KUB Mbowe anapwaya bungeni?

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,999
Heri ya Muungano wadau.

Nimejiuliza tu,nikaona ni vema pia nipate maoni kutoka kwa werevu wa mambo.Ila mimi kwa upande wangu nimeona ya kuwa KUB,Mbowe amepwaya na abadilishwe ili tupate KUB mbadala mwenye weledi.

Na hapa sio jambo la Aibu amwachie Rwakatare Wilfred ambaye alipata kuwa KUB (2000/2005).

Japo kulikuwa na ugumu lakini mara kadhaa aliongoza kambi ya upinzani iliyoweza kuwashawawishi wabunge wa CCM kuunga mkono hoja dhidi ya serikali.

Ikumbukwe tu mara kadhaa KUB wa sasa hayupo "consistent" hili linatokana na sababu kwamba yeye kama kiongozi huyumbishwa na mawazo ya wasaidizi wake yaani hana anachosimamia kama kiongozi,ikitokea Lisu,Kubenea,Mnyika wakatoa ushauri(miluzi) hukosa uamuzi.

Kakosa "Focus" na kutengeneza hoja endelevu ili kuleta matokeo na badala yake anajikita na vijihabari na matukio yasiyo na msingi.

Uwezo wake wa kuchimba ripoti na kuwasilisha mada za kitaalam kwenye hadhira ni mdogo..mara nyingi huongea kwa kufoka foka (povu),hana "details" na mambo mengi ya msingi na sio msomaji.

Ni hayo tu,nipo tayari kukosolewa...nimelazimika kuleta haya kwa sababu KUB ni mtumishi wa umma na analipwa kwa kodi zetu.
 
Sasa ni dhahiri udhaifu wa Mbowe unaonekana wazi......na hii inasababishwa kwa kutokuwepo kwa Dr Slaa
 
Toa boriti kwenye jicho lako ndo utoe kitanzi kwenye jicho na mwenzako. Wapinzan au Mbowe anakuhusu nini?

Acha Mawazo mgando leo ni public holiday naona unataka ulipwe 7 x 2 . Tumekustukia
 
Heri ya Muungano wadau.

Nimejiuliza tu,nikaona ni vema pia nipate maoni kutoka kwa werevu wa mambo.Ila mimi kwa upande wangu nimeona ya kuwa KUB,Mbowe amepwaya na abadilishwe ili tupate KUB mbadala mwenye weledi.Na hapa sio jambo la Aibu amwachie Rwakatare Wilfred ambaye alipata kuwa KUB (2000/2005).Japo kulikuwa na ugumu lakini mara kadhaa aliongoza kambi ya upinzani iliyoweza kuwashawawishi wabunge wa CCM kuunga mkono hoja dhidi ya serikali.

Ikumbukwe tu mara kadhaa KUB wa sasa hayupo "consistent" hili linatokana na sababu kwamba yeye kama kiongozi huyumbishwa na mawazo ya wasaidizi wake yaani hana anachosimamia kama kiongozi,ikitokea Lisu,Kubenea,Mnyika wakatoa ushauri(miluzi) hukosa uamuzi.

Kakosa "Focus" na kutengeneza hoja endelevu ili kuleta matokeo na badala yake anajikita na vijihabari na matukio yasiyo na msingi.

Uwezo wake wa kuchimba ripoti na kuwasilisha mada za kitaalam kwenye hadhira ni mdogo..mara nyingi huongea kwa kufoka foka (povu),hana "details" na mambo mengi ya msingi na sio msomaji.

Ni hayo tu,nipo tayari kukosolewa...nimelazimika kuleta haya kwa sababu KUB ni mtumishi wa umma na analipwa kwa kodi zetu.
Kwani wewe unataka upinzani hapa nchini?
 
lakini siyo mbowe tu,Hata majaliwa kassim amepwaya sana!....Amekacha kipindi cha maswali ya papo kwa waziri mkuu kila alhamisi
 
Sasa ni dhahiri udhaifu wa Mbowe unaonekana wazi......na hii inasababishwa kwa kutokuwepo kwa Dr Slaa
Ni kweli...Mbowe alikuwa bora chini ya Slaa na Zitto..,ndio maana hata kikao cha bunge kilichopita ilibidi amkibilie ZZK baada ya kutowa hoja yenye mashiko.
 
lakini siyo mbowe tu,Hata majaliwa kassim amepwaya sana!....Amekacha kipindi cha maswali ya papo kwa waziri mkuu kila alhamisi
Lazima kunakuwa na Kaimu kiongozi wa shughuli.za serikali,kumbuka Majaliwa ni binadamu huuguwa na hupata dharura.
 
Ukichanganya mambo matatu yafuatayo ndio utaelewa kwa nini amepwaya....

Moja ni aibu ya kumtetea fisadi na kumpa agombee urais ndani ya kipindi kifupi tena bila wanachama wake kuridhia.

Mbili ni kumtosa Think tank wa Chadema Dr Slaa na timu yake.

Tatu ni kiwango chake cha elimu kisichojulikana !
 
na awamu hii ya tano,inahitaji utendaji wenye ubunifu,huwezi kuwa mbunifu kama shule ndogo, elimu f4 f, utapwaya tu hamna namna, utabaki kushabikia mbunge kurushwa huku wananchi hawana dawa mahospitalini
 
Toa boriti kwenye jicho lako ndo utoe kitanzi kwenye jicho na mwenzako. Wapinzan au Mbowe anakuhusu nini? Acha Mawazo mgando leo ni public holiday naona unataka ulipwe 7 x 2 . Tumekustukia
Dogo lazima mjifunze kukubali kukosolewa,jikite kwenye mada.
 
Kitendo cha Zitto kuibuka jana na tamko almost similar na lile la Mbowe linaashiria ombwe la KUB kwenye bunge la awamu ya tano.

yaani zitto aliona Mbowe hajatosha kwa hoja...
 
Watu wengine bwana, wameshikwa na report ya CAG na ndiyo habari ya mjini tangu Jana. Waliokerwa na hali hiyo wana haha kuanzisha mijadala kuhusu Mbowe. Watu wote wapuuzeni kwa kwa sasa tujadili report ya CAG hayo mengine tumesha wahi kuyasikia ama tutayajadili wakati mwingine .
 
Ukichanganya mambo matatu yafuatayo ndio utaelewa kwa nini amepwaya....

Moja ni aibu ya kumtetea fisadi na kumpa agombee urais ndani ya kipindi kifupi tena bila wanachama wake kuridhia.

Mbili ni kumtosa Think tank wa Chadema Dr Slaa na timu yake.

Tatu ni kiwango chake cha elimu kisichojulikana !
Unajuwa bavicha wanajuwa KUB si mtumishi wa umma.
 
Back
Top Bottom