Ni kweli Technology zinapishana na zinaendelea. Nimeangalia hizo mashine za PET na nimeona kweli zinapishana.
Ungelisoma maelezo kwenye michoro juu ungeliewewa hiyo EUro Laki moja nilimaanisha nini.
Kwa mfano mashine kubwa wanatumia Pressure 45 bars wakati hapo juu ni 15 bars.
Pia ukiangalia baadhi ya kazi inabidi ufanye kwa mikono ikiwa na maana ni Semi Automatic.
Mashine za kusaga mahindi au ngano zipo nyingi ila kuna nyingine dola Elfu mbili na za Bakhresa ni mamilioni.
Uzuri ni kuwa jamaa kabla hujanunua, anakuita na mnapanga kila kitu kwenye karatasi na unakwenda kujipanga utanunua kipi kutokana na uwezo wako mfukoni.
Ila bado ukweli utabaki palepale, hata kama bei ni hiyo Laki moja, ni lazima uwe na laki mbili zaidi ili kuweza kuendesha mtambo. Hapo kuna kutafuta maji, kusafisha maji, vibali, usafiri, kuagiza materials kutoka nje nk. Na hapo tunakwenda palepale kuwa ili uanzishe mradi kama huu, itabidi uwe na laki kadhaa. Vinginevyo utakosa hata fedha za kuletea nguzo za umeme kiwandani kwako.
sure thing mfano. Filler ya 40bpm inauzwa around $20,000. Durability yake sijui na running cost (machine nyingine zinaitaji vipuri kibao tena mara kwa mara)hii inakua complete set(conveyor+rinser+filler+capper). Label machine mtu anaweza kuamua kukata manually na kufeed akaingia cost ndogo ya heater ($2000) akaokoa $20,000 ya label machine ambayo lazima anunue baadae mahitaji yakiongezeka. Yote kwa yote uwe na mtaalam wa uchumi afanye cost analysis kabla ujatia mguu. Unaweza tembelea kiwanda cha zakaria kibaha ukajifunza wanafanyaje na changamoto.
Naomba pia uwatoe watu uoga, tujifunze kudare...mimi siuzi machine lakin ni mdau wa industry ya bevarage kwa muda sasa nimetoa offer ya bure ya consultation watu wanaogopa.