KUB Mbowe anapwaya bungeni?

KUB Mbowe anapwaya bungeni?

Dah kwa majibu haya ya Waziri Mkuu hakika Mbowe yupo uchi wa mnyama
 
acheni siasa za matukio!
awamu hii ni siasa za maswala! mkiwa rigid watu hawata waelewa!
 
HOJA ZA MBOWE BUNGENI ZAJIBIWA

#Mosi; "Kwamba hakuna mpango wa maendeleo wa serikali hadi sasa. Yani serikali inaendeshwa kwa matukio. Hakuna mpango mkakati unaotumika kuongoza masuala mbalimbali ya serikali. Yani Rais Magufuli anataka Tanzania ifike mahali ambapo hata yeye hajui ni wapi. Washauri wake wameshindwa kumpa 'Focus'."
JIBU: Mbowe amekurupuka vibaya huenda kuliko kiongozi yeyote wa upinzani Bungeni ktk dunia hii:Tanzania ina Dira ya Taifa 2025 ambayo Mbowe anaijua na inaendelea kutuongoza kuhusu kule tunakotaka kwenda.2.Tanzania ina katiba ambayo Mbowe anaijua na ndiyo inayoongoza masuala ya nchi kwa sasa na ndiyo iliyomuingiza hata yeye Bungeni Dodoma alipo sasa. 3.Tanzania ina Bajeti ya mwaka ambayo Mbowe na wenzake walishiriki kuipitisha June mwaka jana na ndiyo Rais Magufuli anayoitumia kuendesha nchi kwa sasa akiongeza na ubunifu na uchapakazi wake.4.Rais anatokana na CCM na ana ilani anayoitekeleza na ambayo aliiuza kwa wananchi wakaikubali na wakamwamini 5.Chini ya Sheria ya Majukumu ya Mawaziri na nguvu alizopewa na Katiba Rais anaendesha nchi,anateua watendaji kumsaidia na anawapa makukumu ya kuyatekeleza.5.Mpango wa miaka 5 wa Kwanza wa Maendeleo bado unatekelezwa na unaisha Juni mwaka huu na Mpango mpya umeshawasilishwa Bunge-kwa haya tu machache na nchi inavyozidi kwenda ikiwa na amani na utulivu na wananchi wakiwa na matumaini tele, ukiachilia mbali, sheria na taasisi mbalimbali na mipango mingine ya mda wa kati inayoendelea kutekelezwa, kwa mtu kusema Rais JPM hana Mpango na eti anaongozwa na matukio ni kauli inayoweza kutoka tu kwa mtu aliye katika usingizi mnono tena wa pono!!!
#pili "kwamba Waandishi wa habari kuzuiwa kuingia Bungeni ni ukiukwaji wa haki za msingi za kikatiba. Kwa mujibu wa Katiba ya nchi ibara ya 18 na 19 haki ya mtu kupata habari."
Jibu: Kwanza si kweli na anajipotosha.Hakuna mwandishi aliyezuiwa kuingia Bungeni. Kama ni mjadala wa live huu kwanza kimsingi ulishakwisha..kuurejesha tena ndio mfano halisi wa watu wanaokwenda kwa matukio-Ukawa hapa wamedhihirisha wanakwenda na matukio hawana plan yoyote kwa sasa-wamevurugwa.Lakini juu ya hoja kuwa Ibara tajwa inatoa uhuru wa habari ni sawa lakini Je,uhuru wa habari ulioelezwa hapo una maana anayotaka Mbowe tuamini kuwa hauna mipaka wala ukomo...kama anataka tuamini hivyo Je,vikao vya ndani vya Chadema kwa nini havioneshwi live kwa manufaa ya nchi,demokrasia lakini pia na kwa manufaa ya wanachama wa Ukawa.Mbowe aache kwenda na matukio.Bunge limeunda studio waandishi wamepunguziwa gharama a kuweka kila TV kamera zake na inatuma picha za kisasa kabisa lakini pia wanahabari wa vyombo vyote wapo Bungeni na kila siku wanaandika matukio.Mbowe aache siasa za matukio haki ya kupata habari sio lazima iwe live bali mabingwa wa eneo hilo na taaluma hiyo ya habari ambayo yeye haijui wanapigania habari zisibinywe baas na sio lazima iwe live...kama Mbowe anabisha hajakurupuka ataje kifungu na akinukuu kinachosema habari lazima iwe live.
#Tatu; "Kupinga maamuzi ya Ofisi ya Spika kupunguza matumizi ya bajeti ya Bunge na kurudisha fedha serikalini bila kushirikisha bunge. Hata kama Spika alitaka kupunguza bajeti ya Bunge alipaswa kushirikisha Bunge kwanza ili wajadili na kufikia makubaliano, sio kujiamulia kibabe.!

Jibu: Hoja hii nayo ni muflisi kabisa na inaweza kujibiwa kwa ujumla wake kwamba Bajeti iliyopitishwa na inayoyumika sasa ya Serikali ya Awamu ya 5 usimamizi na utekelezaji wake uko chini ya Rais na Waziri wa Fedha.Sheria ya Usimamizi wa Bajeti (Appropriation Act) na kwa hapa nazungumzia ya 2015 kifungu cha 6 Waziri wa Fedha anapewa mamlaka (baada ya maagizo au mashauriano ya ndani Serikalini) kuhamisha matumizi ya fedha yoyote au kuzuia kutumika kwa fedha yoyote iliyotengwa ktk Bajeti kisha akaihamishia katika matumizi mengine ya Serikali.Tofauti na changa la macho analotaka kutuletea Bw. Mbowe kwamba kwa mfano wa fedha za Bunge zilizopelekwa ktk matumizi mengine eti Bunge lingejadili kwanza kifungu hiki cha 6 kinamsuta kinasema tofauti
Katiba unayoiongelea mnaivunja kila Siku kwa matamko yasiyofuata Sheria, kanuni na taratibu za nchi. Magufuli anaingilia Mamlaka ya Bunge kwa kubadili matumizi ya fedha bila kibali cha Bunge. Anawaacha kina Chenge wa Escrow, Lugumi, Kiwira, Meremeta, Kagoda, Kivuko Chakavu, Nyumba za Serikali. Halafu mnasema MNA dira.

CCM ina Kansa ya Rushwa na Ufisadi.
 
Kwakweli nikisoma majibu ya hawa wana CCM mufilisi wa humu JF nikajumlisha na hayo majibu ya hovyo aliyotoa Kassim Majaliwa nikajumlisha na michango ya Joseph Msukuma, Halima Bulembo na Juma Nkamia najiridhisha kuwa CCM ni wamoja kwenye vihoja na CCM ni ileile!
 
Kama haya ni majibu ya Majaliwa basi tuna tatizo kubwa la Uongozi katika Awamu ya 5
 
Sitaki kuamini kama haya kweli ni majibu ya waziri mkuu Kasim M
 
KWELI WW KILAZA,KATIBA INAVUNJWA UNACHEKELEA JAPO KATIBA YENYEWE MBOVU JAPO HAO MACCM WANGEIHESHIMU LAKINI WANATAMANI WAIFUTILIE MBALI.
Huyo ni kati ya kilaza ambaye huwa kila post yake huwa hatumii angalau akili ya kuzaliwa nayo, yeye kikubwa ni mkono kwenda kinywani
 
Iko kishabiki toa ilkitu yako

Bunge lenyewe la kichoyo

Fanyeni mnavyoweza
 
Sioni upanguzi wa hoja wala hoja za maana katika maelezo haya zaidi ya ujinga mwingi na upumbavu ndani yake.

Ili ionekane kapanguwa weka vifungu halisi vya katiba badala ya kuname kifungu ilhali hujakiandika.

ujinga nikazi.
Huyo simiyu yetu ni sawa na mwana futuhi tu
 
Mbowe ni msanii tu!!;maisha ya siasa ya ujanjaujanja tuu!!!;imekula kwao!!
 
Back
Top Bottom