KUB Mbowe anapwaya bungeni?

KUB Mbowe anapwaya bungeni?

Hujitambui dogo acha ushabiki katiba ni sheria mama unapoivunja ni sawa na kumchungulia mzazi wako bafuni.
Humjui Lizabon wewe, mbele ya pesa kumchungulia mama yake bafuni is not a big deal
 
HOJA ZA MBOWE BUNGENI ZAJIBIWA

#Mosi; "Kwamba hakuna mpango wa maendeleo wa serikali hadi sasa. Yani serikali inaendeshwa kwa matukio. Hakuna mpango mkakati unaotumika kuongoza masuala mbalimbali ya serikali. Yani Rais Magufuli anataka Tanzania ifike mahali ambapo hata yeye hajui ni wapi. Washauri wake wameshindwa kumpa 'Focus'."
JIBU: Mbowe amekurupuka vibaya huenda kuliko kiongozi yeyote wa upinzani Bungeni ktk dunia hii:Tanzania ina Dira ya Taifa 2025 ambayo Mbowe anaijua na inaendelea kutuongoza kuhusu kule tunakotaka kwenda.2.Tanzania ina katiba ambayo Mbowe anaijua na ndiyo inayoongoza masuala ya nchi kwa sasa na ndiyo iliyomuingiza hata yeye Bungeni Dodoma alipo sasa. 3.Tanzania ina Bajeti ya mwaka ambayo Mbowe na wenzake walishiriki kuipitisha June mwaka jana na ndiyo Rais Magufuli anayoitumia kuendesha nchi kwa sasa akiongeza na ubunifu na uchapakazi wake.4.Rais anatokana na CCM na ana ilani anayoitekeleza na ambayo aliiuza kwa wananchi wakaikubali na wakamwamini 5.Chini ya Sheria ya Majukumu ya Mawaziri na nguvu alizopewa na Katiba Rais anaendesha nchi,anateua watendaji kumsaidia na anawapa makukumu ya kuyatekeleza.5.Mpango wa miaka 5 wa Kwanza wa Maendeleo bado unatekelezwa na unaisha Juni mwaka huu na Mpango mpya umeshawasilishwa Bunge-kwa haya tu machache na nchi inavyozidi kwenda ikiwa na amani na utulivu na wananchi wakiwa na matumaini tele, ukiachilia mbali, sheria na taasisi mbalimbali na mipango mingine ya mda wa kati inayoendelea kutekelezwa, kwa mtu kusema Rais JPM hana Mpango na eti anaongozwa na matukio ni kauli inayoweza kutoka tu kwa mtu aliye katika usingizi mnono tena wa pono!!!
#pili "kwamba Waandishi wa habari kuzuiwa kuingia Bungeni ni ukiukwaji wa haki za msingi za kikatiba. Kwa mujibu wa Katiba ya nchi ibara ya 18 na 19 haki ya mtu kupata habari."
Jibu: Kwanza si kweli na anajipotosha.Hakuna mwandishi aliyezuiwa kuingia Bungeni. Kama ni mjadala wa live huu kwanza kimsingi ulishakwisha..kuurejesha tena ndio mfano halisi wa watu wanaokwenda kwa matukio-Ukawa hapa wamedhihirisha wanakwenda na matukio hawana plan yoyote kwa sasa-wamevurugwa.Lakini juu ya hoja kuwa Ibara tajwa inatoa uhuru wa habari ni sawa lakini Je,uhuru wa habari ulioelezwa hapo una maana anayotaka Mbowe tuamini kuwa hauna mipaka wala ukomo...kama anataka tuamini hivyo Je,vikao vya ndani vya Chadema kwa nini havioneshwi live kwa manufaa ya nchi,demokrasia lakini pia na kwa manufaa ya wanachama wa Ukawa.Mbowe aache kwenda na matukio.Bunge limeunda studio waandishi wamepunguziwa gharama a kuweka kila TV kamera zake na inatuma picha za kisasa kabisa lakini pia wanahabari wa vyombo vyote wapo Bungeni na kila siku wanaandika matukio.Mbowe aache siasa za matukio haki ya kupata habari sio lazima iwe live bali mabingwa wa eneo hilo na taaluma hiyo ya habari ambayo yeye haijui wanapigania habari zisibinywe baas na sio lazima iwe live...kama Mbowe anabisha hajakurupuka ataje kifungu na akinukuu kinachosema habari lazima iwe live.
#Tatu; "Kupinga maamuzi ya Ofisi ya Spika kupunguza matumizi ya bajeti ya Bunge na kurudisha fedha serikalini bila kushirikisha bunge. Hata kama Spika alitaka kupunguza bajeti ya Bunge alipaswa kushirikisha Bunge kwanza ili wajadili na kufikia makubaliano, sio kujiamulia kibabe.!

Jibu: Hoja hii nayo ni muflisi kabisa na inaweza kujibiwa kwa ujumla wake kwamba Bajeti iliyopitishwa na inayoyumika sasa ya Serikali ya Awamu ya 5 usimamizi na utekelezaji wake uko chini ya Rais na Waziri wa Fedha.Sheria ya Usimamizi wa Bajeti (Appropriation Act) na kwa hapa nazungumzia ya 2015 kifungu cha 6 Waziri wa Fedha anapewa mamlaka (baada ya maagizo au mashauriano ya ndani Serikalini) kuhamisha matumizi ya fedha yoyote au kuzuia kutumika kwa fedha yoyote iliyotengwa ktk Bajeti kisha akaihamishia katika matumizi mengine ya Serikali.Tofauti na changa la macho analotaka kutuletea Bw. Mbowe kwamba kwa mfano wa fedha za Bunge zilizopelekwa ktk matumizi mengine eti Bunge lingejadili kwanza kifungu hiki cha 6 kinamsuta kinasema tofauti
chapa kazi PM
 
Kwa ufupi chadomo hakina kiongozi ni chama cha wapiga dili tu na Mimi huwa nawashangaa maprofesa walioko huko wanaongozwa na huyo kilaza Mbowe.
 
Mjibu mwenzako kwa hoja
sasa bunge liliopita mliahirisha mpango gani na mlipeleka wa nini kama mpango wa 2015/25 upo?

bahati nzuri mnatumia weakness ya IQ ndogo ya watanganyika kufikia malengo yenu! Maana hata wewe mtoa maada umesahau what transpired in the last session! Kikatiba inabidi before anything kama utawala mpya mtoe muelekeo, mliutoa mkagundua una makosa sasa mnakuja na blabla nyingine?
 
Sitashangaa Rais ajaye mwaka 2025 akawa Majaliwa
Laana ya kumpiga mzee warioba bado inakuandama na itaendelea hadi kwa kizazi chako choote
Tehetehetehe. Pole sana ndugu. Mlitaka kumchonganisha Makonda na Mzee Warioba. Aibu imewarudia wenyewe
 
PM nae walewale tu, hivi vikao vya ndani vya chadema ndo analinganisha na vikao vya bunge, kweli hii nchi safari bado ndeeeeefu mno
 
Kama kweli Majaliwa ndo kasema haya nasikitika sana kuongozwa na watu wenye uwezo mdogo kama hawa.
 
sasa bunge liliopita mliahirisha mpango gani na mlipeleka wa nini kama mpango wa 2015/25 upo?

bahati nzuri mnatumia weakness ya IQ ndogo ya watanganyika kufikia malengo yenu! Maana hata wewe mtoa maada umesahau what transpired in the last session! Kikatiba inabidi before anything kama utawala mpya mtoe muelekeo, mliutoa mkagundua una makosa sasa mnakuja na blabla nyingine?
Duh. Kama uelewa wenyewe wa wana UKAWA ndo huu bora kuwa marehemu kuliko kuwa mfuasi wa UKAWA
 
Anayezungumza kwa hoja ajibiwe kwa hoja...nadhani kwa kufanya. Hivyo tutarudisha heshima ya JF
 
Kwani wewe ulitaka Waziri Mkuu amoe majibu gani DJ Ziro?
kwa IQ hapo wewe mwenyewe unajua kama Mbowe alikuwa DJ mwingine alikuwa mcheza mziki nqni zaidi? hebu wekeni hoja sio vioja hapa ndugu, wewe wa kitambo hapa tunategemea u improve kwenye ujengaji hoja! you never change always the same huku mvi zinakuota mkuu!
 
Ukapimwe kwanza wewe unaye endelea kukiunga mkono chama kinacho kumbatia majizi ya rasilimali za taifa
Ungemuuliza BOSI wako anayelalamika hadi kwenye haki za binaadamu akiyatetea hayo hayo majizi ambayo mengi sasa yamehamia chadema. Hataku kutumbua majipu kwa nini?
 
Duh. Kama uelewa wenyewe wa wana UKAWA ndo huu bora kuwa marehemu kuliko kuwa mfuasi wa UKAWA
Wewe unanijua mkongwe humu niliwaachia vijana muongee nao watoe elimu lakini kikosi cha vichwamaji mlichokiongiza kimenorudisha. Nilikuwa guest lakini huu uovyo mnaouandika umenirudisha.

Tulikuachia ukomae na uweze kujenga hoja bado tuu uko kwenye zile hoja za tindikali zako? umezeeka wewe na uzee dawa!
 
Kwa ufupi chadomo hakina kiongozi ni chama cha wapiga dili tu na Mimi huwa nawashangaa maprofesa walioko huko wanaongozwa na huyo kilaza Mbowe.
Eti hiyo Mmawia. Anajifanya kutuaminisha kuwa chadema bado INA Sera ya kutimua mafisadi, Wakati anajua fika Mbowe anavyolalamikia utumbuaji majipu, Mara oooh sheria haifuatwi, Mara oooh hawajapewa Uhuru wa kujieleza Mara ooh wanatumbuliwa hadharani! Kha! Chadema sasa ni kichwa cha mwendawazimu.
 
Ungemuuliza BOSI wako anayelalamika hadi kwenye haki za binaadamu akiyatetea hayo hayo majizi ambayo mengi sasa yamehamia chadema. Hataku kutumbua majipu kwa nini?
Hata kuandika unatetemeka, mmeanza kuisoma namba
 
Sitashangaa Rais ajaye mwaka 2025 akawa Majaliwa

Tehetehetehe. Pole sana ndugu. Mlitaka kumchonganisha Makonda na Mzee Warioba. Aibu imewarudia wenyewe
Endelea kuweweseka
 
Hapo umenena. Hawezi kuwa consistency hata kidogo. Unajua ufisadi ni mtandao ambao haujali chama cha siasa. Lazima Mbowe aogope kwa mfano kuupinga ufisadi ndani ya serikali ya CCM kwa sababu hana uhakika kama Lowasa hayupo kwenye hiyo network au mtandao wa ufisadi huo. Ukidhani kuwa network ya Karamagi, Chenge, Rostam Aziz na Lowasa imefutika eti kwa vile Lowasa kahama CCM ni kupotoka.
Asante kwa ufafanuzi.
 
Back
Top Bottom