KUB Mbowe anapwaya bungeni?

KUB Mbowe anapwaya bungeni?

Watu wengine bwana, wameshikwa na report ya CAG na ndiyo habari ya mjini tangu Jana. Waliokerwa na hali hiyo wana haha kuanzisha mijadala kuhusu Mbowe. Watu wote wapuuzeni kwa kwa sasa tujadili report ya CAG hayo mengine tumesha wahi kuyasikia ama tutayajadili wakati mwingine .
Mkuu wa kaya naye jana alijitutumua na makatibu tawala ili kufukia ripoti hii lakini wapi!
 
Sasa kama ndo yuko hivyo mbona anawanyima usingizi hapo Lumumba. Bila shaka mtakuwa mpo chini yake ndo maana.
Ccm siku watakapo sikia Mbowe kaachia mikoba ya uenyekiti wanachama wao watawakodeshea helicopter kwenda kutalii china oops ikulu!
 
Lazima kunakuwa na Kaimu kiongozi wa shughuli.za serikali,kumbuka Majaliwa ni binadamu huuguwa na hupata dharura.
Ok so ni bahati mbaya kuwa maradhi na dharura humfika siku za alhamisi tu kukiwa na maswali na majibu bungeni?sawa ume eleweka.
 
Dogo lazima mjifunze kukubali kukosolewa,jikite kwenye mada.
Hao ndio wale vijana umri wa kina diamond na ali kiba, wako very irresponsible, hauwezi kusense majukumu kwenye maongezi yao siku zote wanakimbilia kwenye ufundi wa matusi na kejeli za kipumbavu.
 
Ok so ni bahati mbaya kuwa maradhi na dharura humfika siku za alhamisi tu kukiwa na maswali na majibu bungeni?sawa ume eleweka.
Toka bunge lianze kumekuwa na alhamisi ngapi?..hizi ndio siasa mbovi za kurukia vijihabari zisizo na mantiki....!
 
Jikite kwenye mada dogo!
Sikiliza dogo, binafsi hapa sioni hoja bali porojo tu. Unajua sometimes hata maofisini watu wakiishiwa kazi za kufanya baadhi yao hucheza karata kwenye Pc's zao. Ndicho unachokifanya wewe hapa jamvini.
Ni bora ukajikita kwenye kuuza tshirts na kofia za chama hapo Lumumba.
 
Sikiliza dogo, binafsi hapa sioni hoja bali porojo tu. Unajua sometimes hata maofisini watu wakiishiwa kazi za kufanya baadhi yao hucheza karata kwenye Pc's zao. Ndicho unachokifanya wewe hapa jamvini.
Ni bora ukajikita kwenye kuuza tshirts na kofia za chama hapo Lumumba.
kwa hiyo unacheza karata?...pumzi yako ineshakata,huna hoja.
 
Kupinga kuwa uwezo wake ni mkubwa ufinyu wa kifikra.
Ni kweli uwezo wake ni mdogo. Na kusema abadilishwe wala siyo zambi.
ANA UWEZO MDOGO WA KUJENGA HOJA
 
Hao mkuu wasikuumize kichwa.Wametumwa toka Lumumba wajaribu kwa njia za kupitia mitandao kuwasahaulisha wananchi kujadili hoja nzito za CAG kuhusu taifa linavyoangamizwa kwa ufisadi eti tujikite kwenye hoja dhaifu ya kumjadili KUB wa upinzani bungeni.Wenye mamlaka na ukawa wanaridhishwa na uwakilishi wake wao Lumumba wanahusikaje? Tumejanjaruka na mbinu hizi za serikali na chama chao kuwasahaulisha wananchi kwa hoja dhaifu za vikombe vya babu n.k.Hata hivyo leo serikalini ni sikukuu wanahaki ya kulipwa mara mbili ila wajue wananchi tulishtuka siku nyingi kwa sasa tunajadili nchi inavyozidi kuangamizwa na mafisadi na sio vinginevyo.POLENI SANA.
Nchi inaangamia kule karatu na Hai chini ya usimamizi wa Chadema
 
Heri ya Muungano wadau.

Nimejiuliza tu,nikaona ni vema pia nipate maoni kutoka kwa werevu wa mambo.Ila mimi kwa upande wangu nimeona ya kuwa KUB,Mbowe amepwaya na abadilishwe ili tupate KUB mbadala mwenye weledi.

Na hapa sio jambo la Aibu amwachie Rwakatare Wilfred ambaye alipata kuwa KUB (2000/2005).

Japo kulikuwa na ugumu lakini mara kadhaa aliongoza kambi ya upinzani iliyoweza kuwashawawishi wabunge wa CCM kuunga mkono hoja dhidi ya serikali.

Ikumbukwe tu mara kadhaa KUB wa sasa hayupo "consistent" hili linatokana na sababu kwamba yeye kama kiongozi huyumbishwa na mawazo ya wasaidizi wake yaani hana anachosimamia kama kiongozi,ikitokea Lisu,Kubenea,Mnyika wakatoa ushauri(miluzi) hukosa uamuzi.

Kakosa "Focus" na kutengeneza hoja endelevu ili kuleta matokeo na badala yake anajikita na vijihabari na matukio yasiyo na msingi.

Uwezo wake wa kuchimba ripoti na kuwasilisha mada za kitaalam kwenye hadhira ni mdogo..mara nyingi huongea kwa kufoka foka (povu),hana "details" na mambo mengi ya msingi na sio msomaji.

Ni hayo tu,nipo tayari kukosolewa...nimelazimika kuleta haya kwa sababu KUB ni mtumishi wa umma na analipwa kwa kodi zetu.
 
Kitendo cha Zitto kuibuka jana na tamko almost similar na lile la Mbowe linaashiria ombwe la KUB kwenye bunge la awamu ya tano.

yaani zitto aliona Mbowe hajatosha kwa hoja...
Na hapo ndio unapoona ZITTO ni kifaa haswa kwenye siasa za TZ.
uko sawa mkuu.
 
Back
Top Bottom