisi huru bill kuwa mwanaharakati? Magufuli hajabeba uanaharakati Bali ameugandamiza Sana kwa kuwaua wanaharakati na kudampu miili yao cocobeach na pia amezuia na kupiga marufuki mikutano ya kisiasa na majukwaa mengine yote yanayowakutanisha wanaharakati
 
Nikweli kuna mambo mengi yanayo mkabili lowassa ktk binafsi yake, ila kwanini asi wasiliane na uongoz wa cdm, ili iwe ziara ambayo baadaye inakuwa ni rahisi kuwapa majibu wa tanzania?*
 
Hilo halina shida maana hakuianzisha cdm yeye bali aliikuta tena ikiwa kwenye hali nzuri ile mbaya. Lakini baada ya yeye kuingia hapo ndio chama kikaanza kuingia nuksi. Aonyeshe kiwango cha mauziano aliyofanya tena kwa EFD receipt na terms za hiyo biashara, wanachama na sisi washabiki tuonyeshwe. Kisha tutaamua tulipe kulingana na faida aliyoingiza huku tukipima madhara aliyoiletea cdm. Ila kama alifanya biashara ya kitapeli itabidi aondoke na waliopeana naye hizo hela. Una lingine?
Easier said than done.
 
Kupishana mawazo na kutofautiana na msimamo wa mwenyekiti hii ndio demokrasia tunsyoitaka.

Hatutaki akili za kiccm wote muwe kama treni kinapoelekea kichwa mabehewa yote yanafuata.

Ccm hakuna mwenye jeuri wala uthubutu wa kutofautiana na mwenyekiti wao, hawa ni wafu.

Hii ndio demokraia tunayoitaka watu kutofautiana mawazo na mitazamo. Siyo one size fit all.
Mbona membe, nape, bashe etc wametofautiana sana na Magu.
Lakini you was complaining kwanini wale wabunge wasimuunge mkono wakiwa chadema. Sasa Lowasa amemuunga mkono akiwa chadema, mnalalamika
 
Hizo siasa shindani za kukosoana nendeni mkazifanye Somalia.
Unafikir somalia hapajawahi kuwa na amani? Unafikiri walianza siku moja kufika walipofika? Endelea kuamini kuwa yanayotokea somalia hapa hayawezekani ukidhani una mapolisi na wanajeshi wa kutosha tena wanaouwawa kama vifaranga huko mkuranga na kongo
 
Unafikir somalia hapajawahi kuwa na amani? Unafikiri walianza siku moja kufika walipofika? Endelea kuamini kuwa yanayotokea somalia hapa hayawezekani ukidhani una mapolisi na wanajeshi wa kutosha tena wanaouwawa kama vifaranga huko mkuranga na kongo
Mbona unaanza kuweweseka?
 
Kubenea umeeleza vizuri lakini umetupa mfano wa Malim Seif na Karume katika kumbukumbu zangu Seif hakusimama na kuongea na media. Tatizo wa wanachadema hawatendewi haki katika nchi yao.

CCM wajanja sana. Walichokuwa wanatafuta kwa CDM ni kucheza na akili za wanachadema. Angalia igizo lote pale Ikulu mpaka Lowasa a naingia kwenye gari. Ina maana walimwita ili wapate kitu fulani kutoka UKAWA na MZEE wetu hakutambua ya kuwa wanachadema wanahasira namna hii.

Wangekuwa wamemwita kujadili mambo ya maendeleo wasinge ambatana nae vile na kupiga mapicha wakati wanajua kuna mambo ya kurekebisha kati ya Serikali na Ukawa.

Tuangalie wapambe wa CCM walivyolipokea kama Msukuma, Gambo na wengineo. Yaani nikama vile wanamsubiria Lowasa kwa hamu kubwa au wanatafuta amani fulani kwa Ukawa ili ionekane kwamba watanzania tunashirikiana.

Lengo langu ni kwamba Mbowe ndiye M/kiti wa chama na ametoa tamko la chama na tumelisikia. Sisi tuendelee kulikazia lile tamko mpaka hapo atakapofunguka na kueleza kilichotokea mpaka akaongee hayo maneno na kwa Nini alienda bila kuwajulisha viongozi wa Ukawa hata kwa simu.

Wala haina haja ya kumtajataja tena. Punguzeni hasira na haina haja ya kumfukuza tutapasua chama tumwache kama mwanachama na uongozi watahangaika nae kama Shibuda alivyoondoka bila kupasua chama. Ila na sisi tuangalie mzalendo wa Kweli 2020.
 
Back
Top Bottom