Kuazima gari ni ustaarabu?

Daah!! Yani mwanangu ndio umeamua kuja kunimwaga humu sio?? Poa ila nilifika na wageni wangu tulipanda punda...natania.
 
hahahaha eti ana azima gari kama fyekeo hahaha duh dongo hilo
 

kabla sijakujibu naomba uniambie ustaarabu ni kuazima kitu gani?
 
Mmmmh

Kuazimana hatari..... what if wakienda kufanyia ujambazi
 
Kwani gari ina nini usiazime mwenzio? Kama kitu cha maana sana mbona ukifa huzikwi nayo?
Cha msingi
1.mufahamiane,
2.Ajue kuendesha,
3.ujue shughuli anayoenda kufanyia.
Tuache ulimbukeni ukiwa na gari ndo kujiona umemaliza.

Kumuazima mtu gari ni sawa na kuazimisha bunduki.Anaweza kugonga mtu na kuua kisha akakimbia
Unadhani nani ataanza kukamatwa?
 
There must be a very good reason ya kumuazima mtu gari. Mie ukiniomba gari nakupeleka, najua hutakaa urudie kuja kuomba.

Naiga hii tabia yako 4 sure.. Wow I love the idea.. Asante kwa kunipa hii king'asti..
 
kabla sijakujibu naomba uniambie ustaarabu ni kuazima kitu gani?
Vipo vingi hata gari lenyewe kama ni mtu wa karibu haina shida lakini kufahamiana tu! kitaa kwa kusalimiana haitoshi kuwa sababu ya kuazima gari kwa mtu.Gari kuna mambo mengi yanaweza tokea kutokana na matumizi ya mtu mfano; limetumika kwenye tukio la wizi utakwepa vipi kesi kama hii?
 
mtoa mada kesi kama yako imenikuta jana tu.. nikampa jamaa yangu gari kuja kucheki mafuta wa hajaweka...
nikajiuliza maswali mengi sana by the way;
watz tumeathirika na ujamaaa, solution ni ukaudhu tu
 
hii thread inaleflect jinsi watu ufukara ulivyowadumaza akili.

mtu hawezi from no where aje akuombe gari tu ni lazima mna huo ukaribu, mimi sioni tatizo mtu wa karibu akiwa na shida ya gari kifamilia labda anakwenda kwenye harusi au mgeni wake atafika ubungo bus terminal usiku sana.

cha msingi unaporudisha gari yangu mshale usiwe umeshuka atleast uzidi pale nilipoachia mimi.

humu jf wengi tumezaliwa na kukulia mazingira tofauti kwa sisi wengine issue za gari tulishaonaga ni kitu cha kawaida.
 

usimpe Acha UJAMAAA WA KIPUUZI

kuna kusaidiana ila si ki hovyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…