Kuanzisha kiwanda cha kutengeneza maji ya kunywa

Kuanzisha kiwanda cha kutengeneza maji ya kunywa

Mkuu, una wazo zuri sana ila swali hapa, unafikiri watengenezaji maji watakubali? Watakupa bei mbaya sana kiasi kwamba maji yako yatakuwa aghali kuzidi yao, hapo sasa sijui utashindana nao vipi kwenye soko. Labda kama kuna kampuni wanafanya hizo kazi na hawana lebo zao, basi itakuwa rahisi. Vinginevyo, IPP/Mengi au hao watengenezaji wengine, hawatataka hata kukusililiza. Hata kama ningelikuwa mie na maji yangu, nakupa bei ya kihasara.
Au wewe Mkuu ungelikubali utengeneze mshindani mwingine sokoni?

Nakubaliana na waliosema kuwa Mikoani na hasa sehemu kulipo na Wanafunzi wengi, maji yana soko zuri sana. Kwa mikoa ya Dar au Arusha, upinzani wake ni mkali sana kwa wewe unayeanza. Labda uje na maji ya radha na hii ikiwa na maana uwe na maji ya kivyako. Hapo utakuwa umeanza kutafuta wateja wako mwenyewe.
Mimi nina different concept of approach;

Unaonaje in the beginning uki negotiate on big discount na mzalishaji mkubwa wa maji ambaye yuko well established, wewe utengeneze labels zako of different brand say ''JF spring water'' then anazipack kwa labels zako halafu unatest soko limekaaje kwa say miezi 6 ? na kuweza kupata experience wakati huohuo, hapo risk of investment itakuwa very low,wakati wowote unaweza ku pull out mambo yakikaa vibaya...ni idea tuu.. samahani wakuu kuchanganya kiingereza na kiswahili ..
 
Ni wazo zuri na hasa kama utaweza kuyaprocess ili yadumu siku nyingi bila ya kuwekwa kwenye friji.

Hapo utatengeneza sana Mkuu kwani maziwa mengi ni yale unanunua na lazima unywe leo - Ninavyofahamu. Sijui kwa sasa hali ikoje kwani si mwenyeji wa sehemu nyingi.
Mimi nina wazo la kusindika maziwa fresh na mtindi ya ng'ombe wa kienyeji. Eti jamani inalipa?
 
Mkuu inategemea. Ila siyo bei nafuu. Kama unahitaji kweli, ninamfahamu mtaalamu mmoja hapa anaweza kukufungia mtambo mzima kwa bei kati ya Euro 50,000 na Euro 100,000. Itategemea na ukubwa wa mtambo.

..Duh! mbona ghali hivyo? au ndio biashara.. tulishawahi kuwasaidia wahanga mashariki ya mbali reverse osmosis desalination plant (suitable for 400 families) kwa gharama isiyozidi $30,000..
 
Hiyo 5 M kwa bei ya kununua tu au na kutuma? tuseme iwe kwenye 3M ambayo inaleta kama US $ 2,000. Nafikiri unaweza kupata mashine nyingi tu. Ila sasa sijui unataka kutengeneza nini. Kaa ufikirie na ukishapata jibu, nitumie nikutafutie. Ila nina wasiwai kuwa nyingi zitakuwa ni nusu automatiki yaani kazi nyingine ufanye kwa mkono.

Hizi zinazojiendesha zenyewe mara nyingi zinakuwa na bei kubwa sana.
Hivi mkuu Stiven huko ulipo siwezi kupata kamashine chini ya m5 kanakoweza kutengeneza bidhaa zozote ambazo jamii inaweza kuzitumia?
 
Hiyo 5 M kwa bei ya kununua tu au na kutuma? tuseme iwe kwenye 3M ambayo inaleta kama US $ 2,000. Nafikiri unaweza kupata mashine nyingi tu. Ila sasa sijui unataka kutengeneza nini. Kaa ufikirie na ukishapata jibu, nitumie nikutafutie. Ila nina wasiwai kuwa nyingi zitakuwa ni nusu automatiki yaani kazi nyingine ufanye kwa mkono.

Hizi zinazojiendesha zenyewe mara nyingi zinakuwa na bei kubwa sana.

Mkuu
Kwa wastani inagharimu kiasi hasa kwa pesa ya Tanzania mpaka Ifungwe kiwandani?

Mashine ambayo ni Automaticaly.
Asante.
 
Mkuu, hiki ni kiwanda cha kuzalisha maji ya chupa. Chupa zinatengenezwa hapohapo na kujazwa maji. Pia kumbuka jamaa anafanya kila kitu na wewe hadi anahakikisha kiwanda kinafanya kazi. Hata hivyo sijasema kuwa huyu jamaa ni Mhandisi pekee na fundi wa kutengeneza hizo mashine za kujaza maji.

Pia unaweza kununua China kwa bei nafuu sana ila huna uhakika itadumu kiasi gani na huna garantii.

Kama nyie mna bei nafuu, basi mwambie jamaa aje anunue kwenu. Sifurahii kuona mtu anatoa fedha nyingi kwa kitu kilekile wakati anaweza kununua kwa bei nafuu kwenu. Kama mna bei nzuri na mashine zenu ni imara na mnatoa ushirikiano mzuri kwa wateja wenu, basi mwandikie jamaa Email aje anunue kwenu.

Katika hii biashara, mie sihusiki. Mimi siyo mtu wa kati na mtu akifanikisha biashara yake na akanikumbuka kwa asante, basi ntashukuru ila sintakuwa na masharti yoyote kuwa ni lazima nipewe asante. Nikishamkabidhi kwa Mhusika, basi mie nanawa mikono kwa lawama au asante yoyote.

Pia kumbuka, mtambo unaoweza kuzalisha tuseme chupa 1,000 kwa saa, ina maana kwa siku utatengeneza chupa kama 20,000. Hizi chupa zitatumiwa na familia ngapi?
Nina wasiwasi unaongelea kitu kingine kabisa hapa. Huo mtambo wenu ni wa kuondoa chumvi kwenye maji. Huu unachukua maji yaliyosafi tayari na kuyafunga kwenye chupa. Ina maana kama hayo maji nyie mnazalisha, inabidi sasa ndiyo uje huu mtambo na kufungwa ili uzalishe maji ya chupa.
..Duh! mbona ghali hivyo? au ndio biashara.. tulishawahi kuwasaidia wahanga mashariki ya mbali reverse osmosis desalination plant (suitable for 400 families) kwa gharama isiyozidi $30,000..
 
Mkuu, inategema unataka mashine gani. Zipo mashine nyingi sana duniani kuanzia mashine ya kutengeneza kahawa, kusafisha nyumba, kutengeneza magari, vinywaji, vyakula nk. Hivyo, gharama zinategemea unataka ktengeneza nini na huo mtambo una ukubwa gani nk.

Huo wa 5M, nafikiri hata huhitaji kuufungwa kwa sababu itakuwa ni kipande kimoja tu.
Mkuu
Kwa wastani inagharimu kiasi hasa kwa pesa ya Tanzania mpaka Ifungwe kiwandani?

Mashine ambayo ni Automaticaly.
Asante.
 
duh,yaani mie nilikuwa najua kama bilioni moja au rahisi milioni mita nane hivi.
Yaani steven unatisha kaka.yaani hata maswali hakuna,maana data kamili.

Ngoja mie nifanye mchakato mwakani nitakutafuta nime save email yako.

Au wana jf mnaonaje tujipange watu kama 100 hivi then tuanzishe sehem kiwanda chetu.
Hili ni wazo tu,mie naweza kutoa mpaka share ya 15m.
Ni wazo tu jamani,maana tutumie muda humu kwa faida.
Tunaweza kuweka utaratibu wa kuwa na wamiliki kisha humuhumu tukaajiri watu wa marketing wenye taaluma na uzoefu.na pia humuhumu tukapata suppliers.
Zanzibar_spice umefikiri vyema sana enlist me by jan 2015, <15m>
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, inategema unataka mashine gani. Zipo mashine nyingi sana duniani kuanzia mashine ya kutengeneza kahawa, kusafisha nyumba, kutengeneza magari, vinywaji, vyakula nk. Hivyo, gharama zinategemea unataka ktengeneza nini na huo mtambo una ukubwa gani nk.

Huo wa 5M, nafikiri hata huhitaji kuufungwa kwa sababu itakuwa ni kipande kimoja tu.


Nataka ya kuzalisha Maji pamoja na chupa zake na lebo.
 
Bei nimeweka tangu mapema, bei kati ya Euro 50,000 na Euro 100,000.

Sijui bei ya Euro kwa sasa Tanzania ikoje. Ukipata hiyo bei, basi zidisha kwa fedha hizo hapo juu na utapata bei ya mtambo. Ila nafikiri kwa Prado Mpya zinavyouzwa huko, kama unaweza kununua gari jipya, basi unaweza pia kununua huu mtambo.
Nataka ya kuzalisha Maji pamoja na chupa zake na lebo.
 
Saafi sana aisee,nimeipenda hii idea,baada ya kusoma comments naomba nifanye majumuisho machache mpaka kifikia hapa

1. Wazo la kuwa na brand yetu na kutumia makampuni makubwa kutufanyia process si nzuri sana.Lady jay dee hakufanikiwa sababu alitumia hii na Mohamed enterprises ndio alikuwa anawatumia mwisho wa siku inaonekana kama kulikuwa na kuhujumiwa.So kuwe na lengo la kufanya our own processing which means expensive and high risk

2. Hoja ya ushindani wa biashara Dar na kuwa mikoani kuna uhitaji mkubwa,hii imepita hivyo target ni mikoani.Swala ni mikoa ipi? Mimi naona kanda ya kati itafaa,Dodoma,Singida,Tabora na Kigoma.

3. Uchangiaji wa capital,15M mkiwa watu kumi ni 150M,ambayo kwa haraka haraka kama sijakosea hesabu za exchange rate inatosha kufunga huo mtambo.So kama kila mwaka mwanahisa atatoa 15M then in two years kiwanda kitakuwa up and running

Naunga mkono hoja na nipo kwenye mkakati kama mpo serious.Nawasilisha.


Duh,yaani mie nilikuwa najua kama Bilioni moja au rahisi milioni mita nane hivi.
Yaani Steven unatisha kaka.Yaani hata Maswali hakuna,maana Data kamili.

Ngoja mie nifanye mchakato mwakani nitakutafuta nime save email yako.

Au wana JF mnaonaje tujipange watu kama 100 hivi then tuanzishe sehem kiwanda chetu.
Hili ni wazo tu,mie naweza kutoa mpaka share ya 15m.
Ni wazo tu jamani,maana tutumie muda humu kwa faida.
Tunaweza kuweka Utaratibu wa kuwa na Wamiliki kisha humuhumu tukaajiri watu wa Marketing wenye taaluma na uzoefu.Na pia humuhumu tukapata suppliers.
 
Steven Sambali Nimependa mchango wako sana ..nisaidie kujua mtambo wa kuzalisha chupa peke yake ni shilling ngap?..chupa za maji cz wa production ya maji makubwa ninao tayar
 
Last edited by a moderator:
Sawa mku.
Haya nataka tu update list ya owners on daily basis na pia kiasi cha wastan wa shared capital(Note that this is a really serious issue)

1 :Zanzibar Spices : Tsh:15,000,000 (hali ikiruhusu nawezakuongeza)
2 :Majigo :Weka kiasi mkuu

Current Total Capital:Tsh:15,000,000


Pia Pendekezo la Jina la Maji:
-Jamii Pure Drinking Water
-JF Pure Drinking water(ila hapa lazima tuombe kibali kwa JF Owners,najua hawa ni wetu tu watatukubalia)
-JF Members Drinking Water (the same)

Ifahamike kwamba inatakiwa ndani ya miezi sita tuwe tayari kunauelekeo ili kuindia awamu ya pili.
Concept hii napendekeza iwe ya mwaka mzima ili by January kwa waliotayari tuanze baada ya kupitia michajkato mingine kama vile,mkoa wa kufungua kiwanda kidogo hiki,na mambo mengine yakiutawala.

Pia nakaribisha wataalam wa mambo ya uchambuzi wa miradi na Marketing pia watupe uzoefu wao,maana najua mmo humu na mchango wenu wa mawazo ni muhim sana.Ili penye makosa muweze kukosoa na penye ushauri muweze kuweka.

Xidian 15,000,000
 
Humu yanaletwa mawazo mengi na watu wanapokea kwa Shangwe tatizo Utekelezaji cjui tutatokaje Eneo hilo,,,,! Hili ni wazo zuri sana Ukichukulia humu kuna watu wakila FANI cdhani km kuna kukwama! Nataka kujua jambo hasa kwenye mambo ya Production ya Maji kuna kipindi nilikuwa nakunywa Maji nadhani yanatengenezwa ARUSHA yale maji yalikuwa na Test ya matunda km EMBE ,NANASI nk,hv product km ile inatenezwaje? kwaanaejua msaada wandugu!
 
mm natumia mikono na ni mfanyabiashra mdogo sana
ngoja nifanye hivyo kama ulivyonishauri kisha kama
itatokea product imekuwa kubwa nitawasiliana nawe

Mashine kama hizo zipo nyingi sana. Ila cha kujiuliza, kwa sasa unataka kweli hiyo mashine? Je utengenezaji wako na kujaza asali kwenye chupa zako unakufanya kwa mashine kiasi kwamba unahitaji hiyo mashine iweke lebo? Kama unazalisha kwa kutumia mkono, basi ningelikushauri wewe tengeneza hizo lebo/chapisha na weka. Pia hata watoto/vijana/akina mama wanaweza wakaweka hizo lebo. Vijana watafurahia wanapata kazi na hasa wanafunzi wa Primary au Secondary za kata na wewe utatupia pesa kidogo sana kwa kazi hiyo. Mashine pia inaweza kuhtaji umeme ambao kwa mikoa kama ya Tabora ambako mimi natoka, umeme ni matatizo sana. Ulaya kazi kama hizo zinafanywa sana na Wanafunzi ili wajipatie kipato kidogo.

Ila kama kweli wahitaji, basi naweza kukutafutia na kukujulisha bei zake zikoje - Fikiri tena na nijulishe.
 
Latest:
1 :Zanzibar Spices : Tsh:15,000,000 (hali ikiruhusu nawezakuongeza)
2 :Xidian : Tsh:15,000,0000

Current Total Capital:Tsh:30,000,000


Tunakaribisha Stake Holders wengine walio Serious

Wazo lako ni zuri ila mimi naushahuri, Tuachane na hii Biashara ya Maji na tufanye Biashara ya Kukamua Mafuta ya alzeti maana huu Mtambo sio bei kubwa sana na kwa sasa mafuta ya Alzeti ni Dili kumbuka wamepigiga marufukiu uagizaji wa Mafuta kutoka Njee.
 
Mimi nina wazo la kusindika maziwa fresh na mtindi ya ng'ombe wa kienyeji. Eti jamani inalipa?
Hebu Steven tusaidie hapa cost za mashine ya kiwanda kidogo cha kusindika maziwa, au hata coldroom peke yake.
 
Back
Top Bottom