Kuanzia Leo, nampa Tuzo ya Heshima Pascal Mayalla

Kuanzia Leo, nampa Tuzo ya Heshima Pascal Mayalla

Pascal kuwa na mwenye upeo mzuri na mchambuzi bora, no question about it.

Ningependa siku moja Pascal angekuwa na kipindi chake maalum cha watu wenye uchambuzi wa mambo mbalimbali wenye upeo wa hali ya juu. Hakika kipindi hicho kingejiuza vizuri, na kingekuwa na mchango mkubwa kwa jamii ya Tanzania na Afrika.
Una maanisha , Nape, Bashe, Mtatiro, Zito, Mnyika na CEO mmoja alimaarufu kama mafuru au Mafruki theni mada unaiweka mezani bila kuwa na upande?? Ongeza list hapo. Hata mimi nitachangia hicho kipindi.
 
Hata mm namkubali na naamini ni mzalendo haswaa. Hiyo tuzo anastahili na nyongeza juu. Japo toka ahojiwe na kamati alibadilika kiasi. Huenda alienda kuyajua tusiyoyajua. Heshima yake kwangu iko pale pale.
 
Kwa upande wangu huwa ni vigumu sana kumsifia mtu bila kujiridhisha vya Kutosha,

Nina sababu za msingi za kufanya nimuheshimu nimuangalie kwa Umakini huyu mtu anayeitwa Pascal Mayalla

We unayesoma hapa waweza kuwa unadhani natania lakin nauliza swali,

1. Unakumbuka swali lolote lile aliloulizwa Rais Magufuli wakati wa mikutano wake na waandishi wa habari? Kama walikumbuka ni lipi? Na kwanin usikumbuke ya wengine ukumbuke ilo?

Mi nakumbuka kulikuwa na mwandishi mmoja aliuliza swali kwamba Mheshimiwa ametoa wapi mamlaka ya kukataza mikutano na kuingilia mamlaka nyingine kama Bunge?

Kuuliza swali kama ilo mbele ya jiwe ni risk kubwa mno, nadhani mnajua madhara yake, lakin Pascal Mayalla ni mtu pekee aliyeuliza swali la maana na mkuu akajichanganya,

2. Unakumbuka aliyetabiri au alisema kwamba Magufuli ndo rais ajaye? Ilikuwa mwaka 2014 watu wengi wakiwaza kwa matumbo yao kujazwa na Membe na Lowassa, lakin Huyu alisema japo alificha sababu zake, na alibezwa na kutukanwa,

3. Huyu wajua kwamba aliwahi kudokeza kwenye bandiko fulani kwamba Lowassa akifukuzwa CCM atahamia CHADEMA na watu wakamtukana kwamba nani ampokee fisadi? Lakin ikawa mpaka Leo wako kimya

4. Kuna uzi ameuandika mwaka 2016 kuhus mtatiro kutoweza kutatua matatizo ya CUf na kienda mbali zaid kwamba msishangae hata kabla ya 2020 Mtatiro anaitosa Cuf, watu wakamtukana na kusema anamuonea wivu mtatiro,.leo yametimia,

Kwakweli sijaona mwandishi Pasco Mayalla,
Wapo kina Mzee Mwanakijiji, ila wao staili yao ya kuandika so ya ushauri na maono, na kuuma na kupuliza kama Mayalla,

Maana Mayalla Leo anaweza weka uzi timu Lumumba wakamtukana kweli, kesho akaweka akatukanwa na CHADEMA, yaan ni mwandishi wa hivo hiyo yote ni kwamba anaandika ukweli,

5. Mayalla kuna tunaohisi ni wale watu wa Kijitonyama maana ukitaka habari za ndani zaid muulize Mayalla, anaandika haogopi mtu,

6. Ndugai anamjua sana Mayalla bahati nzuri kwenye kamati iliyomuhoji Bungeni kuna mtu alivujisha siri kwamba Mayalla kawajibu kisomi mpaka wakaanza wao kama wanasikiliza story toka kwake badala ya kumuhoji, na mbali zaid akaongeza marafiki ndani ya kamati ile

Mi nakupa tuzo ya heshima hapa JF bwana Pascal Mayalla popote ulipo,

Nathan JR
Ni kweli kabsaa, na ndio maana hata mimi nimuomba atudaidie kuchambua nin kitatokea huko mbeleni iwapo wapinzani watanunuliwa wote, je kuna nchi iliwahi kufanya hivo ? mara nyingi tumezoea kuona vyama pandikizi kama ACT au CUF lipumba.
 
Naunga mkono hoja, i really appreciate paschal Mayala, huyu Jamaa Kuna post yake ilikuwa inahusu nguvu ya asili aliyonayo kila mtu, Hakika alibadili Sana mtazamo wangu.
Huyu Jamaa anastahili Sana.
Tunaomba atutabilie nini kitatokea endapo viongozi wa upinzani watakimbilia chama tawala.
 
Huwa silipiti bandiko lake na mala nyingi ulisoma mala mbilimbili.
Huyu ni nguli wa kweli.
Tahadhali: usivimbe kichwa kisije pasuka.
 
Mkuu Pascal Mayala ni kada mtìifu wa lumumba ila ana hofu ya Mungu kidogo anapenda haki na ukweli tofauti na lumumba wenzie ambao wao ni kusifu tu,ni mwandishi mzuri sana lkn kuna siku aliniuzi sn alikua TBC akawa ana muhoji sijui Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi NEC kabla ya huyu mpya mayalla alisema "sasa hakuna ubishi kumbe ukweli magufuli alipata kura million 8 na ndo raisi wa Tz hao wengine waendelee na rais wao wa moyoni ila rais wa URT ni mmoja tu magufuli nyie ambao hamridhiki endeleen na rais wenu wa moyoni"sasa nikajiuliza ana conclude kama nani ?au na yeye amejipa mamlaka ya kimahakama..kipindi kile lkn ndo ilikuwaga kipindi cha tumbua tumbua sasa sikujua nini kilimpata maana sijamuona tena TBC
 
Pasco hatabiri hayo, ila anapata udambu pale lumumba wa wale wazee waosha magari
kiukweli Pascal Mayala anapiga kotekote, tatizo lenu makamanda hamtaki mguswe kabisaa...hata kwenye mapungufu ya wazi kabisa, nyie mnataka kusifiwa tu!

Badilikeni, mkikosolewa kubalini mfanyie kazi mapungufu kisha mbadilike - hakuna aliye timilifu, hata huyo jiwe mwenyewe anayo mapungufu kibao lakini hata mazuri pia anayo!!!.
 
Back
Top Bottom