Kubenea: Lowassa ameonesha njia

Kubenea: Lowassa ameonesha njia

Leo hii kubenea wa kusema mazuri kuhusu lowassa .. nikikumbuka kipindi kile gazeti lilivokuwa likimnanga
 
Saed Kubenea

HATUA ya Edward Lowassa, waziri mkuu mstaafu na mgombea urais katika uchaguzi mkuu wa 2015 ya kukutana na Rais John Magufuli, imezusha taharuki ndani na nje ya chama chake.

Kinacholeta taharuki, ni kauli zake kuhusiana na utawala wa Magufuli. Binafsi, nimewasikiliza wote.

Hata hivyo, naomba niseme machache.
Kati ya mwaka 1995 hadi 2010, Zanzibar ilikumbwa na mkwamo mkubwa wa kisiasa.

Ndani ya visiwa hivyo, uhasama ulitalamaki. Fitina na maonevu mengine lukuki - yalikuwa yameshamiri.

Jemedari la kisiasa Visiwani, Maalim Seif Sharif Hamad, aliamua kukutana na hasimu wake mkuu kisiasa, Rais Amani Abeid Karume.

Mkutano kati ya Seif na Karume, ulifanyika wakati mamia ya wananchi wa Pemba wakiwa ukimbizini nje ya nchi.

Aidha, wakati Maalim anakutana na Karume, makumi ya akina mama walikuwa wamebakwa na kulawitiwa na watu wengine kadhaa walikuwa wamefunguliwa kesi za jinai mahakamani.

Si hivyo tu: Mamia ya wananchi, hasa wafuasi wa CUF walikuwa wamefutwa kazi serikalini.

Wengine kadhaa, wakiharibiwa mali zao, yakiwamo majumba, mashamba na baadhi wakiwa wameachwa wajane kutokana na mateso waliyopata wenza wao.

Maalim alikutana na Karume kimya kimya na bila kushirikisha wenzake kwenye chama.

Alikutana na kuzungumza na Karume na kukataa katakata kutaja kile walichojaliana.

Ilidaiwa kuwa Maalim alichukua hatua hiyo kwa kuwa alihofia kuwa kueleza mapema kile walichojadili; na au wanachokwenda kujadiliana, kungevuruga mikakati yake.

Hata Rais Karume naye hakueleza kuwapo mkutano na Maalim Seif. Hakueleza walichotaka kukizungumza na wala hakusema kile walichokijadili baada ya mkutano wao.

Mkutano kati ya viongozi hawa wawili ulifanyika wakati tayari vyama vya CUF na CCM, vikiwa vimefunga miafaka mitatu ya kisiasa bila mavuno kwa CUF.

Mwasisi wa mazungumzo kati ya Karume na Seif, ni mzee Nassoro Moyo, Eddy Lyami na Mansour Hamid.

Baada ya taarifa za kuwapo mkutano huo kuvuja, wafuasi wa CUF walikuja juu. Walimtukana Maalim Seif matusi ya nguoni.

Nakumbuka katika mkutano mmoja wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kibandamaiti, wafusi wa chama hicho, walimtupia mawe na maganda ya machungwa kiongozi wao huyo.

Kuna mengi ya kueleza juu ya tukio hilo. Lakini itoshe tu kusema, mkutano kati ya Maalim na Karume ndio uliozaa Katiba mpya ya Zanzibar na ndio msingi wa CUF kuingia serikalini katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Hivyo basi, naifananisha ziara ya Lowassa ya jana na tukio hilo la mwaka 2010 Visiwani.

Lowassa amekutana na Magufuli, kipindi ambacho chama chake kiko kwenye mkwamo. Hakiwezi kufanya mkutano wa hadhara.

Kimefika mbali zaidi; sasa hata uchaguzi mdogo hakiwezi kushiriki.

Baadhi ya viongozi wakuu chama badala ya kuwaongoza wanachama, nao wamegeuka kuwa walalamishi.

Ni kwa sababu, CHADEMA ya mwaka 2010 hadi 2014 ya maandamano na mikutano haipo tena.

Katika muktadha huo, njia pekee ya kutoka hapa tulipo ni kujadiliana adui yako. Lowassa amefungua njia hiyo. Ni vema ikatumiwa.

Mwisho
Kubenea kumbe wakati mwingine zimoe,hongera sana kwa kuliona hili.
 
lowasa alikwenda ikulu kwa maslahi binafsi kubenea asifanye maigizo. hakuna zaidi hapo
 
Hilo halina shida maana hakuianzisha cdm yeye bali aliikuta tena ikiwa kwenye hali nzuri ile mbaya. Lakini baada ya yeye kuingia hapo ndio chama kikaanza kuingia nuksi. Aonyeshe kiwango cha mauziano aliyofanya tena kwa EFD receipt na terms za hiyo biashara, wanachama na sisi washabiki tuonyeshwe. Kisha tutaamua tulipe kulingana na faida aliyoingiza huku tukipima madhara aliyoiletea cdm. Ila kama alifanya biashara ya kitapeli itabidi aondoke na waliopeana naye hizo hela. Una lingine?
Kama hamrudishi chenji yake basi yeyote atakayejitokeza kujifanya kuwa msemaji wa chama basi yatampata yaliyompata [HASHTAG]#lissumsaliti[/HASHTAG]
Chenji lazima irudi, la sivyo chama kitakufa. Mnapenda kula vya bure siyo?!
 
Hata mkileta maelezo marefu vipi, Lowassa bado sio mtu sahihi kuwepo cdm. Anaweza kurudi tu ccm na kutoa huo ushauri wake mzuri akiwa huko. Ama anaweza kwenda hata TLP na kuongeza nguvu huko na hizo siasa zake. Watavuna watu wengi tu tunaombiwa walimpa kura mpaka cdm ikapata wabunge wengi.
Ndo mmejua leo?
 
Kama hamrudishi chenji yake basi yeyote atakayejitokeza kujifanya kuwa msemaji wa chama basi yatampata yaliyompata [HASHTAG]#lissumsaliti[/HASHTAG]
Chenji lazima irudi, la sivyo chama kitakufa. Mnapenda kula vya bure siyo?!

Hatupendi kula la vya bure mama Regina, ila muambie mumeo mjini hakutaki papara matokeo yake ndio haya kaingizwa mjini.
 
Saed Kubenea

HATUA ya Edward Lowassa, waziri mkuu mstaafu na mgombea urais katika uchaguzi mkuu wa 2015 ya kukutana na Rais John Magufuli, imezusha taharuki ndani na nje ya chama chake.

Kinacholeta taharuki, ni kauli zake kuhusiana na utawala wa Magufuli. Binafsi, nimewasikiliza wote.

Hata hivyo, naomba niseme machache.
Kati ya mwaka 1995 hadi 2010, Zanzibar ilikumbwa na mkwamo mkubwa wa kisiasa.

Ndani ya visiwa hivyo, uhasama ulitalamaki. Fitina na maonevu mengine lukuki - yalikuwa yameshamiri.

Jemedari la kisiasa Visiwani, Maalim Seif Sharif Hamad, aliamua kukutana na hasimu wake mkuu kisiasa, Rais Amani Abeid Karume.

Mkutano kati ya Seif na Karume, ulifanyika wakati mamia ya wananchi wa Pemba wakiwa ukimbizini nje ya nchi.

Aidha, wakati Maalim anakutana na Karume, makumi ya akina mama walikuwa wamebakwa na kulawitiwa na watu wengine kadhaa walikuwa wamefunguliwa kesi za jinai mahakamani.

Si hivyo tu: Mamia ya wananchi, hasa wafuasi wa CUF walikuwa wamefutwa kazi serikalini.

Wengine kadhaa, wakiharibiwa mali zao, yakiwamo majumba, mashamba na baadhi wakiwa wameachwa wajane kutokana na mateso waliyopata wenza wao.

Maalim alikutana na Karume kimya kimya na bila kushirikisha wenzake kwenye chama.

Alikutana na kuzungumza na Karume na kukataa katakata kutaja kile walichojaliana.

Ilidaiwa kuwa Maalim alichukua hatua hiyo kwa kuwa alihofia kuwa kueleza mapema kile walichojadili; na au wanachokwenda kujadiliana, kungevuruga mikakati yake.

Hata Rais Karume naye hakueleza kuwapo mkutano na Maalim Seif. Hakueleza walichotaka kukizungumza na wala hakusema kile walichokijadili baada ya mkutano wao.

Mkutano kati ya viongozi hawa wawili ulifanyika wakati tayari vyama vya CUF na CCM, vikiwa vimefunga miafaka mitatu ya kisiasa bila mavuno kwa CUF.

Mwasisi wa mazungumzo kati ya Karume na Seif, ni mzee Nassoro Moyo, Eddy Lyami na Mansour Hamid.

Baada ya taarifa za kuwapo mkutano huo kuvuja, wafuasi wa CUF walikuja juu. Walimtukana Maalim Seif matusi ya nguoni.

Nakumbuka katika mkutano mmoja wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kibandamaiti, wafusi wa chama hicho, walimtupia mawe na maganda ya machungwa kiongozi wao huyo.

Kuna mengi ya kueleza juu ya tukio hilo. Lakini itoshe tu kusema, mkutano kati ya Maalim na Karume ndio uliozaa Katiba mpya ya Zanzibar na ndio msingi wa CUF kuingia serikalini katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Hivyo basi, naifananisha ziara ya Lowassa ya jana na tukio hilo la mwaka 2010 Visiwani.

Lowassa amekutana na Magufuli, kipindi ambacho chama chake kiko kwenye mkwamo. Hakiwezi kufanya mkutano wa hadhara.

Kimefika mbali zaidi; sasa hata uchaguzi mdogo hakiwezi kushiriki.

Baadhi ya viongozi wakuu chama badala ya kuwaongoza wanachama, nao wamegeuka kuwa walalamishi.

Ni kwa sababu, CHADEMA ya mwaka 2010 hadi 2014 ya maandamano na mikutano haipo tena.

Katika muktadha huo, njia pekee ya kutoka hapa tulipo ni kujadiliana adui yako. Lowassa amefungua njia hiyo. Ni vema ikatumiwa.

Mwisho
Umetumia mfano mzuri kbs naomba tujifunze pia kupitia huo mfano wako ndugu yngu jee wapemba walifukuzwa makazini walirudishwa je wapemba waliokuwa njee km wakimbizi wamerudi kifupi kitu ambacho umekisahau hapo Maalim Seif alikwenda kwa ajiri ya maslahi yke na familia yke ndicho nikionacho kwa mzee wngu lowasa ngoja tuone ila nina hakika baada wiki mbili mkwewe atapewa dhamana miradi yke iliyopingwa pin watalengeza kifupi tunaweza kurudi kwenye kitabu cha the are beautifuly one's are not yet born sina na ilo jina la kitabu naweza kuwa nmechapia ila kitabu hicho kinaeleza mengi khs waafrika na Siasa zetu za matumbo yetu...
 
Back
Top Bottom