Kuanzia IGP Harun Mahundi aondoke Polisi imekuwa mafia

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,753
Mimi ni mtoto wa Polisi na mzee wangu alikuwa mkubwa sana kwa miaka mingi kwenye jeshi hili. Kuanzia IGP harun mahundi aondoke 1996 Polisi imegeuzwa genge la wahuni na mafia.

IGP Mahita ndiye aliye anzisha genge la umafia Polisi na viongozi wa serikali wamekuwa wakifumbia macho makusudi kwasababu genge hili limekuwa likitumia kuwasaidia kisiasa na kuwazuia wapinzani na kuiba kura.

1. Kwanza walianzisha mifuko ambayo haipo kisheria ambayo inakata makato kwa kila polisi mfano kuna mfuko wa kufa na kuzikana ambao Polisi wa chini hawaruhusiwi kuhoji pesa inatumikaje na wala hawapati chcochote! hata wakifiwa

2. Kikosi cha ulinzi maalamu kama wa banks na sehemu nyeti kampuni zinalipa Polisi lakini sio serikali wala Polisi wengine wanajua pesa inaenda wapi.

3. Rushwa barabarani kila RPC anapata chake kutoka kwa mkuu wa traffic wa mkoa na kati ya hizo kuna fungu linaenda kwa wakubwa makao makuu na hakuna mtu wa kuhoji

4. Kuna pesa inategemea kuletwa ya rushwa kutoka kwa RPC wa mikoa ya mpakani. Hii ruhswa na kuingiza na kutoa magendo bila kodi. RPC asipo tuma pesa anahamishwa haraka sana. Mikoa kama Kagera, Mwanza, Mara, Tanga, Mbeya, Kilimanjaro na Arusha wanahusika na hili. Yaani ilifika wakati RPC akipandishwa cheo na kupekwa makao makuu Dar anachukia kama kapata msiba kwasababu hakuna rushwa makao makuu kama mikoani.

IGP mwema alijaribu kusafisha lakini hajafanikiwa kwasababu mitandao ilikuwa imeota mizizi sana na utamaduni wa rushwa umekuwa mkubwa sana kwa muda mrefu. Bado kuna wizi mkubwa kwa Polisi wa railways, vitengo vya magari na spair parts.

Polisi ni lazima ivunjwe na kuundwa upya na Polisi wa chini wawe na uhuru wa kusema maovu bila kuogopa mabosi wao. Lakini kuwe na uangalizi maalumu kama Bodi ambayo iwe na wanasheria na ofisi ya mkaguzi mkuu na iruhusiwe kohoji Polisi wa kawaidia bila vipingamizi kwa wakati wowote.

Yaani Sirro nyumba yake ya Musoma ilikuwa inasimamiwa na maafisa wa Polisi kwenye ujenzi wakati ni nyumba binafsi. Lakini imejegwa na wadhamini. Tibaigana alijengewa mpaka Hoteli na wadhamini waziwazi. Hawa wadhamini ni watoa rushwa na wenye magendo

Hakuna kitengo wafanyakazi wanafanya kazi kwa shida kama Polisi wa chini. Lakini hakuna kitengo wakubwa wanaishi vizuri kama Polisi Mahita alikuwa na helikopta yake kabisa ya kumpeleka Morogoro kwao weekend

Naomba niongezee kitu kingine: kuna magari yanashikwa na Polisi ya wizi au wauza madawa yanataifishwa. Je umewahi kusikia mnada wa magari ya Polisi. Nakumbuka wakati mzee wangu akiwa RPC zamani tulishangaa tumeletewa Toyota 4 runner tukaambiwa ni magari ya wizi ya mnada na mzee kalipa laki moja tu kwa gari mpya. Halafu RCO naye alipewa gari zuri yaani ulikuwa ni utamaduni na hakuna wa kuuliza wala kuhoji

Hakuna kiongozi amesaidia Polisi huko nyuma kama Mahundi ambaye alikuwa nasifika kwa kuwa na akili sana.

Kikwete+mahundi.jpg
1680534134152.jpeg


Mwanzilishi wa mafia ya polisi

1680534343704.jpeg
1.JPG
 
Ndugu yangu mmoja amekuwa mtu wa mwisho kwenye ukoo wetu kutumikia TanPol baada ya "kuokoka" kwa kupata nafasi ya kusoma MBA na kuchomoka kabisa upolisi .

Anasema kama unamjua Mungu kweli na kulishika neno na mafundisho yake,huwezi kufanya kazi TanPol.
 
Wakati huohuo wazee wa kaunda suti wapo huko, kuanzia DSOs na RSO wao, wamejiongezea na nafasi za ma DAS na RAS. Na wana maafisa vipenyo sijui vificho kibao huko sehemu, lakini wapi.

TAKUKURU ipo kila wilaya, lakini hawa walishaamua kutowafuatilia polisi, kwasababu mfumo wa mashtaka umejaa polisi na ikiwaletea unaa hawakupi ushirikiano 😎.

Waadilifu kidogo hasa mipakani ni watu wa TPDF, lakini ndio vile tena hawawezi ku overstep majukumu yasiyo wahusu, lazima waishi na watu vizuri.

Mageuzi yanaanzia juu kwenda chini, sio vibaya serikali ikampa u IGP Hamduni au Diwani Athumani. Hao jamaa ukileta ujinga hauna kazi, roho mbaya lakini watu wa haki.
 
Polisi wana maisha magumu sana hivyo rushwa ni jambo lisilo kwepeka.

Watu wana maisha magumu, mishahara midogo halafu wanasimamia makosa ya jinai watawezaje kukwepa vishawishi?

Polisi hawana scheme of service inayoeleweka na iliyo wazi hata Rais Samia alisema, unakuta mtu ni mzee wa miaka 60 ama 59, amefanya kazi polisi miaka 30 ama zaidi lakini ana cheo kile kile alichoajiriwa nacho miaka 30 iliyopita.

Career growth ndani ya polisi ni ngumu sana kuliko jeshi la wananchi, hakuna uwazi nani apande daraja nani asipande.

Kuhusu umafia, nakubaliana na wewe, Mahita alianzisha umafia ama vikundi vya kimafia ndani ya jeshi la polisi. Jeshi letu pia linaongozwa kimafia zaidi, wadago wanaumia zaidi.

Tunahitaji kubomoa na kusuka upya jeshi la polisi, kuwe na uwazi, jeshi lijiendeshe kitaalamu, waajiri professionals na wataalamu na wasomi.
 
Ni vituko hii nchi eti kamanda wa TAKUKURU wa mkoa ana mshahara wa Milioni 3.8 halafu, meneja wa TRA wa mkoa ana mshahara wa zaidi ya 9M halafu huyu wa TAKUKURU ndio aende kumkamata meneja wa TRA.

Mshahara wa mkuu wa takukuru wa mkoa ni mshahara wa kufikia kwa maafisa wa chini kabisa wa TRA, TANESCO na mashirika mengine makubwa ambayo tunalalamikia yamejaa rushwa halafu anaesimamia rushwa ana mshahara mdogo, hiyo rushwa ataisimamiaje huku ana njaa.

Takukuru iko kama geresha tu, hatuko serious kwenye kupambana na rushwa ndio maana kesi nyingi za takukuru ni za watendaji wa vijiji, hakimu wa mahakama za mwanzo, nk.
 
Back
Top Bottom